Abie
JF-Expert Member
- Jul 15, 2021
- 289
- 535
Wakuu salaam,
Watu wengi tumekuwa tukihangaika kupata matibabu ya magonjwa mbalimbali yanayotusumbua kwa muda mrefu bila mafanikio yoyote. Tunatembelea hospitali mbalimbali, kupata vipimo na kupewa dawa (medications) tofautitofauti lakini mwisho wa siku hatupati nafuu.
Lakini kwa upande mwingine inawezekana kuna ambao wamehangaika lakini mwisho wa siku wakapata dawa na wamepona. Hivyo basi uzi huu ni special kwa kutoa ushuhuda wa namna ulivyopona tatizo lililokusumbua kwa muda mrefu.
Inawezekana ulisumbuliwa na ama kifua, fangasi, maumivu ya kichwa, kiuno, vidonda vya tumbo kwa miezi au miaka kadhaa halafu ukapata dawa na imekusaidia. Kwahiyo karibu utoe ushuhuda wako wa namna ulivyopona ili watu wengine iwasaidie.
Karibu sana.