Ulishawahi kumchukia member wa JF pasipo kumjua

Ulishawahi kumchukia member wa JF pasipo kumjua

Ukimchukia unajipa jakamoyo lisilo na maana yoyote! Huwezi kumpangia mtu anachokiwaza hivyo tupendane kwa ajili ya Allah
ni kweli kabisa chuki hazifai sio humu tu hata huko mitaani kwa maana ni chanzo cha magonjwa mengi sana.

Tukija kwenye hii post, nimeona imetamalaki unafiki wa kufa mtu, na humu JF kiukweli watu tunachukiana sana tu.. Nimetolea mfano hai wa cocochanel, huyu dada kwa miezi michache ya hivi karibu nimeona akitengeneza chuki na members wengi humu tu humu kupitia comments zake za ovyo na zenye ukakasi. sasa nashangaa kwenye Uzi huu wale ambao nimewahi kuwaona mara kadhaa wakimtusi na kumtolea maneno ya chuki huyu dada wakisema hawajahi kuwa na mikwaruzano wala chuki na mtu humu JF. It's so funny to read the comments.
 
Kuna mmoja humu nirilushiana nae matus naye akarusha aiseee tulijaza uzi mitusi halafu baada ya hapo nikajishangaa MTU mwenyewe simjui ni useless kabisa
 
Mimi nitakuwa mnafiki kusema hakuna watu nawachukia humu:

Kuna watu humu ni wagomvi au wanapenda kutukana tukana hovyo, ili nisimjibu au kuendelea kukereka na issue za mtu huyo huwa naenda kwenye kitufe cha ignore nakibonyeza mchezo umekwisha.

Mfano, zamani GENTAMYCINE alikuwa ni mkorofi sana na anatukana ovyo, nikamwignore, siku hizi jamaa kabadilika sana na hata akitukanwa anajibu vizuri tu, so hayuko tena kwenye ignore list yangu.

Hii ni list yangu ya watu ambao wako kwenye ignore list kwa sababu zangu mwenyewe:

View attachment 512005

Usiponizoea na kunijulia unaweza kudhani Mimi ni Mtu mmoja mbaya sana na wa ajabu ila ukinijulia tu unaweza ukatamani hata siku isipite hujafanya interaction na Mimi au hujanifuatilia humu JF. Napenda sana Utani na kuchangamsha Watu na bahati mbaya sana nina ' ukomedi ' mkubwa mno ndani yangu.

Pole kwa kunifikiria vibaya hapo mwanzoni ila pongezi pia kwa kutambua umuhimu wa GENTAMYCINE Mkuu.
 
Mambozzz
.
Ivi ulishawahi kumchukia members yeyote wa jf. Kutokana na mijadala,mabishano yanayoendelea humu.mimi binafsi sijawahi mchukia members yoyote humu jf. Hata anikashifu vipi.
Ila.
Humu ndani kuna mijitu inajifanya much know sana kabla hata hujamaliza kuandika uzi walishaaanz kuponda, mingine mi bazazi....
 
Mmh! Cdhani na sina taarifa kitoka kwenye ubongo wangu km kina mtu namchukia au nna wivu nae hata kama c mchangiaj sna wa post either za politics, economic,religious au yoyote ile. Ila huwa inaniudhi na inanipain pale mtu anapoamua kwa maksud kuichosha point ya msingi ya mtu eti kwa mahaba tu ya upanfe unaozungumzwa bila kuangalia mustakabali wa Tz yetu, hilo tu.
 
Usiowajua sio sawa kuwachukia, ila wale unaowajua kama kina le mutuz hapo ni uamuz wako. Maana vingi anavyoongea haviendani na umri wake wa kustaafu
 
Maisha yangu huwa siwezi kumchukia mtu nisie mjua na hata ninaemjua tukikwanzana basi huwa natafuta faragha tuyamalize maana hujui huyo atakuwa msaada wako siku moja. Na Mungu huwaumbua wanafiki au walichukiana kwa kuwakutanisha kwenye shida ili maafikiano yapatikane.

Mleta Uzi umefikiria mbali sana. Na Mungu akubaliki sana. Ombi kwa kuwa tuna mitizamo tofauti na tumekutana humu tukiwa na tabia yofauti na malezi tofauti basi si busara tofauti hizo zikaonekana humu na Jamii forum lengo ni kukaa pamoja na tubadilishane mawazo positively.
 
Back
Top Bottom