Ulitumia mbinu gani kumfanya Mtoto wako aache kulala chumbani kwako?

Ulitumia mbinu gani kumfanya Mtoto wako aache kulala chumbani kwako?

Bado sana hao watoto wanaweza kulala na kwa mzazi hadi umri wa miaka 9 anaweza kuwa bado anakuja kulala chumbani kwako mzazi. Ukishakuwa na watoto unaweka rehani sehemu ya uhuru wako.
 
Hebu naomba mnisaidie hapa jaman ili niweze kuwahamisha hawa Watoto chumbani kwangu (Miaka 4&2). Imekuwa vita ya muda mrefu sana hawataki kulala kwenye Chumba chao, wanalazimisha kuendelea kulala kwangu

Hata nikisubiri walale halafu niwahamishe wakishtuka kwenye zoezi la kuhamishwa mtanange unaanza upya, walalia kama ndio wanakufa siku hiyo 😀 😀 😀 😀😀😀

Wenzangu mlifanyaje kwenye hili?
Hata hili linahitaji ushauri? Kizazi cha wazazi dhaifu
 
Mnawadekeza sana watoto.
Ni kuwakunjia tu sura na kuwaambia ni marufuku kulala chumbani kwangu. Watoto wanaelewa.
Huyo wa miaka minne akielewa basi na mdogo wake ataelewa taratibu.
Mtu anakwambia chumba changu kifanyeni stoo Mimi nabaki humu humu halafu anaendelea na shughuli zake
 
Kuna mmoja nilitimua akalala ilipofika saa tano usiku akanigongea kufungua akaniaga "mama Mimi nakufa na nguo zangu nahisi atachukua "Y" (binamu), nikamjibu haya usiku mwema nikafunga mlango asubuhi nikamsalimia "hujambo akajibu sijambo" nikamwambia hicho ndio chumba chako tusisumbuane
 
Hebu naomba mnisaidie hapa jaman ili niweze kuwahamisha hawa Watoto chumbani kwangu (Miaka 4&2). Imekuwa vita ya muda mrefu sana hawataki kulala kwenye Chumba chao, wanalazimisha kuendelea kulala kwangu

Hata nikisubiri walale halafu niwahamishe wakishtuka kwenye zoezi la kuhamishwa mtanange unaanza upya, walalia kama ndio wanakufa siku hiyo 😀 😀 😀 😀😀😀

Wenzangu mlifanyaje kwenye hili?
Wazungu kuanzia kakiwa kichanga kanalala kwenye kitanda chake kile cha kutumbukia huko sebleni. Kakishtuka ucku wanaamka kuja kukatizama.
 
Suluhisho ni hili. Waache watoto walale kwenye chumba hicho hicho lakini tafuta godoro la pili litandike sakafuni ili kwamba mchepuko wako akifika mfanye mambo yenu chini.
Kamwe usiwalaze watoto chini kisa unataka kufanya tendo la ndoa kwa kitanda, hiyo ni mbaya.
 
Hebu naomba mnisaidie hapa jaman ili niweze kuwahamisha hawa Watoto chumbani kwangu (Miaka 4&2). Imekuwa vita ya muda mrefu sana hawataki kulala kwenye Chumba chao, wanalazimisha kuendelea kulala kwangu

Hata nikisubiri walale halafu niwahamishe wakishtuka kwenye zoezi la kuhamishwa mtanange unaanza upya, walalia kama ndio wanakufa siku hiyo 😀 😀 😀 😀😀😀

Wenzangu mlifanyaje kwenye hili?
Moyo wa mtoto umejaa na ujinga fimbo itautoa, sasa wewe waendekeze
 
Jinsia gani kwani?
Kama wa kike, wapeleke chumba kwao mbembleza hadi walale
Kama wa kiume fukuza chumbani kwako, Ata Kwa kulala usiwaonyeshe , watajua Wenyewe wakitaka walale sebuleni kwenye sofa
Huko ni kuwanyanyasa watoto miaka miwili na minne awafukuze eti watajua wenyewe!! aendelee kulala nao huku akiwafundisha taratibu kulala chumba chao mwisho watazoea bado wadogo hao inaonekana hujazaa bado
 
Hii sio sawa kwa ustawi wa familia. Kila kitu inatakiwa familia ijumuike pamoja isipokuwa muda wa kulala tu watoto walale chumba chao.

Sasa huyo jamaa hata kula tu anawatenga watoto? Ana uhakika gani huko jikoni kama watoto wanakula vizuri wanashiba? Usikute beki tatu ndio anabugia minofu yote watoto wanaambulia mifupa tu.
Umesema kweli, wazazi kama hao wanasumbuliwa na uchoyo siyo vyema kuwatenga watoto
 
Hamia chumbani kwao kwa muda, wakilala unasepa
Hivi inachukua mda gani had mtoto azoee?Nina karibia mwaka sasa napambana…dogo akiamka anakuja kugonga mlangoni,basi shughuli yangu ni kuhama vyumba tu usiku had natamani kulia 😒
 
Huyu mdogo ilibidi nianze na affirmations za hapa na pale, kidogo kidogo.

Nikaanza kumwambia ‘you’re a big girl now’. Nikapamba chumba chake na posters za Dora the Explorer.

Nikamwekea ka TV kadogo ili awe anaangalia vitu anavyopenda.

Akiwa na usingizi akika kuniambia anataka kulala, namchukua tunaenda wote chumbani wake, namlaza.

Nimeenda naye hivyo mwishowe akazoea.
 
Back
Top Bottom