Ulisikia muziki huu kwa mara ya kwanza Ukiwa wapi?

Ulisikia muziki huu kwa mara ya kwanza Ukiwa wapi?

Kaoma (Loalwa Braz)- Lambada

Huyo mwimbaji Loalwa Braz mwenyewe alifariki 2017; hao watoto wawili walioweka chachu kwenye wimbo huo walichukua maisha ya tofauti kabisa baada ya hapo. Yule mvulana Chico alimua kuwa mchungaji kwenye kanisa la kiprotestant, na yule msichana Roberta akawa mcheza sinema.


View: https://www.youtube.com/watch?v=-hosJTEjYQ4

Wimbo mwingine uliowapa umaarufu sana hawa jamaa ni huu wa Decando Lambada. Ulivuma sana kuanzia mwaka 1993 hadi 1997. Wewe uliusikia kwa mara ya kwanza ukiwa wapi?

Pamoja na kujaribiana na wanawake wa kutoka sehemu mbalimbali za dunia wakati wa ujana wangu; sikufanikiwa kubanana na wabrazili ila wanawake hawa wa Brazili wanaonekana wanajua sana kutokana na miondoko yao.

View: https://www.youtube.com/watch?v=vXr-X-cqpAk
 
Hakutokea Burkinafaso.
Nafikiri jina lake la Badarou liliwachanganya wajanja wa Dar wakita Wagadugu, na ndipo huu mziki kitaa ukawa unaitwa wagadugu.
Mwanamziki ni Mfaransa mwenye asili ya Benin.
Nadhani uko sahihi sana ila Muziki huo uliuzwa Afrika kuwa ni kutokea Wagadugu, na hata cover ya Album yake ilionyesha hivyo. Ilikuwa imeandikwa nadhani kitu kama "Ougadougu Hits". Kwa hiyo wote tukaamini kuwa ni wa Wagadugu
 
Celine Dion sasa ni mgonjwa, mapenzi na maisha ya Celine Dion ni changamoto kwakweli
Miaka ya tisini Selina alikuwa moto sana, lakini Mungu ndiye anayejua hatima yeu kwani iko mikononi mwake siku zote. Selina wa leo siyo yule wa mwaka 1997.
 
ni vile tu vitoto vya saiv tumekosa adabu,, yaani kuna watu mmezaliwa miaka ya wazazi wetu humu

Shkamooni wakubwa
 
Isuna disco tech Singida huko, Mbeya jkt itende, Shilam disco Dodoma iringa road.
 
Alafu kulikua na dansa anaitwa Black Moses sijui alipotelea wapi.yule jamaa alipewa kipaji aisee sidhani km kuna dansa atamfikia yule
 
Alafu kulikua na dansa anaitwa Black Moses sijui alipotelea wapi.yule jamaa alipewa kipaji aisee sidhani km kuna dansa atamfikia yule
Kuna dansa mwingine alikuwa anaitwa Double D, yaani Diga Diga, na mwingine akiitwa Super Ngedere
 
Kuna dansa mwingine alikuwa anaitwa Double D, yaani Diga Diga, na mwingine akiitwa Super Ngedere
Black Moses,Diga diga ,Wametoka Morogoro hao, Super Ngedere, Nyamwela,, Latifa,lango la jiji(Flora), kuna mwingine alikua muigizaji na anadance sana tu kwa macheni pale makutano sikumbuki jina lake walikuja baadae na kina Jobiso na mama zao walikuja baadae.
Nafikiri wote wamekufa.
 
Donna Summer alivuma sana miaka ya sabini na mwanzoni mwa miaka ya themanini. Siyo wengi wanajua muziki wake leo. Mmoja wa vijana walioshiriki kwenye video hii ndio waliokuja kuanzisha Boyz-II-Men

Nilisisikiliza mziki wake mara ya kwanza kwenye LP nikiwa Seconday school kabla ya Vita ya Kagera.


View: https://www.youtube.com/watch?v=vGTs4EXKUWc

Daa mkuu naona tuko umri sawa
Marehemu Donna Summer mpaka last week nilikuwa namsikiliza nikiwa naelekea Manchester
Wimbo wake wa The Woman in me
Asante sana kwa uzi huu wa nyimbo za zamani
Yaani karibu zote ndio favorite songs zangu
 
Back
Top Bottom