Ulivyokuwa mdogo ulikuwa na ndoto ya kuja kufanya kazi gani?

Ulivyokuwa mdogo ulikuwa na ndoto ya kuja kufanya kazi gani?

Ulivyokuwa mdogo ulikuwa na ndoto ya kuja kufanya kazi gani?
»uDaktari
✍️
 
Ndoto yangu kubwa ilikuwa nisomee sheria na nije kuwa muajiriwa wa Usalama wa Taifa.

Hii ndio kazi ya ndoto yangu basi tu sikubahatika nayo.
 
Pilot, doctor na Dereva simultaneously! Nimekuwa napigia mbuzi gitaa na watoto wananawiri Kama avatar yangu tu!
 
Leo nimekumbuka kipindi nipo mdogo nilikua na ndoto ya kuja kua Miss Tanzania.

Akili yangu yote ilikua inajua Miss Tanzania ni kazi kama daktari, mwanasheria, mwalimu au kazi zingine.

Nilivyofika form 1 ndo nikajua kumbe sio kama nilivyodhani, hapo nikapata mawazo ya kua mwanauchumi mpaka sasa napambania ndoto yangu.

Mliotimiza ndoto zenu nyoosheni mikono juu tuwapigie makofi!😹
Dah! yaani ulikuwa na mawazo ya kujiuza mwili wako kuanzia mdogo?
 
  • Kicheko
Reactions: EEX
Kuuza mafuta ya nishati (vituo vya mafuta) nilikua najua zile Hela ni za wale wahudumu🤣🤣 nilipo kuja jua ukweli NILICHOKA.
 
Watu wengi humu mawazo ya utumwa tu.

Ndiyo maana Waarabu na Wahindi wanatupiga mabao.

Wao wanafikiria wafanye biashara gani , waajiri watu wangapi. Nyie mnafikiria kuwa watumwa?
 
  • Thanks
Reactions: EEX
Nilipokuwa mdogo nilitamani kuwa parde, nikajiunga na shirika la St. Aloysius nikawa natumikia misa. Nikasoma seminary miaka mingi mpaka advance.

Ndoto ikafa baada ya kuona askofu ana mtoto ni padre, sister katiwa mimba na jamaa yangu mseminary, parde anatoka ibada anawasha fegi.

Nikaona isiwe kesi nikagoma kwenda major seminary nikawa chalii wa mtaa mpaka sasa nimekuwa mhuni kupindukia. Kanisani siendi, huwa sisali, siamini uwepo wa Mungu.

Ila nalishukuru kanisa kwa elimu niliyopata imenifungua kuhusu mambo mengi.

Crazy twist of the plot.
 
Mi nilitamani nisome wild life maana napenda wanyama lakini ndo hivyo tena nikaishia kusomea ualimu, ila kwa sasa nafuga kuku na nyau tu
 
Watu wengi humu mawazo ya utumwa tu.

Ndiyo maana Waarabu na Wahindi wanatupiga mabao.

Wao wanafikiria wafanye biashara gani , waajiri watu wangapi. Nyie mnafikiria kuwa watumwa?
Ndio maana umeamua kuuza bandari sio? Si biashara hiyo?
 
Back
Top Bottom