Uliwahi kula vyakula gani kutoka sehemu mbalimbali Duniani ukafaidi?

Uliwahi kula vyakula gani kutoka sehemu mbalimbali Duniani ukafaidi?

Huu uzi nimegundua kuna jinsia wametengwa kiaina kwa sababu wanajua wakisema vyakula walivyokula kuna maeneo hukumu itaambatana nao. Ila naona vyakula vya Tanga havijaacha kusifiwa. Naongezea kura yangu hapo.

Pia najazia kama alivyosema bamdogo Pasco kuwa vyakula vinavyoonekana kwa nje ni vya kawaida ni vitamu kuliko mtizamo wake. Wale wa ''ndanindani'' na wanaoonekana hawajui kujipara wana balaa.
 
Nipasuke msamba aku babu, hivi list ya pasi umeiona?
List isikuogopeshe, ukipita kwenye meza ya buffet, sio lazima kula kila kitu, unaweza kuonja tuu kwanza, ukijiona ni kitamu, na umependezewa, ndipo unajipakulia na kwenda kujilia zako.

Mfano, leo ninapoandika hapa, niko zangu Mtwara, ndio najishauri nikapige menu wapi..., nishuke restaurant, niitishe room service, au nikachukue take away.

Kama mtu unapenda kulo misosi mizuri, hali ya mfuko inakuruhusu kula vitu vizuri, na viti vizuri vya kuliwa vipo plenty!, why not?., ni unajilia tuu ...
P
 
Nikajua umeacha kula mahotelini kumbe bado hata mama ntilie unakulaga, na wewe ndo mtu mzima hivyo je hawa walio kwenye 30-40 si ndo watalala huko huko vibandani wakila na makombo, wanaume punguzeni uroho
 
Kuna aina 3 za walaji wa vyakula vya hotelini.
1. Wasafiri, unapokuwa safarini, unajikuta lazima ule vyakula vya hotelini hivyo hawa ni walaji wa hotel in need, lazima wale hotelini.
2. Wale ambao wanaboreka na chakula cha nyumbani, hivyo wanakula hotelini kwa hamu tuu.
3. Kundi la 3, ni diners, hawa ni regular, wanakula hotelini not for need but for choice, mimii ndio niko kundi hili.

Mimi nilioa very young na wife ni classmates wangu, wale school sweethearts. I was 25, she was 21. Tukaondoka bongo, tukahamia UK, our first born akazaliwa kule, tukahamia US, our 2nd born akazaliwa kule. Kule wife akapata scholarship ya 4 years, hivyo ikanibidi mimi na watoto turudi Bongo. Tulikuwa tunakula nyumbani Monday to Thursday's, from Friday night, Saturday's and Sunday's ni kula out.

After 4 years, akaongeza 2 years za Ph.D, hivyo 6 years. na baada ya hapo nikampelekea watoto, mimi nikarudi Bongo, ikawa sihitaji tena kula home, mimi nikawa ni mtu wa eating out kuanzia chips vumbi, takeaways na dinning out.

Hii sasa kula hotelini imegeuka tabia, nikisafiri ndio kabisa, lazima nile vyakula vya huko nilipo, ndio mpaka leo, mpaka kesho, mimi na misosi ya hotelini, misosi ya hotelini na mimi. Hii sasa ni tabia.

Dah umetisha kwahiyo kilichopikwa home kichache kimwagwe au hotelini unakula ukirudi home napo unakula? Kwani ukifunga chakula kutokea nyumbani ukaenda nacho kinapungua utamu?
 
Dah umetisha kwahiyo kilichopikwa home kichache kimwagwe au hotelini unakula ukirudi home napo unakula? Kwani ukifunga chakula kutokea nyumbani ukaenda nacho kinapungua utamu?
Wanaume wa Kiswahili hatuna utamaduni wa kufungasha vyakula, labda wenzetu wazungu na wanawake.

Siwekewi chakula home, huwa nakula mchana tuu siku nipo, na nakula home kile cha usiku, siku akiwepo, lakini nikisafiri, ni kula hoteli tuu.

Kuna siku zinatokeaga, unapita mahali anatamani kuonja chakula cha nje, huku home, chakula cha ndani kinakusubiri, unaonja cha nje, na ukifika home, unazuga kula cha ndani, na kujifanya umechoka sana, unapiga tonge moja, mbili kuzugia tuu ili usishtukiwe umeisha kula, na kujifanya umechoka sana ili usile kile chakula cha usiku. Enzi zile za ujana, unakula chakula cha nje, na ukifika ndani, unakula tena na cha nyumbani .

Hakuna kitu kinatuumiza kama msipokula chakula tunachowaandalieni nyumbani na kuishia kukimwaga
 
Hakuna kitu kinatuumiza kama msipokula chakula tunachowaandalieni nyumbani na kuishia kukimwaga
No mimi kwangu, hata kama sili, hatumwagi chakula, kesho yake mchana napashiwa. Nina bahati sana wife sio Mwanamke wa kupika type, she is a working class with no love na kupika, hivyo mpishi ni dada, ule, usile, it makes no difference, ila usipokula kile chakula cha usiku, ni kesi, ndio maana unakula nje, unashiba, ukifika ndani unakula tena as if haujala.

Pasco, chakula cha usiku unachomaanisha ni kipi?
 
Wanabodi,

Sisi binadamu tofauti tofauti tuna hobies mbalimbali, wengine wanapenda kutulia sehemu moja, wengine wanapenda kusafiri safiri.

Mimi hobby yangu ni safari, na kula. yaani travelling na eating delicious meals na feasting on anything good! Yaani napenda sana kusafiri na kula vitu vizuri.

Mastori.

Nikiwa shule nilipenda kusomea sheria ili niwe mwanasheria, lakini kwa vile nilikuwa kijana ambaye damu inachemka sana, nikiwa sekondari ya Ilboru, na baridi la mlima Meru, nikajikuta sijatulia hivyo kukosa division 1, ya kuingia sheria.

Enzi zetu ukimaliza form six lazima upite jeshini JKT kwa mujibu wa sheria, na kufuatia mimi kusoma Shule za boys only, Tambaza na Ilboru, jeshini ndio sehemu yangu ya kwanza ya ujana kuchanganyika na wasichana.

Nilipangiwa JKT Makotupora Dodoma, mabweni ya kiume waliita Ngorongoro na ya kike Serengeti. Japo wengi jeshini waliona ni mateso lakini baadhi yetu ile kuangalia tuu wanyama wa Serengeti, kwetu raha!.

Kwa vile napenda kula, JKT ndiko nilikoanza kuharibikia maana misosi ni ya kumwaga!. Ilikuwa ni kata mti, panda mti, unajilia tuu!.

Kufuatia kuona raha sana jeshini, mtu ukikipenda kitu unakifanya vizuri kwa moyo wa kujituma, hivyo jeshini nikawa a very good performer kwenye somo la kulega shabaha, yaani nilikuwa sharp shooter, nikilenga, nagonga, na hit the bull!. Post za chuo kikuu zilipotoka nimekosa sheria!.

Hivyo baada ya kumaliza JKT nikapelekwa moja kwa moja kujiunga na JWTZ na kupiga deppo mpya ya JW pale Airwing Ukonga kusubiria kwenda cadet.

Jeshini JWTZ ndipo nikajigundua sijatulia kupokea kila amri, jeshi linataka nidhamu ya hali ya juu, mchana ni mafunzo na usiku ni kupumzika, kufuatia mimi kupenda kula, ikawa mchana ni mafunzo na usiku ni hakuna kulala!, ni unakimbizana na misosi ya mitaani!.
Jeshi likanishinda!.

Ndipo nikajiunga na chuo cha uandishi wa habari TSJ enzi hizo kiko Ilala Bungoni. Serengeti na Ngorongoro za TSJ ziko mkabala, hivyo kwa upande wa misosi ni kujilia tuu!. Kumaliza TSJ nikapostiwa RTD, na kujichukulia jumla ka swala fulani ka TSJ.

Kazi ya uandishi wa habari inahusisha kusafiri sana, ni trips na trips na kila nikisafiri mahali popote hupendelea sana kula the local foods za mahali hapo.

Japo baadaye, huku nikiwa ni mwandishi wa habari, nikikuja kusoma sheria, lakini kufuatia kupenda trips na kula, niliendelea na kazi ya uandishi wa habari, ila sasa naelekea 60, nimeanza kuzeeka, hivyo kupunguza kula maana meno hayawezi tena kutafuna sana nyama, labda vitu laini laini kama maini na vi spring chicken mara moja moja!.

Vyakula tofauti tofauti vina tastes tofauti tofauti, kuna vyakula kwa kuvitazama tuu kwa macho unaviona they look good to taste hivyo ukila utafaidi lakini unapokula unakuta ni tasteless, na kuna vyakula kusema ukweli ukivitazama machoni kama zile nyama za mnadani, they don't look so good au mazingira kama ya kwa Mromboo pale Arusha, mazingira ni horrible fulani but the meat is so good, so tasty!, ukila una enjoy!, hivyo don't judge the book by its cover!.

Wewe unaweza kukumbuka baadhi ya vyakula ulivyokula vya makabila, jamii, na mataifa mbalimbali? Vipi ulifaidi, ukikumbuka unajisikia raha?

Kwa upande wangu nimewahi kula vyakula vya makabila haya, jamii hizi na mataifa haya;
  • Moshi Wachagga wa Kirua Vunjo​
  • Moshi Machame​
  • Moshi Kibosho​
  • Moshi Siha​
  • Moshi Wapare​
  • Arusha Waarusha​
  • Arusha Wameru​
  • Arusha Wamasai​
  • Babati Wambulu​
  • Singida Wanyaturu​
  • Singida Wanyiramba​
  • Dodoma Wagogo​
  • Morogoro Wapogoro​
  • Morogoro Waluguru​
  • Morogoro Wakaguru​
  • Pwani Wadengereko​
  • Dar es Salaam, Wazaramo​
  • Iringa Wahehe​
  • Iriga wabena​
  • Iringa Wakinga​
  • Mbeya Wanyakyusa​
  • Songea Wangoni​
  • Songea Wanyasa​
  • Tanga Wasambaa​
  • Tanga Wadigo​
  • Tanga Wabondei​
  • Bukoba Wahaya​
  • Bukoba Wahangaza​
  • Lindi Wamachinga​
  • Mtwara Wamakonde​
  • Musoma Wajita​
  • Tarime Wakurya​
  • Ukwerewe Wakerewe​
  • Mwanza Wasukuma​
  • Tabora Wanyawezi​
  • Zanzibar Wazanzibari​
  • Pemba Wapemba​
  • Mafia Wamafya​
  • Kigoma Waha​
  • Kenya Wakikuyu​
  • Kenya Wakamba​
  • Uganda Watoro​
  • Uganda Waganda​
  • Uganda Wanyankole​
  • Rwanda Wanyarwanda​
  • Burundi Warundi​
  • Zambia Wazambia​
  • Malawi Wamalawi​
  • Msimbiji Wasumbiji​
  • Angola wa Mulato​
  • Swaziland Wazwazi​
  • Lesotho Wasotho​
  • South Africa Wazulu​
  • South Africa Wakhosa​
  • South Africa Africans​
  • Zimbabwe wa Matebele​
  • Malawi Wamaawi​
  • Congo Wakongo​
  • Ghana Waghana​
  • Liberia wa Liberia​
  • Cote d'ivoire Wakote​
  • Ethiopia Wahabeshi​
  • Sudan ya Kusini Wasudani​
  • Somalia Wasomali​
  • UK Waingereza​
  • US Waamerica​
  • Swiss Wa Swiss​
  • Italy Wataliano​
  • Sweden wa Swedish​
  • Norway wa Norwegians​
  • Finland wa Fini​
  • Germany Wajerumani​
  • Poland wa Polish,​
  • Canada wa Canadian​
  • India Wahindu​
  • Russia Warusi​
  • China Wachina​
  • Japan Wajapan.​
Ukisafiri ukifika popote ukalala hata kwa usiku mmoja, hakikisha usiishie kula vyakula vya hoteli tuu, toka nje, walk around, grab a local taxi, madereva taxi wanajua wapi you can get a local good tasty meals, kama unapenda kula kila ukisafiri hakikisha you feast the good stuff kuonja difference taste!.

Kwa vile leo tumeanza Kwaresma, baada ya Kwaresma nitarejea kwenye uzi huu niwape mastori ya kwa upande wapi vyakula vya wapi ni vitamu na nilifaidi!.

NB. Kwa vile vyakula vipo vya aina nyingi, na vinaliwa wakati tofauti tofauti, mfano cha asubuhi ambacho ni breakfast, cha mchana ambacho ni lunch, na cha usiku ambacho ni dinner, it's worldwide believed kuwa kitamu zaidi sio cha asubuhi au cha mchana bali ni cha usiku!, hivyo hapa mimi nazungumzia kile 'chakula cha usiku!'!, na ndio maana mialiko mingi ya chakula cha usiku hutanguliwa na kualikwa dinner au kutolewa out, kisha unaishia kujilia!.

Kwa leo nawatakia Kwaresma njema.

Paskali
Masikini Pascal! Nafsi haikusuti?
Kwa usalama wako ni bora tu uokoke!
 
Vyakula vya kichina - hivi nimekula kwa miaka mingi, jamaa wana mapishi lukuki na misosi yao ni mitamu haswa (miaka ya nyuma nishawahi weka uzi) cc Mshana Jr, kuna jamii ya Wachina wanatokea jimbo la Xinjiang kaskazini magharibi mwa Uchina, wana aina moja ya msosi unakuwa ni mchanyato wa kuku kaanga na viazi kaanga ndani ya mchuzi mzito wa viungo (Da pan ji), hatari sana hiki kisinia....

Vyakula vya kihindi/kipakistan - majina siyajui lakini miaka ya nyuma nimekula sana haswa nikiwa Hong Kong, vingi ya vyakula vyao vina mahadhi ya kipwani, viungo, michuzi michuzi yenye vikorombwezo haswa...

Vyakula vya Kiindonesia - Huko huko uchina katika kusaka misosi yenye mahadhi ya Kiafrika, nikaangukia kwenye mgahawa wa hawa mabwana, kuna kuku fulani shatashata wa mchuzi wenye nazi nzitoooo...hatari sana!

Vyakula vya kipopo (Naija) - Hawa jamaa nao wana vyakula vya michuzi mingi yenye mafuta na pilipili, lakini wana wali wao mmoja mtamu huo unaitwa 'jollof rice', hii upate iliyotiwa pilipili na pande la kuku...noma sana...
Mtoa mada hajaongelea vyakula vya kawaida, amejisifia uzinifu!
 
Back
Top Bottom