LA7
JF-Expert Member
- Aug 26, 2019
- 655
- 2,369
Ndugu zangu humu hamjambo wote?
Humu ndani kuna wakati tunakuwa au tumewahi kuishi kwa watu au ndugu, lakini huwa baada ya kuishi kwa kipindi fulani mkiwa pamoja linakuja suala la kuchokana au kuchokwa. Hii inatokana na wewe kuhitaji msaada wao zaidi hasa wa hifadhi na chakula.
Sasa mimi nakumbuka nilipoacha kazi kwa Wahindi nikaenda kuishi kwenye familia moja huko Gongo la mboto, kutokana na maisha ya hiyo familia kuwa ni ya hali ya chini hivyo ilibidi nitumie akili sana ili wasinichoke.
Kwanza kabisa ilikuwa nikienda baharini kuvua samaki, nikirudi nabeba samaki kama wa 20,000 hivi maana nilikuwa nikienda Msasani au Feri nilikuwa namaliza hata mwezi ndio nashuka Gongo la mboto.
Baada ya kucha kazi ya uvuvi nikawa tu pale nyumbani, sasa ilikuwa maji ni ya shida kidogo ila uyapate ni umbali kama wa Km 1 hivi, kwahiyo nilihijitahidi sana maji yasiishe ndani, na kunawakati nikipiga saidia fundi narudi nyumbani na mazaga ya kula pale nyumbani. Kuna wakati nilimsaidia mama kufua, kufanya usafi wa ndani, kupika hasa ugali.
Nilifanya mambo mengi tu, ila zaidi ni baada pia ya kuonyeshwa upendo na ile familia.
Mpaka leo hii huwa wanatamani nirudi japo nilishajitegemea. Ila nikienda kuwasalimia mwendo ni ule ule, japo zingine mama ananiambia niache maana nimeshakuwa na familia na mimi.
Pia Mungu aibariki ile familia, nilijuana nao toka 2014 mpaka leo hii tumekuwa kama ndugu.