Ulishawahi kuwa kwenye mahusisno na msichana anayechagua vyakula? Mimi nilimlaza njaa siku mbili akaanza kula ugali dagaa

Ulishawahi kuwa kwenye mahusisno na msichana anayechagua vyakula? Mimi nilimlaza njaa siku mbili akaanza kula ugali dagaa

Hata kuishi nae muda mrefu ingewezekana
Aaah ingekuwa si busara maana alikuwa ni demu wa mshikaji,we ungemnunulia sato mkubwa ale siku mbili sato akiisha aende zake ungekupa raha zote za dunia
 
Huyu binti alikuwa ni mpenzi wa rafiki yangu,sijui walizinguana nini,saa nne usiku akanipigia simu kuwa amezinguana na rafiki yangu yaani mpenzi wake na hajui atalala wapi hana hata mia mbovu

Nikamwambia njoo ulale kwangu,usiku mrefu ndugu zanguni,nilikuwa naishi kighetogheto chumba kimoja ,itoshe kusema tukalala mzungu wa pili kufumba na kufumbua tuko tunaivunja amri ya sita kimasihara.,shetani mtu mbaya sana

Kesho yake ilikuwa weekend ,sie watu wa pwani tunajua kukirimu wageni,mjinga mimi nikanunua kilo ya nyama akasema hali nyama,ndani kulikuwa na kabeji akasema huwa hali kabeji,nikazunguka genge la jiranikuchukua dagaa akasema dagaa akila anasikia kichefuchefu,nikazunguka nyuma kuchuma matembele nayo hatumii,nyanya chungu na bamia pia hatumii,maarage akasema anasikia kiungulia,anataka samaki tu,
Ugali wa dona akasema hatumii pia.

nilimpuuza siku mbili mpaka alipoanza kula ugalii dagaa nikampa nauli arudi kwao

Nilishangaa jamaa aliwezake kuishi na huyu kiumbe kwa muda wote huo

Mimi bunafsi ni mtu ninayekula kila kitu kasoro sumu,nilikuwa njombe nikaletewa ugali na mboga inaitwa mkalifya ni chungu mithili ya shubiri ila ugali uliisha
Utatoboa kufikisha miaka 60
 
Nikamwambia njoo ulale kwangu,usiku mrefu ndugu zanguni,nilikuwa naishi kighetogheto chumba kimoja ,itoshe kusema tukalala mzungu wa pili kufumba na kufumbua tuko tunaivunja amri ya sita kimasihara.,shetani mtu mbaya sana
Samahan, kwani wewe ni Mngoni😁?
 
Nilishindwa kabisa kula hiyo mboga mdau.

Ila mimi ni mpenzi wa jamii zote za samaki kasoro dagaa!
Dagaa wa kigoma ni wazuri Sana Kama NYAMA.

Pia ukerewe Kuna dagaa wakubwa wakubwa Kama SAMAKI wanaitwa FURU.

Pia Kuna SAMAKI KAMONGO unamfaham?
 
Dagaa wa kigoma ni wazuri Sana Kama NYAMA.

Pia ukerewe Kuna dagaa wakubwa wakubwa Kama SAMAKI wanaitwa FURU.

Pia Kuna SAMAKI KAMONGO unamfaham?
Samaki ninaowafahamu ni
Tasi, changu, sato, sangara, kolekole, pweza, ngisi n.k pengine kamongo namjua kwa kumwangalia.

Dagaa wa Kigoma wakoje? anyway siwajui maybe kwa sababu siko interested.
 
Samaki ninaowafahamu ni
Tasi, changu, sato, sangara, kolekole, pweza, ngisi n.k pengine kamongo namjua kwa kumwangalia.

Dagaa wa Kigoma wakoje? anyway siwajui maybe kwa sababu siko interested.
Screenshot_20241105-151105.png

Screenshot_20241105-150845.png

Huyu ndio KAMONGO...Wajita huwa Wana msemo wao "KAMONGO IKO SHINDA NYAMA ILA KWA MAHARAGE IKO TOKA DROO" 😅
 
Si Bora aliyegundua majani ya kunde....aliyegundua mchunga alikuwa anatafuta nini mara nyanya chungu.....Kabichi sijui alikuwa anataka kugundua nini mara sukuma wiki ...kwanza alianzaje kuona hii mboga ni ya kusukumia wiki ... daaah
Je yule aliyeanza kutumia majani ya mkaratusi na ya mpapai alifikiria kitu gani.
 
Back
Top Bottom