Ulitumia kiasi gani cha fedha ama umepanga kutumia kiasi gani cha fedha kugharamia harusi yako?

Somo zuri Kwa Vijana hili
Kuna mengi ya kujifunza sana kupitia harusi ambazo tunaenda! Mjomba wangu alikwenda kuoa sehemu kwa ujasiri aliwaambia kabsa kuwa hana kipato cha maana enzi hizo 1990s na baba mkwe alikuwa afande! Alimpatia binti yake na wapo pamoja mpaka leo! Kuna swahiba yake na Mjomba alitusimulia kisa hicho nikasema ni ngumu sana kukutana na sampuli hizo katika nyakati hizi. Watu walitoka Sengerema mpaka Tinde kwa ajili ya kufuata binti!
 
Hongera sana Mkuu, nimependa kwamba ulitenga na Fedha ya dharura 👏👏🙌
Siku ya harusi ilitokea dharula ya kulipia kila sahani ya chakula inayoingia ukumbini, hivyo pesa ya dharula ikasaidia eneo hilo.
 
Siku ya harusi ilitokea dharula ya kulipia kila sahani ya chakula inayoingia ukumbini, hivyo pesa ya dharula ikasaidia eneo hilo.
Tuipe hongera Kamati yako ya maandalizi, ilikushauri vizuri aisee 👏👏

Otherwise usingefanikiwa kutoboa
 
Tinde ile ya Shinyanga?

Wazee wengi wa zamani walikuwa waelewa kuliko wa miaka ya hivi karibuni.

Japo nahisi kukosekana Kwa u-seriousness miongoni mwa Vijana wa sasa huenda umechangia

Vijana wengi wanapenda kuchezea mabinti za watu
 
Tuipe hongera Kamati yako ya maandalizi, ilikushauri vizuri aisee 👏👏

Otherwise usingefanikiwa kutoboa
Uzuri mhazini nilikuwa ni mimi mwenyewe hivyo pesa zote nilikuwa nalipa kwa mhusika wa tukio moja kwa moja bila kutumia middle men.
 
Mbona gharama kubwa sana yan 10 M kasoro[emoji55]kumbe harusi gharama hivi!
 
Mbona gharama kubwa sana yan 10 M kasoro[emoji55]kumbe harusi gharama hivi!
Mkuu harusi hutegemeana na vile utakavyokuwa umejiandaa

Kuna ambao hutumia gharama za less than 3M, wengine less than 10M na wengine huenda hata 20M and above

Mkiwa mna nia ya kufanya sherehe ya harusi, anzeni Mipango mapema

Harusi huwa nzuri mkijiandaa mapema
 
Uzuri mhazini nilikuwa ni mimi mwenyewe hivyo pesa zote nilikuwa nalipa kwa mhusika wa tukio moja kwa moja bila kutumia middle men.
Hiyo Mkuu ilisaidia sana, japo najua baadhi ya Wajumbe wa Kamati hawakupendezwa na utaratibu huo

Kuna watu wanapiga hela kupitia kamati za harusi za watu 😜
 
Tinde ile ya Shinyanga?

Wazee wengi wa zamani walikuwa waelewa kuliko wa miaka ya hivi karibuni.

Japo nahisi kukosekana Kwa u-seriousness miongoni mwa Vijana wa sasa huenda umechangia

Vijana wengi wanapenda kuchezea mabinti za watu
Ndio Mkuu Tinde ya Shinyanga! Hapo miguu ilifanya kazi! Wakati ule hata mahari tu inapelekwa na mbio hatari.
 
Kwahiyo, hizo hela zote ukazichoma kwa siku moja?

Hela unaivujia jasho miaka 5 ili utumie kwa siku moja kisa sherehe. Hizo pesa ungemtunzia mwanao si angekushukuru baadaye au zingeendelea kukaa kwenye serving si ungekuwa na mpunga mzuri.

Ukute umechomwa pesa kufanya sherehe na mwanamke anakukimbia.

Mimi katu sitakuja kufanya hizo sherehe za kuoana. Mwanamke nimemtolea mahari, amekuja kwangu tumezaa watoto, tunalea na kuishi kwa heshima. Na nimemkataza asije leta habari za sherehe, oo mara nikafunge ndoa kanisani, huo ujinga sifanyi.
 
Umeongea hoja ya msingi sana. Binafsi niliwahi kupiga stori sana na Marehemu Bibi! Aliwahi kunihimiza kuwa Niulize maswali magumu wakati wa uchumba, nimuulize mwenzangu kuwa anatamani maisha ya namna gani, na anataka kuishi maisha gani? Muulize anatamani watoto wake waishi maisha gani? Muulize fedha na mali zina nafasi ipi kwenye maisha yake? Muulize kuwa endapo ukipata ajali, atabakia au ataondoka? Muulize kwa macho makavu kabsa!​
 
Kuachana ni matokeo tu, hakuna anayeoa ili waje kuachana

Kuna watu wameoana kimya kimya lakini wakaja kuachana.

Wanasema tuishi nao Kwa akili Hawa viumbe (Wanawake).
 
Unadhani kwenye hayo maswali anaweza akajibu tofauti na matarajio yako?

Tuishi nao Kwa akili tu
 
Ndio Mkuu Tinde ya Shinyanga! Hapo miguu ilifanya kazi! Wakati ule hata mahari tu inapelekwa na mbio hatari.
Hahaha........ hongera sana Mkuu, muhimu ulitimiza lengo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…