Ulishawahi kupewa zawadi hewa mbele za watu?

Ulishawahi kupewa zawadi hewa mbele za watu?

amadala

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2017
Posts
4,265
Reaction score
12,268
Hello Wadau wa JF!

Weekend ipo vipi pande hizo?

Binafsi ipo poa nimeshapata breakfast ya chapati za kusukuma, rosti la maini na kachai ka maziwa pembeni.

Kwa wale wapenzi wa Korean Drama Leo nimerudi 2016 naangalia Shopaholic Luis.

Kwenye 1 2 3 nimekumbuka siku ya sherehe yangu kaka yangu nitampa jina la Steve , wakati wa kutoa zawadi ulipofika na yeye alikuwa miongoni waliotoka mbele kufanya hivyo, basi bwana zamu yake ikafika akachukua MIC pale Kwa mikogo tena alikuwa amejipigilia suti na shades juu🙌 akatangaza kuwa amenipa zawadi ya kunilipia trip ya kwenda Dubai😂 niliposikia tu hii kitu nikajua hii ni zawadi hewa kabisa Kwa sababu najua fika Kaka Steve yeye mwenyewe Kwa kipindi kile Dubai anaiona Kwa picha za google😂

Je, wewe ulishawahi kupewa zawadi hewa mbele za watu?
3c7d66bcc879a835d5a938e6d8a57cb4.jpg
 
Kuna muda tunafosiwa kufanya hivyo. Mtu umetulia zako kwenye sherehe na mchango ushatoa, unashtukizwa fulani bin fulani hebu simama tuambie utawapa wahusika wa sherehe kitu gani. Hata mimi ntaahidi uongo kwakuwa sikujiandaa.
 
Binafsi ipo poa nimeshapata breakfast ya chapati za kusukuma, rosti la maini na kachai ka maziwa pembeni.

Mi uzi wote hapa tuu ndo pamenikosha maana chapati za kusukuma na rost haijalishi rost la nini ila huwa zina nichanganya sana.
😋😋😋😋😋😋😋🙌😋😋😋
Nimejikuta natokwa na mate
 
Ha ha ha kesho ukate hiyo kiu😂
 
Back
Top Bottom