Ulishawahi kukutana na mwanamke/mwanaume mtandaoni akaku-prove wrong kinyume na matarajio kabla ya kuonana live?

Makutano ya mke/mume huwa yana mambo unashindwa kuelewa.. Yule unayempania sana inakuwa chenga
 
mkuu ungezea nyama sentensi yako ieleweke.

nilishindwa kuelewa nini?
 
Watu waliozoea stori za masikitiko wakiona mtu analeta stori kuwa anafuraha na anaenjoy, huleta maneno ya ajabu ajabu 😏
wapo wanakutana na utofauti mkuu, wanaishia kukimbiana
 
Baada ya kujikita kusoma sana nyuzi za watu na mimi leo naandika uzi wangu.

Miaka mitano huko nyuma nilikuwa na tabia ya kutumia ukurasa wangu wa facebook kushare mambo yanayohusiana na utaalamu wa fani yangu, na watu wengi wakawa wanachangia maoni

Siku moja nikapokea text messenger kutoka kwa mtoto wa kike akinisalimia na kuhitaji msaada wa kimasomo, alikuwa anasoma telecom pale udsm.Tukaelekezana, tukaachana kwa hiyo siku. Mimi kama mimi sikuwa na interest nae kabisa na kadri siku zilivyokuwa zinaenda ndivyo nikawa napokea text za kunisalimu messenger zingine nikawa sizijibu hata zaidi ya mwezi.

Ukapita mwaka, ukaenda wa pili akawa anajiandaa kumaliza chuo na mimi nikawa siandiki tena kwenye wall yangu ya fb kama mwanzo kulingana na kutingwa na mambo yangu binafsi lakini bado akawa ananitext messenger, sasa kuna siku usiku nikiwa nimepumzika najiandaa kulala nakutana na mlolongo na message fb kutoka kwake mojawapo akiwa analamika kwamba simjibu message zake na kuna somo limemkamata anahitaji nimsaidie. siku hii ndio niliyojikuta napitia kwenye ukurasa wake kuangalia picha zake, nikakuta mara ya mwisho kuweka picha zake ni kama miaka 4 iliyopita halafu hata zilizopo ni za kawaida sana.

Kumbuka kipindi chote hiki sikuwahi hata kumfikiria, nilijua tu ni wale wanawake wagumu wa fani zetu za kiinjinia..Ule usiku tukaongea nae sana messanger pamoja na mambo mengine tukabadilishana mawasiliano rasmi, Baada ya mda akafanya UE akawa mtaani rasmi. Kipindi chote hiki hatukuwahi hata kuombana picha japo tulikuwa tunachart what'sapp, profile yake na yangu hakukuwa na picha zetu, tulikuwa tunawasiliana tu kawaida.

Alipomaliza akataka tuonane, Yeye ndiye aliyeomba hii appointment na mara kadhaa nikawa navunja ahadi ya kuonana. Sasa kuna siku ambayo tulipanga tuonane, Kesho yake ilipofika mimi sikuona umuhimu kwanza ndio alikuwa anamaliza shule na pili picha zake kule fb nilimuona ni mtu wa kawaida hata kimapenzi hakunivutia, sikuona cha muhimu kutoka kwake, na wala sikumpigia simu ili kumuelekeza sehemu ya kuonana badala yake nikawa niko kwangu na washkaji zangu tunapanga mikakati yetu.

Mida ya saa nne akanipigia simu anajiandaa kuja, Pale kwangu kuna rafiki yangu nilikuwa nae kiwembe sana nikampanga na kumuelezea kila kitu na jinsi tulivyokutana na huyo mdada nikamueleza kwamba nitamtambulisha kwake kama akivutiwa aweke mitego yake na akija kufanikiwa sio mbaya akawa koloni lake mimi siko tayari, saa sita napokea simu yake akiniambia tayari ashafika yale maeneo. Mimi na rafiki yangu tukatoka kwenda kumpokea, kufika pale hatuoni mtu ikabidi tumpigie simu, akatuelekeza mahala alipo.

Alisindikizwa na dada yake, alimpa lift ili amuache pale yeye aendelee na safari zake, kufika kwenye gari alilotuelekeza, walipaki sehemu ya kituo cha mafuta na yeye akawa tayari ameshaniona maana nilikuwa naongea nae kwa simu, Nikashangaa kuona mlango wa gari unafunguliwa Aisee alitoka mle mtoto mkali sikutaka kuamini macho yangu kama ndio yeye, tukasalimiana na dada mtu naye ni kisu hatari baadae dada mtu akatuacha akaendelea na safari zake.

Huyu mdada ni mzuri sana, mpole, mcheshi, anaongea taratibu. Na ahadi niliyompa rafiki yangu nikaivunja rasmi.
Sasa tukawa karibu zaidi tofauti na mwanzo, Niliridhika nae na nilipojaribu kumlinganisha na wale niliokuwa nao kwenye mahusiano sikuona kama wanamfikia iwe kwa tabia, uzuri, utafutaji hata uthubutu na hana ulimbukeni wa pesa, kwao amezaliwa amezikuta zipo nyingi tu.

Nikawa natumia pesa kwake kwenye kumnunulia zawadi na kumtoa out za gharama na wala sihisi kama nimepoteza.

Ikawa ni kazi nyepesi tu kuweka maombi yangu kwake, kama kawaida ya wasichana chenga za hapa na pale hatimae akaingia kingi mpaka leo ndio mke wangu.

Amenizalia watoto mapacha warembo kama yeye na familia yangu ina furaha sana.
Familia yao ina watoto sita, wawili wa kiume na wanne wa kike na wote ni visu balaa, mungu anajua kuumba aiseee
Hongera mkuu ila mambo ya zarau zarau sio mazur muda mwingne
 
Nilikutana na mdada humu jf ni mzuri pisi flani Kali hivi ni rafiki angu tu mkubwa [emoji3].maana wengine wanakuwa na mentality huku mkikutana hakuna urafiki ni kulana tu

Nanii najua utapita hapa mi chapombe nakusalimia sijakutenga rafiki
 
Nilikutana na mdada humu jf ni mzuri pisi flani Kali hivi ni rafiki angu tu mkubwa [emoji3].maana wengine wanakuwa na mentality huku mkikutana hakuna urafiki ni kulana tu

Nanii najua utapata hapa mi chapombe nakusalimia sijakutenga rafiki
Mzee Hilo cheko hujala kweli😃😃

Urafiki wa demu mkali Mimi siwezi mkuu haha.

Kama unataka uwe rafiki yangu halafu basi uwe mbovu halafu ni demu mgumu flani lakini type za kina mobeto haiwezekani hata kwa kabali haha
 
Kuna dada mmoja nilikutana naye humu jf , tukawa tunachart za hapa na pale .. akanipa number kile nikimchek dp whatsap giza .... Hhalafu anasisitiza tuonane ... Siku moja nikaona sio mbaya akafunga safari from mbeya to dsm ... Nilipomuona ... Nadhani alihic kitu .. kbs alikuwa mbaya kama mwaname .. halafu kila kitu anajidai anafahamu kisa alisoma pale UDSM ..

Ule usiku nilijikaza kwenye mechi alikuwa yuko poa anajituma haswa ila usoni hapana ... Alivyoondoka kurudi mbeya nikampotezea kbs ... Anajitahidi sana kunitext wapi

Nimeona kafungua uzi wake anatafuta mwanaume wa kumuoa ... Nikapita kama si muoni maana muda wote anansisitiza ndoa kisa umri umri umemtupa mkono ... Niliona kama nimepata bonge la hasara
 
Hahaha pamoja na mimi kuwa baharia mwandamizi najua ni vigumu kuamini sijafanya hivyo hata wazo ilo sina [emoji3] .

Ni suala la mda itatokea tu siku hatakuwa upo interested nao kivile utawaona wakawaida na utakuwa na urafiki nao hao wakali kama kina mobeto bila hisia kuingilia kati
Mzee Hilo cheko hujala kweli[emoji2][emoji2]

Duh..!
cariha pita hapa
 
Hahaha pamoja na mimi kuwa baharia mwandamizi najua ni vigumu kuamini sijafanya hivyo hata wazo ilo sina [emoji3] .

Ni suala la mda itatokea tu siku hatakuwa upo interested nao kivile utawaona wakawaida na utakuwa na urafiki nao hao wakali kama kina mobeto bila hisia kuingilia kati
Kwangu haiwezekani mkuu
 
Hongera yako!

Miaka kadhaa nyuma nilikuwa nikiwasiliana na dada mmoja Fc. Yeye alikuwa Dar na mimi mkoani. Tulikuwa tukiwasiliana sana Messenger lakini hatukuwahi kuonana kwa zaidi ya mwaka. Aliniambia yeye ni mfanyakazi wa katika saluni moja hapo Kinondoni B. Katika ukurasa wake wa Fb alikuwa akirusha picha zake nzuri sana zenye mvuto wa hali ya juu.

Ilitokea nilipata msiba, mtoto wa dada yangu alifariki hapo Dar, hivyo nikalazimika kusafiri kwenda msibani. Nilipenda kutumis fursa hii ya msiba kuweza kukutana naye. Basi baada ya msiba nilimtaarifu kuwa ningependa kuonana naye. Nilimuomba tukutane katika mgahawa mmoja jirani na ofisi yake muda wa saa nne na nusu tupate supu kufahamiana zaidi.

Nilipofika sehemu ya tukio niliingia ndani ya mgahawa, kulikuwa na mdada mmoja ndani ya mgahawa, alikuwa na sura mbaya kumzidi marehemu Remmy Ongala! Nilijiambia hawezi kuwa huyu nilipitiliza kikaenda maliwatoni, nikatoa sauti ktk simu yangu, kisha nikatoka maliwatoni nakupiga namba ya huyo mdada na kuiweka mfukoni simu yangu.

Wakati natoka nikaona mdada kapokea simu na kuanza kuangaza huku na kule kisha akatoka nje kuangaza! Nikajiridhisha kuwa ni yeye nikaondoka eneo la tukio. Baada ya dakika kumi nilimpigia simu kumuomba msamaha kuwa nimepata tatizo na sitaweza fika eneo la tukio........nilikataa mawasiliano mazima!
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Baada ya kujikita kusoma sana nyuzi za watu na mimi leo naandika uzi wangu.

Miaka mitano huko nyuma nilikuwa na tabia ya kutumia ukurasa wangu wa facebook kushare mambo yanayohusiana na utaalamu wa fani yangu, na watu wengi wakawa wanachangia maoni

Siku moja nikapokea text messenger kutoka kwa mtoto wa kike akinisalimia na kuhitaji msaada wa kimasomo, alikuwa anasoma telecom pale udsm.Tukaelekezana, tukaachana kwa hiyo siku. Mimi kama mimi sikuwa na interest nae kabisa na kadri siku zilivyokuwa zinaenda ndivyo nikawa napokea text za kunisalimu messenger zingine nikawa sizijibu hata zaidi ya mwezi.

Ukapita mwaka, ukaenda wa pili akawa anajiandaa kumaliza chuo na mimi nikawa siandiki tena kwenye wall yangu ya fb kama mwanzo kulingana na kutingwa na mambo yangu binafsi lakini bado akawa ananitext messenger, sasa kuna siku usiku nikiwa nimepumzika najiandaa kulala nakutana na mlolongo na message fb kutoka kwake mojawapo akiwa analamika kwamba simjibu message zake na kuna somo limemkamata anahitaji nimsaidie. siku hii ndio niliyojikuta napitia kwenye ukurasa wake kuangalia picha zake, nikakuta mara ya mwisho kuweka picha zake ni kama miaka 4 iliyopita halafu hata zilizopo ni za kawaida sana.

Kumbuka kipindi chote hiki sikuwahi hata kumfikiria, nilijua tu ni wale wanawake wagumu wa fani zetu za kiinjinia..Ule usiku tukaongea nae sana messanger pamoja na mambo mengine tukabadilishana mawasiliano rasmi, Baada ya mda akafanya UE akawa mtaani rasmi. Kipindi chote hiki hatukuwahi hata kuombana picha japo tulikuwa tunachart what'sapp, profile yake na yangu hakukuwa na picha zetu, tulikuwa tunawasiliana tu kawaida.

Alipomaliza akataka tuonane, Yeye ndiye aliyeomba hii appointment na mara kadhaa nikawa navunja ahadi ya kuonana. Sasa kuna siku ambayo tulipanga tuonane, Kesho yake ilipofika mimi sikuona umuhimu kwanza ndio alikuwa anamaliza shule na pili picha zake kule fb nilimuona ni mtu wa kawaida hata kimapenzi hakunivutia, sikuona cha muhimu kutoka kwake, na wala sikumpigia simu ili kumuelekeza sehemu ya kuonana badala yake nikawa niko kwangu na washkaji zangu tunapanga mikakati yetu.

Mida ya saa nne akanipigia simu anajiandaa kuja, Pale kwangu kuna rafiki yangu nilikuwa nae kiwembe sana nikampanga na kumuelezea kila kitu na jinsi tulivyokutana na huyo mdada nikamueleza kwamba nitamtambulisha kwake kama akivutiwa aweke mitego yake na akija kufanikiwa sio mbaya akawa koloni lake mimi siko tayari, saa sita napokea simu yake akiniambia tayari ashafika yale maeneo. Mimi na rafiki yangu tukatoka kwenda kumpokea, kufika pale hatuoni mtu ikabidi tumpigie simu, akatuelekeza mahala alipo.

Alisindikizwa na dada yake, alimpa lift ili amuache pale yeye aendelee na safari zake, kufika kwenye gari alilotuelekeza, walipaki sehemu ya kituo cha mafuta na yeye akawa tayari ameshaniona maana nilikuwa naongea nae kwa simu, Nikashangaa kuona mlango wa gari unafunguliwa Aisee alitoka mle mtoto mkali sikutaka kuamini macho yangu kama ndio yeye, tukasalimiana na dada mtu naye ni kisu hatari baadae dada mtu akatuacha akaendelea na safari zake.

Huyu mdada ni mzuri sana, mpole, mcheshi, anaongea taratibu. Na ahadi niliyompa rafiki yangu nikaivunja rasmi.
Sasa tukawa karibu zaidi tofauti na mwanzo, Niliridhika nae na nilipojaribu kumlinganisha na wale niliokuwa nao kwenye mahusiano sikuona kama wanamfikia iwe kwa tabia, uzuri, utafutaji hata uthubutu na hana ulimbukeni wa pesa, kwao amezaliwa amezikuta zipo nyingi tu.

Nikawa natumia pesa kwake kwenye kumnunulia zawadi na kumtoa out za gharama na wala sihisi kama nimepoteza.

Ikawa ni kazi nyepesi tu kuweka maombi yangu kwake, kama kawaida ya wasichana chenga za hapa na pale hatimae akaingia kingi mpaka leo ndio mke wangu.

Amenizalia watoto mapacha warembo kama yeye na familia yangu ina furaha sana.
Familia yao ina watoto sita, wawili wa kiume na wanne wa kike na wote ni visu balaa, mungu anajua kuumba aiseee
Kwenye hii hadithi tunajifunza nini ?
 
Back
Top Bottom