Ulitumia kiasi gani cha fedha ama umepanga kutumia kiasi gani cha fedha kugharamia harusi yako?

Ufanya vitu kufurahisha watu au sio ?

Una miaka mingapi bwana mdogo ?
 
Hongera sana Mkuu, ulikuwa na event planner nini?

Hiyo ratiba ilikuwa fupi isiyochosha.

Kama ulivyosema, vyema kufanya sherehe ambayo itawafanya wanandoa kufurahia sio kuondoka na Madeni baada ya tukio

Hapakua na event planner ndugu yangu. Kamati ndogo sana ya kuratibu chakula tu.
 

Uko sahihi Mnyampaa, na pia kuondoa ile kasumba ya kuvifanya jambo la kuoa kuwa gumu na mzigo.
 
Uko sahihi Mnyampaa, na pia kuondoa ile kasumba ya kuvifanya jambo la kuoa kuwa gumu na mzigo.
Ulimbukeni na kufuata mkumbo ndio jambo linatusumbua kwa sasa hasa tunaoishi mjini.

Kila mtu atataka afanye jambo kubwa kuliko uwezo wake, lengo kubwa ili aonekane naye kafanye na afurahishe wengine.

Binafsi sio muumini wa michango, kwenye ngazi ya familia(ukoo) hapo sawa na huwa nasema ni vizuri jambo lianzie ngazi ya familia. Kama familia ina uwezo wamalize jambo. Watu wengine mbali na hapo nitachanga kulingana na mahusiano(ukaribu) niliyonayo.

Kuna jamaa alikuwa na uwezo wa kufanya shughuli ambapo hadi alirusha harusi yake TBC kwenye kipindi cha Chereko Chereko lakini kwenye maandalizi aliomba michango[emoji2][emoji2]
 
Mkuu hiyo michango ukiiendekeza unaweza kutoboka mifuko.

Kama unaletewa michango ya 700k si balaa hilo πŸ™Œ
Ni shida sana, kadi mbili za laki mbili na hamsini Kila moja, moja ya laki na nusu. Pesa inauma mbaya kwenda kwenye ndoa ya mtu daaah!
 
Ila Kuna watu Wana Hela aisee. Nineshashuhudia ndoa za 40M+ na nimesimamia Moja kama mhasibu ya 30M+ aisee. Inategemea na unaona nani, familia yao ipoje, na wewe binafsi unataka nini.
 
Sitofanya sherehe ya harusi...
Gauni langu nataka liwe zuri sanaaa... nipige picha za ukumbusho nikitoka kanisani

Baada ya kanisani kila mtu akale kwao!
Ahsante sanaπŸ™πŸ»
 
Nalipa mahari na posa
Vingine atafanya yeye akitaka

Siwezi kuchangisha watu kwenye mambo kama hayo
 
Nilitumia milion 20 tuuuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…