Meno yalikua yananisumbua na kila likianza kuuma natumia kila aina ya dawa na ushauri kutoka kwa wadau wa kila aina ila maumivu yalikua yanaongezeka tu hadi hatimaye naishia kuling'oa, ikaja kutokea jino lingine likaanza maumivu makali nikawa najaribu kila aina ya dawa ila wapi, siku moja nasafiri kwenye bus huko Tanzania, jino likiwa kama linaniua vile, akaibuka jamaa mmoja alikua anauza madawa kwenye bus.
Akatangaza kwenye baadhi ya dawa yake, anayo pia ya maumivu ya jino, nikanunua dawa fulani hivi ya unga unga mweupe, nikatia kwenye jino baada ya muda mfupi likaacha kuuma, na la kushangaza likapata nafu halijawahi kunisumbua tena, tatizo sikuchukua namba za jamaa maana kwa uvumbuzi wake anaweza akapiga hela sana.