Ulishawahi kuulizwa swali gani na mwanao ukakosa jibu?

Ulishawahi kuulizwa swali gani na mwanao ukakosa jibu?

Aliwahi kuniuliza mbona siku ya harusi yenu mimi sikuwepo? Nikamjibu tulikuwa bado hatujakununua? Akasema namdanganya mbona watoto wanazaliwa ikabidi niwe pole ha ha ha
 
Wakati huo sina usafiri hali ngumu balaa,mtoto wangu aliwahi kuniuliza hivi Baba kwanini na wewe hununui gari,nikamjibu mimi sina hela,akasema mbona kila siku naona unampa mama hela,nilichoka,maana yeye alikuwa anaona zile elf 5 nazoacha pale za mboga alikuwa anaziona nyingi balaa...
Hivi gari linauzwa shilingi ngapi ambayo wewe huna? Hapo nimemfuata shule tunarudi nyumbani kwa mguu na rafiki zake wanatupita njiani wakiwa kwenye magari ya kwao
 
naamini kuna ukweli ila unaongeza chumvi
Nadhani wewe ndiye unaongeza chumvi kwenye majibu yako. Mtoto wa miaka 5 ni mkubwa saana.

Ni aidha hauna mtoto au anaishi na mama yake huna ukaribu naye.
 
Kipindi cha ujauzito niliwahi kuulizwa, mbona tumbo lako limevimba....nikamjibu kuwa kuna mtoto...akaendelea kuniuliza Kaingiaje??? Sikumjibu
 
Back
Top Bottom