Ulivyokuwa mdogo ulikuwa na ndoto ya kuja kufanya kazi gani?

Aisee ...mie nilitamani kuwa mtaalam wa kutengeneza mabomu ya nuclear...mwe! Saa hivi nafukuzia upepo na boxer yangu. Maisha haya acheni tuu
 
Hiyo ndiyo ukisikia kusomea ujinga.
 
Hahahahaha, we kweli ulikuwa mdg...
 
Nilitaka kuwa daktari,,,, nimesoma na kuhitimu,,,,
Ila sasa niko jobless….🥹🥹🥹🥹🥹
 
Nilitaka kua Pilot. Ila hesabu zilianza kunipiga chenga tangu primary😂 niliaminishwa bila ufaulu mzuri wa hesabu sitoboi. Nikaanza kuhusudu kuwa mtu wa Usalama wa Taifa (TISS) Lakini nikaona taasisi imeianza kua ya kisiasa zaidi. Kwa sasa ni mwanasheria, japo sijatoboa bado kimaisha lakini nafurahi fani yangu. Nikifa na kuzaliwa tena bado nitachagua kua mwanasheria😊
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…