Ulisikia muziki huu kwa mara ya kwanza Ukiwa wapi?

Ulisikia muziki huu kwa mara ya kwanza Ukiwa wapi?

Old school Ndio nyimbo zangu pendwa sana! huwa nikisikiliza naimba mwenyew na huwa zinaniondoa stress
 
Franklin Boukaka alinyongwa mwaka 1972; alitoa wimbo huo mwaka 1970 ukampa umaarufu sana na kusababisha apendwe sana na wanamapinduzi wa wakati huo waliochukia wakoloni weupe kuondoka na kupata wakaloni weusi; jambo hilo lililomfanya achukiwe na viongozi wa Congo wakati huo na kusababisha anyongwe.
Aaiiyeeeee Africa.......


Aaiiyeeeee Africa eeeh

Ooh liberte.....

Boukaka

Sijui aliimba lugha gani lkn hiki kibao lzm nikisikilize kabla sijalala..... Nakipenda sana nasikia alinyongwa daah

R.I.P Franklin Boukaka
 
Kuna Mnigeria huyu kwa jina la Onyeka Onwenu ambaye amefariki mwaka jana. Alivuma kwa muda mrefu sana ila kwenye miaka ya themanini alitoa wimbo wa "Ekwe" uliotawala la anga la Afrika. Wewe uliusikia wimbo huo kwa mara ya kwanza ukiwa wapi?


View: https://www.youtube.com/watch?v=9_Vu19wiDC0
 
Guantanamera ni wimbo wa kutokea Cuba na ni wa zamani sana karibu karne moja iliyopita. Umeimbwa na watu wengi sana ila wimbo huu ulipata umaarufu baada ya kuimbwa na Julio Iglesias mwaka 1981. Wewe version hii ya Julio uliisikia kwa mara ya kwanza ukiwa wapi?


View: https://www.youtube.com/watch?v=Wg5-m0tNeoY
 
Honestly speaking. Me ni kijana wa 90 mwishoni na ni music enthusiasts. Hizi nyimbo nimezisikiliza sana na nazipenda pia.

Drc hapo
1.King Kester _Nzinzi
2.Mayaula mayoni_Mbongo
 
Honestly speaking. Me ni kijana wa 90 mwishoni na ni music enthusiasts. Hizi nyimbo nimezisikiliza sana na nazipenda pia.

Drc hapo
1.King Kester _Nzinzi
2.Mayaula mayoni_Mbongo
Ni kweli, Nzinzi wa Kester Emeneya ulitoka nadhani mwaka 1986 au 1987 hivi, na ulitawala sana anga wakati huo.


View: https://www.youtube.com/watch?v=sVPx2sLCO48

Mayaula Mayoni alikuwa na vipaji sana. Alisoma chuo kikuu cha Dar es salaam akapata digrii ya Methametics; wakati akiwa mwanafunzi wa Dar alikuwa mcheza mpira akiichezea timu Yanga (jangwani). Baada ya kupata digrii na kurudi kwao Zaire, hakupenda kuwa mwalimu ndipo akajiunga na bendi ya TP OK Jazz kama muimbaji.

Wimbo huo wa Mbongo ulivuma sana mwanazi mwa miaka ya tisini. Pale Mwenge kulikuwa na baa inaitwa Mbogwe, ilimwalika mwaka 1995 apiga wimbo huo wa Mbongwe mfululizo na watu wakacheza mpaka saa kumi alfajiri.


View: https://www.youtube.com/watch?v=Zf6kBV1NNvs
 
Back
Top Bottom