Uliwahi kula vyakula gani kutoka sehemu mbalimbali Duniani ukafaidi?

Kaka Mimi niki taka oa Nita tazama vyakula kutoka tanga, tabora, Ethiopia, au somalia hapo.

Hizo sehemu zina vyakula vyenye ladha murua. Sana, hata wapishi wajua kazi yao.
 
Loh! Paskali sikupata wasaa wa kusoma huu Uzi wako wa kula vyakula tofauti tofauti toka makabila tofauti tofauti hapa nchini na pia nje ya nchi. Nakumbuka tulipokuwa pale Kibiti na Ikwiriri wakati ukiwa na RTD kwenye Disco, kulikuwa na vyakula vitamu vya Wandengereko. Nina hakika ulivifaidi sana. Miaka inakwenda, ila nadhani unayo kumbukumbu ya vyakula hivyo. Umenifurahisha sana kwa kunikumbusha enzi hizo. The good old days!
 
Loh! Paskali sikupata wasaa wa kusoma huu Uzi wako wa kula vyakula tofauti tofauti toka makabila tofauti tofauti hapa nchini na pia nje ya nchi.
Ni kweli kama ni kula tuu, kiukweli tumekula sana, tungekuwa Wachagga saahizi tuna maghorofa kadhaa tumejenga, wakati wenzetu wanajenga kwenda juu,sisi wengine tumejengea chini!.
Duu..., Kutata ,@kutatabhetakule, umetisha!, umenikumbusha mbali!, vyakula vya Wandenge!, hatari!, mtu unamaliza ile standard three course meal, unaletewa desert, unajikuta unabugia tena bila hata kunawa!, na Ikwiriri ndio hatari zaidi , sio vya Wandenge tuu, hadi vya Wabulushi!, tumeacha vialama alama hapa na pale!, kusema ukweli mtu kuwa mtangazaji wa RTD enzi za redio moja halafu wewe ndio DJ, kiukweli ni mitihani!.
P
 
Sema tanga inasifiwa sana nina shauku ya kujaribu CHAKULA cha tanga even though najua hakita reach the hype. Duh inapewa promo mnoo
 
Uende Nachingwea Kwa wamwera kaka.
 
Uende Nachingwea Kwa wamwera kaka.
Nachingwea sijafika vyakula vya wamwera sijakula, ila siku hizi umri umesonga sana siwezi kutafuna nyama, siku hizi ni kula kwa macho tuu au mara moja moja sana vyakula laini laini kama maini!
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…