Ulitumia kiasi gani cha fedha ama umepanga kutumia kiasi gani cha fedha kugharamia harusi yako?

Mi nilikuwa na watu 6 kamati,kikao dk 20 basi,na budget yetu ilienda vizuri kabisa 25m , Harusi ilifungwa DSM,ukumbi Golden Memory -Sinza
 
Mie pia nilikua na kamati ndogo nzito...harusi ilikua ukumbi wa moja ya fukwe za hotel...ma mc walikua wa tatu..wawili watangazaji wa redio maarufu za mjini...ilikua na section ya ma djs wa town kadhaa..vigoo kadhaa wa vyama na serikali....
Hapo lazima kulikuwa na mashoga waliohudhuria.
 
jamii ya mabanianai wafanyabiashara na wanaojua nini mana ya maisha walishaachana na huu ushamba wa kufanya sherehe kubwa za ndoa kwa kuchanga pesa na kuzipeleka kwenye ukumbi na ushamba kama huo

wao huchanga pesa na kuzitumia kukuza mji wa anae oa na sherehe hufanyika hapohapo kwenye huo mji mf kamati ikichanga ml30 jua hizo zitatumika kujenga au kukuza mji na sherehe itafanyika apo na ni kwa muda mchache watu wanatawanyika kuendelea na shuhuli zao

wabongo masifa sasa sherehe kwanzia kwa mke hadi ndoa jumla 90m bada ya shuhuli zote wanakwenda kupanga huku mchango wa pesa zote wamewatajirisha watu wa ukumbi na ndoa ni yao
 
Mi nilikuwa na watu 6 kamati,kikao dk 20 basi,na budget yetu ilienda vizuri kabisa 25m , Harusi ilifungwa DSM,ukumbi Golden Memory -Sinza
Hongera sana Mkuu, budget ya 25M sio mchezo

Natamani kujua japo kidogo, kwenye kiasi hicho cha Fedha, component ipi ilikuwa na gharama kubwa
 
Kubadirika hapo sio rahisi, nadhani Kuna haja tuendelee kupewa somo pengine tutaelewa mbele ya safari

Japo hoja yako ina mashiko sana. Vipi hicho kiasi kingekuwa kinachangwa kumpa Mtaji Bwana harusi 🤗
 
Nikikumbuka harusi yangu😂
1. Muziki 50000/=
2. Ukumbi wa kanisa 25000/=
3. Usafiri wafanyakazi wenzangu niliwapa ten ten magari matatu
Mengine nikikumbuka nacheka sana😂 Bora niishie hapahapa
 
Sitofanya sherehe ya harusi...
Gauni langu nataka liwe zuri sanaaa... nipige picha za ukumbusho nikitoka kanisani

Baada ya kanisani kila mtu akale kwao!
This will never happen, wewe tutakuozesha Kwa harusi kubwa.
Jiandae kisaikolojia
 
Hicho kiasi kilitosha kugharamia nini na nini Mkuu?

Nahisi haikuweza kutosha kununua hata koti na necktie
Ndoa ya kiislamu, kanzu na kilemba nlikuwa navyo tayari, shela la Bi harusi tulikodi Kwa 20k tu, 10k nilimpa aliyenifunga kilemba kichwani. 20k nilimpa mdogo wa mke wangu ambae aligoma kupisha mlangoni wakati naondoka na dada yake Hadi nitoe chochote kitu.
Msafara wa magari matatu langu moja na mengine walijitolea washkaji wa kazini kwangu, mpiga picha pia alikuwa mshkaj wa kazini ambapo alitumia camera ya ofisini pia. Hayo yote ni nje ya mahari.
Nkarudi nyumbani na mke kiroho safi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…