2015 iliwahi kunitokea kwenye msiba wa babu.
Babu yetu alikuwa na wake watatu hivyo kufanya wajukuu tuwe wengi sana kwa haraka haraka si chini ya 60. Sasa ujinga wetu ni tunashirikiana kipindi cha misiba tu.
Pia tuna matabaka ya urafiki, wale ambao wapo fresh kiuchumi ndio marafiki na wale wa kawaida ivo ivo hata kutembeleana
Sasa mimi na dogo langu mmoja hivi(mtoto wa mama mdogo kwa bibi mwingine) tupo kivyetu tu, sio uchumi wala kielimu yaani tunajijua wenyewe na ndio angalau tumeishi kule bush kwa babu hivyo kutufanya tuwe maarufu kuliko wengine huko kwa upande wa wanaume.
Ujinga ukaanzia kwenye kunyonyoa kuku na kusaidia kazi msibani, ndugu zetu wanajifanya wa mjini et hata kunyonyoa kuku hawawezi, wanachofanya ni kutusifia tu mimi na huyo dogo et tunanyonyoa kuku vizuri.
Tukawa tunajiuliza na dogo je kunyonyoa kuku kuna utalamu gani, tukaona hapa ni ujinga, wao ni kufata vitu dukani na gari basi. Tena kuna mgari fulani hivi mbovu ikifika time ya kuni, dogo anambiwa aliendeshe yeye.
Tukagundua kuwa hawa wanatuchukulia poa, tena enzi hizo hata hatuna ajira ila harakati zetu tunakula na kuvaa fresh bila kusumbua mtu na totozi tunahudumia.
Siku tunamaliza msiba ndio yalinikuta mazito wakati wa kikao
Kuna dada yetu mtoto wake alikuwa anasomeshwa na babu na sisita huyu aliishi pale baada ya kufeli life huko Zambia, yaani kifupi alikuwa ni mtu anaehitaji msaada na bila hivyo dogo asingefanya pepa.
Kutokana na matabaka yetu watu wakawa wazito kukunjua nafsi kumchangia dada hata hada dogo amalize shule maana alikua form four na pesa iliyobakia ni 1M tu.
Ili kuweka heshima nikanyosha mkono baada ya kuona ukimya, nikasema hili jambo si la mjadala kwakuwa huyu alikuwa anasomeshwa na babu, na babu kafariki na tumekuja kumzika, hatuwezi kuwa tumemsindikiza kwa aman kama vitu alivyoanzisha vinaishia pabaya na madume yote haya tupo, dada zetu wapo.
Nikatoa laki 2 pale pale, nikasema mimi naanzia, na wengine muendelee.
Wakashtuka hao, basi mchango ukaendelea pale na kunae mwamba huyo akasema hizo pesa mpen dada yeye atamsomesha.
Baadae wakanza kuulizia siku hizi nipo wapi na nafanya nini, mara ooh chuo ulimaliza basi najibu kimwamba fulani.
Ila badae nilijuta sana mana pale pesa yangu ilikuwa 70k tu, zingine zilikuwa za boss wake dogo alimuagiza mchele tunaporudui Dar na hiyo 70 ilikuwa ya nauli ya kurudi Dar. Ilibidi tuombe mchele kwa ndugu na kudandia fuso wakati wa kurudi Dar.
Sent using
Jamii Forums mobile app