Hiyo mbinu ilinisaidia mara nyingi sana, wife akianzisha fujo tu nafungua mlango natembea hatua 20 niko grocery, nikirudi ni kulala tu.Wala usipige. Ondoka zako nenda bar au kwenye starehe nyingine. Kushachafuka watu wanatembea na magonjwa ni sababu tu ya kumalizia ndo inahitajika. Unakuwa muuaji wakati ulipiga tu kofi.
Haukuwa na watoto nae? Unasema haukurudi so ulisamehe kila ulichokichuma ndani ya hiyo nyumba na kumwachia huyo mwanamke?Nilimuacha, na niliapa sintooa mwanamke wa kinyiramba.
Alafu Ile case sijui inaendeleaje, nahisi yule mwanamke aliachishwa kaziMkuu kuna jamaa huku chuga alijichanganya akaoa afande wa kike, siku alipotumiwa majambazi yamshughurikie ndio alijua hakika hakupaswa kuoa polisi mwenye cheo π
Eti kwa wafanyakazi wenzako alafu hujui "kumalizana kishkaji"π€£πHuko kumalizana kishikaji,,ndio kumalizana gani??embu fafanua inaweza kuwa ni mbinu Bora ya kutumia endapo na Mimi huyu wangu naye akibahatika siku kunipeleka Kwa wafanyakazi wenzangu
Subiri kwanza, we ni nani? Yupi? JF bwana! πππSasa hasira za nini dada yangu mweupe mweupe π€©
πππ chukua ushaur huo wa bure mkuu jela tulijengewa wabishiπ π π π Nimecheka mpaka machozi yametoka .....vayolensi
His wife did unwise act to his husband,he called Kanjo on him wich caused his husband to sleep in cell.fortunately to him and unfortunately to his wife the marriage ended there.Mhusika ameisema kwa kejeli nami nikamuuliza kwa kejeli kwanini mkeo hakuwa na nauli? Ameisema as if it is funny wakati si kitu kizuri.
Malizia stori mkuu
Duuh
Pole na hongera ππ aiseee
Malizia mkuuπ
Sikurudi nyumbani kwa siku tatu.Endelea π
Kwenye emoj nitakujibu, subiri. π€Subiri kwanza, we ni nani? Yupi? JF bwana! πππ
Ila mkuu umenikera sana jinsi ulivyomtreat huyo mwanamke wako kwenye hilo suala, yawezekana una mazuri yako kwake, lakini hilo specifically umekosea sana, ndio maana Masai dada hapo juu amekuuliza kama bado mpo pamoja. Ilitosha sana huyo dada kutokukuangalia usoni tena.
πππMimi wife aliniweka lupango kwa kudai nimekaa mda mrefu sana grocery. Nashangaa gari inapaki naambiwa natakiwa kituoni, kufika naambiwa wife kanipeleka kwa kosa la kulewa. Nikalala selo kesho yake nikatoka. Grocery yenyewe ni mita 20 tu toka home.
Huu uelewa wangu kdg niingie Chaka. Nilijua unamaanisha ulilala na mkeo polisi kwa maana wote mlishikiliwa kumbe mke ndo alikusababishia kulala polisi. Pole sana!Niliwekwa ndani na mke wangu baada ya mimi kugoma kutoa mchango wa kumdhamini kaka yake aliyekamatwa na pembe za ndovu.
Zilitakiwa milioni 5 kumdhamini kaka wa mke wangu, ndugu zake walijikusanya wakachanga milioni 3. Zile mbili zilizopungua mke wangu alikuja kuniomba nitoe hizo hela ili kukamilisha malipo ya dhamana.
Sikuwa na hiyo hela, nilimwambia wazi kuwa sina hela. Kilichotokea sasa baada ya kumwambia hivyo alinifokea kwa ukali akinituhumu kuwa nina roho mbaya na sipendi kusaidia ndugu zake Ila naweza kuhonga malaya tu huko mitaani.
Sikufurahishwa na hayo aliyoniambia so nilimfata na kumcharaza kwa vibao vitatu vya shavu ili kumshikisha adabu. Alipiga yowe la uchungu na kutoka baru akatokomea sijui wapi huko.
Baada ya kama lisaa limoja hivi nilipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni polisi akinitaka nifike kituoni, nilishangaa Ila niliitikia wito.
Nilipofika kituoni mshangao wangu ukawa mkubwa zaidi baada ya kumkuta mke wangu yupo hapo na alifika hapo kuripoti kuwa nimemshambulia kwa kukusudia. Nilishindwa kujitetea maana ni kweli nilimpa Kichapo.
Afande aliyeshughurikia hayo malalamiko ya mke wangu alisema hawezi kulimaliza hilo suala muda huo maana ilikuwa ni saa mbili usiku, atalishughurikia kesho yake asubuhi. Afande alimtaka mke wangu arudi nyumbani Ila mimi sikuruhusiwa kurudi nyumbani bali nilitakiwa kulala hapo kituoni.
Muda mfupi baada ya mke wangu kuondoka niliamriwa na afande wa zamu kuvua viatu na mkanda wa suruali kisha nikasukumwa kwenye kachumba kasiko na dirisha wala taa nikawa nimelala polisi kwa mara ya kwanza.
Nililala kwa usiku mmoja tu, asubuhi tuliyamaliza mambo ya kipolisi kishikaji nikaachiwa huru asubuhi hiyo.
Nikiwa na hasira kali sikurudi home niliamua tu kuachana na huyo mwanamke wa kinyiramba.
Tuliowahi kulazwa polisi na wake zetu tujuane hapa.
Unajiepusha na mengi boss, usije fumua mtu ubongo kisa kuonyesha wewe ni mwanaume, na ukikaa hapo uvumilivu utakushinda, kuondoka ndo suluhisho sahihi.Hiyo mbinu ilinisaidia mara nyingi sana, wife akianzisha fujo tu nafungua mlango natembea hatua 20 niko grocery, nikirudi ni kulala tu.
Chezea nini wewe πππππππ
AsieeeπSikurudi nyumbani kwa siku tatu.
Tulipokuwa tunakaa sio mbali na kwao, ni mji mmoja. Nikaamua kuwapeleka watoto kwa bibi yao (mama yake) lakini nikamsimulia kilichotokea na kumuomba asimwambie nataka kumfundisha tu asiwe anapenda kukimbilia polisi kwa tatizo dogo kama hilo. Mama akakubali (alikuwa ananipenda sana kama mkwe anaemjali) akawa anampigia simu mwanae kuhakikisha yuko salama (huruma ya mzazi) lakini hasemi chochote kuhusu watoto.
Baada ya siku 3 nikarudi home peke yangu, akauliza watoto nikamwambia siku ile ulivyoamua kuwaacha na njaa ulitegemea wanaangaliwa na nani? Nimeona huwajali nimewapeleka kituo cha watoto yatimaπ . In short aliteseka sana mpaka kujua watoto walipo, maana polisi aliogopa kurudi tena, nyumbani kwao hakutaka kuwaeleza ukweli wa tukio maana ni aibu kwake na kwao nakubarika sana wangembadikikia wote.
NB: ukitaka kumaliza kiherehere cha mwanamke, waweke karibu ndugu zake, hasa mama. Automatically anakosa mtetezi kwao.
Ndo maana hata mimi nikawahi mapema kusoma huu mkasa daah ππππππHuu uelewa wangu kdg niingie Chaka. Nilijua unamaanisha ulilala na mkeo polisi kwa maana wote mlishikiliwa kumbe mke ndo alikusababishia kulala polisi. Pole sana!
hapa itakuwa kuna kidume muda huu kinafurahia sana ulivyomkacha mnyiramba wa watu,hasira hasaraNi miezi tisa imepita sijarudi home hadi leo na sina mpango wa kurudi, nilimwachia kila kitu likiwemo jukumu la kulipa kodi ya nyumba
Lucha kama luchaMimi mke wangu alichukua 3M ya biashara akamkopesha shoga yake anaedaiwa kwenye mikopo nyonya damu wakati shoga yake hana kazi yoyote itakayo msaidia kulipa hilo deni.
Ikabidi niende polisi mwenyewe nikawaambia polisi waniweke ndani maana nikibaki nje ntamuua wife.
lazima atakuwa afande alijiongeza tuπ π πukute afande alivyokuweka nguvuni akaenda kulala kwako halafu asubuh ukampongeza na lififte