Ulitumia kiasi gani cha fedha ama umepanga kutumia kiasi gani cha fedha kugharamia harusi yako?

Ulitumia kiasi gani cha fedha ama umepanga kutumia kiasi gani cha fedha kugharamia harusi yako?

Mkuu nilifanya vile kumfurahisha Bibi yenu pamoja na baadhi ya ndugu, kama nilivyosema awali, Wanawake hawapendi kuolewa kimya kimya.

Ndiyo maana niliamua kujiandaa miaka 5 ili kufanikisha tukio

Lakini wapo watu, wanatumia zaidi hata ya 100M kugharamia harusi.
Ufanya vitu kufurahisha watu au sio ?

Una miaka mingapi bwana mdogo ?
 
Hongera sana Mkuu, ulikuwa na event planner nini?

Hiyo ratiba ilikuwa fupi isiyochosha.

Kama ulivyosema, vyema kufanya sherehe ambayo itawafanya wanandoa kufurahia sio kuondoka na Madeni baada ya tukio

Hapakua na event planner ndugu yangu. Kamati ndogo sana ya kuratibu chakula tu.
 
Kufanya shughuli kwa gharama zako hata ziwe kubwa haina shida.

Shida inakuja unapochangisha watu ili ufanye jambo la gharama kubwa(kifahari), wengi unakuta hawana vipato vikubwa ila wanataka mambo makubwa na kuanza kutegemea kuchangiwa.

Hatukatai kuchangia ila tuchangie kwenye mambo ya msingi. Hivi hapa mjini kuna gharama za Saloon zinazofika hadi 500,000?

Uko sahihi Mnyampaa, na pia kuondoa ile kasumba ya kuvifanya jambo la kuoa kuwa gumu na mzigo.
 
Uko sahihi Mnyampaa, na pia kuondoa ile kasumba ya kuvifanya jambo la kuoa kuwa gumu na mzigo.
Ulimbukeni na kufuata mkumbo ndio jambo linatusumbua kwa sasa hasa tunaoishi mjini.

Kila mtu atataka afanye jambo kubwa kuliko uwezo wake, lengo kubwa ili aonekane naye kafanye na afurahishe wengine.

Binafsi sio muumini wa michango, kwenye ngazi ya familia(ukoo) hapo sawa na huwa nasema ni vizuri jambo lianzie ngazi ya familia. Kama familia ina uwezo wamalize jambo. Watu wengine mbali na hapo nitachanga kulingana na mahusiano(ukaribu) niliyonayo.

Kuna jamaa alikuwa na uwezo wa kufanya shughuli ambapo hadi alirusha harusi yake TBC kwenye kipindi cha Chereko Chereko lakini kwenye maandalizi aliomba michango[emoji2][emoji2]
 
Mkuu hiyo michango ukiiendekeza unaweza kutoboka mifuko.

Kama unaletewa michango ya 700k si balaa hilo 🙌
Ni shida sana, kadi mbili za laki mbili na hamsini Kila moja, moja ya laki na nusu. Pesa inauma mbaya kwenda kwenye ndoa ya mtu daaah!
 
Ila Kuna watu Wana Hela aisee. Nineshashuhudia ndoa za 40M+ na nimesimamia Moja kama mhasibu ya 30M+ aisee. Inategemea na unaona nani, familia yao ipoje, na wewe binafsi unataka nini.
 
Nalipa mahari na posa
Vingine atafanya yeye akitaka

Siwezi kuchangisha watu kwenye mambo kama hayo
 
Suala la Kuoa ama kuolewa bado litaendelea kuwa ni hitaji muhimu miongoni mwa Jamii ya watu wengi Ulimwenguni.

Kwa Tanzania, tunazo Ndoa za aina mbalimbali ambazo zinatambulika kisheria ambazo ni Ndoa za Kidini, Kimila na Kiserikali.

Mara baada ya kufunga Ndoa, maharusi wengi Kwa kushirikiana na jamii zao, hupenda kufanya sherehe. Sherehe hizo huambatana na michango Kwa walio wengi kupitisha Kadi kwaajili ya kuomba kuchangiwa kufanikisha sherehe za harusi zao.

Japo baadhi hufanya sherehe za harusi zao pasipo kuomba michango Kwa ndugu/jamaa na marafiki. Wao hugharamia Kila kitu wao wenyewe na hao ndugu/jamaa na marafiki hupewa Kadi za mwaliko kuweza kuhudhuria sherehe tu.

Kwa utafiti usio rasmi, sherehe za harusi hupendwa zaidi na Wanawake kuliko Wanaume. Wanaume wako tayari kufunga Ndoa za kimya kimya lakini sio Wanawake.

Je, ulitumia fedha kiasi gani kufanikisha harusi yako ama umepanga kutumia fedha kiasi gani kwaajili ya harusi yako na mwenzi wako?

Binafsi, nilitumia kiasi cha shilingi milioni 10 kuweza kufanikisha harusi yangu na Bibi yenu miaka kadhaa iliyopita 🤗🙏

Sikuhitaji kuchangiwa fedha kufanikisha sherehe ile, bali niliweza kujipanga mwenyewe Kwa muda wa miaka 5.

Nilifungua akaunti maalumu Benki (Fixed deposit account) ambayo nilikuwa nina ruhusiwa kuweka fedha pasipo kutoa Kwa muda wa miaka 5 hivi, japo nilikuwa napata interest kidogo za Benki.

Baada ya miaka 4 hivi, nilikwenda kuchungulia fedha nikakuta nina milioni 9.35 so nikaanza maandalizi kujiandaa na harusi Mwaka unaofatia.

Mind you, tayari nilikuwa nina Cheti cha Ndoa ya Serikali na mwenzangu lakini yeye Kiu yake ni lazima tukafunge ile ya Kanisani 🙌

Kuna wakati nilikuwa nafanya biashara ya kununua na kuuza mazao ya nafaka. Nilikuwa naenda Mashambani, nawakopesha fedha Wakulima then wakati wa mavuno nilikuwa naenda kukusanya mazao hasa zao la Mpunga.

Kwahiyo kwenye ile harusi, sikuwa na hofu ya Chakula maana tayari nilikuwa nina stock ya magunia ya kutosha ya Mpunga.

Wanasema harusi ni kula na Kunywa. Kwahiyo nilijiandaa kwenye eneo hili.

Kwenye upande wa Chakula niliandaa wali mweupe,Pilau, chips, mtori, nyama za kukaanga, kachumbali

Vinywaji niliandaa Soda na Maji tu.

Niliandaa Kadi za Mwaliko za watu 300 lakini walifika watu 358 japo hili nilijua lazima lingetokea maana harusi yenyewe niliifanyia Kijijini kwahiyo wengi ni wale watu mnajuana. Kwahiyo niliweka chakula na Vinywaji Kwa zaidi (excess budgeting)

Pamoja na Wageni waalikwa, usiku ule nilikuwa na Mchungaji pamoja na Mwinjilisti ambao walishiriki kuanzia mwanzo wa harusi hadi tunamaliza tukio majira ya saa 9 usiku.

Gharama za mavazi za Wapambe niligharamia mwenyewe kuanzia mavazi ya Kanisani hadi Ukumbini 🙌

Niliamua kukodisha Ma-MC wawili ili kunogesha sherehe 🤗

Pete nilinunua zenye ppt ya dhahabu, kuogopa zisije kupauka.

Mchanganuo wa Bajeti yangu kufanikisha sherehe ile, nimeambatisha kwaajili ya wengine kujifunza.

Kumbukeni, hata kama umeoa bado unaweza kuja kuozesha watoto wako miaka ijayo. Baadhi yetu mnaweza kuwa Wanakamati kwenye harusi za wengine pia

Kwahiyo Harusi zitaendelea kufanyika hata baada ya kufa kwetu maana tutakuwa tumeacha Kizazi chetu kinaendelea Kuoa na kuolewa.
Nilitumia milion 20 tuuuu
 
Back
Top Bottom