Ulishawahi kuulizwa swali gani na mwanao ukakosa jibu?

Ulishawahi kuulizwa swali gani na mwanao ukakosa jibu?

Binti yangu wa miaka 7 ameniuliza juzi mama unasema mimi kabila langu mchaga na baba yangu pia ni mchaga nikamwambia ndio, akasema wewe umesema kabila lako ni mbena kwanini wakati wewe ndio umenizaa ikabidi nianze kumuelekeza kwamba mtoto akizaliwa jina la ukoo, kabila na dini anafwata kwa baba yake na sio mama kwa sababu amezaliwa na sisi wote wawili.

Nadhani bado hajaridhika na jibu maana haelewi kwanini afwate kila kitu kwa baba na asifwate kwa mama wakati wote wazazi wake.

Kinachomchanganya zaidi baba yake wazazi wake wote wachaga na mimi wazazi wangu wote wabena haelewi combo yake imekuwaje 😀😀😀😀
A Smart Question
 
A Smart Question
Anachoshangaa zaidi kama mtoto akizaliwa anafwata kabila kwa baba mbona bibi yake mzaa mama ni mbena kama mama yake halafu bibi mzaa baba ni mchaga kama baba yake kwanini nao wasingekuwa na makabila tofauti mbona wazazi wake tunafanana makabila na mama zetu kwanini yeye tuu ndio awe wa tofauti.

Kila nikijaribu kumuelewesha naona nazidi kumchanganya tuu😂😂😂😂
 
Hivi gari linauzwa shilingi ngapi ambayo wewe huna? Hapo nimemfuata shule tunarudi nyumbani kwa mguu na rafiki zake wanatupita njiani wakiwa kwenye magari ya kwao
Hili swali nadhani karibia kila mzazi amewahi kuulizwa. Mvua ilikuwa inanyesha nikaenda kumfwata na mwamvuli tukapishana na ndugu yetu amewabeba wanae kwenye gari akaniuliza " mama kwann usinunue na wewe gari uwe unanifwata tusilowe na mvua???" Nikamwambia tuu unavyosali niombee mama yako siku nitanunua tuu
 
Watoto wenye umri kati ya 4 hadi 7 ni exquisitive/curious saana. Huu ndiyo umri wao wa kuanza kuchukuza ulimwengu unaowazunguka na ubongo unakua kwa kasi saana.

Kama wewe ni mzazi/mlezi/kaka au dada bila shaka ushawahi kuulizwa swali na mtoto mdogo. Je ni swali gani? Ulijibuje?

Wataalam wanakuambia mtoto anapouliza swali usili-dismiss swali unatakiwa kumjibu. Tunapoyapotezea maswali yao kwa kudhani tunaogopa kuwafunza yawakubwa hapa ndipo tunapowateza.
Mbona mama akiwa anabadilisha nguo unatufukuza alafu wewe hutoki!!??

Na Mimi nikikuwa baba alafu wewe mtoto ntakukomesha

😂😂💧
 
mtoto wa miaka 5 aende kuuliza YouTube?
Kingine kitakachokufanya uendelee kusema ni chai isiyo na sukari ni maswali yote aliuliza kwa kiingereza bado anajifunza kiswahili.

Nimemfundisha chochote asichoelewa anauliza Gemini au Youtube majibu yote yapo hapo.
 
hivi unamjua mtoto wa miaka 5 lakini?

umebaki kutuwashia moto tu tuuzunguke
 
hivi unamjua mtoto wa miaka 5 lakini?

umebaki kutuwashia moto tu tuuzunguke
Mkuu unaishi wapi kwani ? Mwanangu wa miaka 5 anajua kusoma, anatumia simu anatupigia wazazi wake simu tunapokuwa mbali, anakaa na kaka yake mdogo na kumlisha, anacheza game zingine mimi nahitaji siku kadhaa kuzimaster.....

Na nimeona watoto wanaofanya vingi zaidi ya huyu.

Mtoto wa jirani yangu ana miaka 10 anatangeneza logos....anawauzia watu na anapiga pesa.
 
Sasa mbona 80% wote humu mnaulizwa maswali yenye uelekeo wa mambo ya kukulana 🤣🤣
 
Mkuu unaishi wapi kwani ? Mwanangu wa miaka 5 anajua kusoma, anatumia simu anatupigia wazazi wake simu tunapokuwa mbali, anakaa na kaka yake mdogo na kumlisha, anacheza game zingine mimi nahitaji siku kadhaa kuzimaster.....

Na nimeona watoto wanaofanya vingi zaidi ya huyu.

Mtoto wa jirani yangu ana miaka 10 anatangeneza logos....anawauzia watu na anapiga pesa.
😂😂😂😅😅 hizi kamba zinatosha mkuu

anawauzia watu na anapiga pesa au sio.
 
Back
Top Bottom