Ulishawahi kumpa Baba yako zawadi?

Kuna mzee mmoja mwenye busara aliwahi sema kama wewe " wazazi wenu wanapendana sana na wanaoneana wivu wavumilieni" itakua labda .... ila nimependa sana spirit ya mshua wako kwa mkewe na ndiyo staili ninayoenda nayo na mke wangu. Nashukuru sana Mungu mke wangu hana mizengwe kabisa, angekua nayo ase ningeshindwa kuvumilia, kuvumilia yataka moyo
 
Hongera....all the best
 
Nikipata chance huwa na mrushia Mzee pesa kidogo yeye na Bi mkubwa
Jambo lilonifanya nisipende kumtumia ni MTU wa tungi sna analewa kupitiliza

Nafikiria labda nimnunulie zawadi badala ya pesa kama suti ivi
Acha kumtumia hela direct. Tuma hela mara mbili, hela ya matumizi ya ndani mpe mama yeye hawezi kuwafelisha. Mama utamuongezea kidogo hela yake ya kutumia kisha mzee utampa hela kidogo tu ya kula tungi ila muda huo matumizi nyumbani yapo.
 
Mzee wangu hanitaki hata simu zangu anakaa mwaka hajazipokea. Kwanza sijui kwake ni wapi wala hajui nasoma nini wala naishije. Huwa nambahatisha nikienda likizo kwa bibi naye akaja, au kwa simu huwa nambahatisha nikimpigia bibi nae akawepo. Hata nikienda kwa ndugu zake huwa hawamwambii hawa nina ukaribu nao kumzidi, mtu kama huyu zawadi atazisikia redioni.

Babu yangu alinifaidi hata kufia mikononi mwangu, nilifunga shule nikasikia anaumwa nikafunga safari kumuuguza. Nimefanana nae character ndio maana tuliivana sana
 
Hakutaki? Ww mtoto wa nje ya ndoa au? Khaa..wazee wengine bwana!
 
Zawadi mzee ananunuliwa kutokana na mahitaji na kitu anachokipenda au angetamani kuwa nacho
Pamoja na kuwa zawadi za baba mara nyingi huwa ni za familia ila ni kweli kuwa baba alitakiwa ahakikishe vinapatikana
Mf:
  1. Kumkatia Bima ya Afya (Kama hana ni zawadi muhimu kuliko suti)
  2. Kumkarabatia/ Kumjengea nyumba kama iliyopo imechoka au haikidhi hali ya sasa
  3. kumwekea maji & Umeme nyumbani kwake nk
  4. Kumnunulia Simu, radio, TV nk
  5. Usafiri wowote kulingana na uwezo (Kama anahitaji)
  6. Kumwekea fixed amount ya kumpatia kila mwezi kwa kadri Mungu alivyo kubariki.
Mwisho;
Kuangalia Changamoto anazopata kutoka kwa familia na kumsaidia kuzibeba

Wababa wengi wanashukrani sana ukimsaidia kubeba majukumu yanayo muumiza kichwa hata kama sio ya kwake binafsi
 
Hakutaki? Ww mtoto wa nje ya ndoa au? Khaa..wazee wengine bwana!
Alihama kikazi akaoa uko kwa siri. Mke wake alipojua kuwa kaacha familia somewhere akaanzisha safari za waganga nyingi na akarasimishwa rasmi. Story nilipata kwa bibi mzaa baba. Sema kwetu huwa hawapangii mtu maisha hata wajue unakosea vipi. Utashauriwa vizuri kisha uachiwe nafasi kuamua
 
Duh...pole
 
Sikulelewa na baba,alifariki nikiwa mdogo,nikalelewa na mama na kaka yangu ambaye ni marehemu sasa,kaka yangu alinilea kama mwanae nilimpenda sana,angekuwa hai leo ningemfanyia mambo makubwa mwenyewe angeshangaa,kuna kipindi nikiona vitu vizuri vya kiume namkumbuka natamani angekuwepo nimfanyie sapraise.endelea kupumzika kwa amani kaka[emoji22][emoji22][emoji26][emoji26][emoji26][emoji26]
 
Pole sana shibela
 
Sema mkuu wazazi wengine wanazidi ukatili ........coz wana assume ukatili ni prestige
 

Wanatibuana kisa nini[emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…