2015 iliwahi kunitokea kwenye msiba wa babu.
Babu yetu alikua na wake watatu hivyo kufanya wajukuu tuwe wengi sana kwa haraka haraka si chini ya 60.sasa ujinga wetu ni tunashirikiana kipindi cha misiba tu.
Pia tunamatabaka ya urafiki,wale ambao wapo fresh kiuchumi ndio marafiki,na wale wa kawaida ivo ivo hata kutembeleaba
Sasa mimi na dogo langu mmoja hivi(mtoto wa mana mdogo kwa bibi mwingine) tupo kivyetu tu,sio uchumi wala kielimu yani tunajijua wenyewe na ndio angalau tumeishi kule bush kwa babu hivyo kutufanya tuwe maarufu kuliko wengini huko kwa upande wa wanaume.
Ujinga ukanzia kwenye kunyonyoa kuku na kusaidia kazi msibani,ndugu zetu wanajifanya wa mjini et hata kunyonyoa kuku hawawezi,wanachofanya ni kutusifia tu mimi na hyo dogo et tunanyonyoa kuku vizuri.
Tukawa tunajiuliza na dogo je kunyonyoa kuku kuna utalamu gani,tukaona hapa ni ujinga,wao ni kufata vitu dukani na gari basi.tena kuna mgari fulan hivi mbovu ikifika time ya kuni,dogo anambiwa aliendeshe yeye.
Tukagundua kuwa hawa wanatuchukulia poa,tena enzi hizo hata hatuna ajira ila harakati zetu tunakula na kuvaa fresh bila kusumbua mtu na totozi tunahudumia.
Siku tunamaliza msiba ndio yalinikuta mazito.wakati wa kikao
Kuna dada yetu mtoto wake alikua anasomeshwa na babu,na sisita huyu aliishi pale baada ya kufeli life huko zambia,yani kifupi alikua ni mtu anaehitaji msaada na bila hivyo dogo asingefanya pepa.
Kutokana na matabaka yetu watu wakawa wazito kukunjua nafsi kumchangia dada hata ada dogo amalize shule mana alikua form four na pesa iliyobakia ni 1M tu.
Ili kuweka heshima nikanyosha mkono baada ya kuona ukimya,nikasema hili jambo si la mjadala kwakua huyu alikua anasomeshwa na babu,na babu kafariki na tumekuja kumzika,hatuwezi kuwa tumemsindikiza kwa aman kama vitu alivyoanzisha vinaishia pabaya na madume yote haya tupo,dada zetu wapo.
Nikatoa laki2 pale pale ,nikasema mimi naanzia,na wengine muendelee,
Wakashtuka hao,basi mchango ukaendelea pale na kunae mwamba huyo akasema hizo pesa mpen dada yeye atamsomesha.
Badae wakanza kuulizia siku hizi nipo wapi na nafanya nn,mara ooh chuo ulimaliza basi najibu kimwamba fulani.
Ila badae nilijuta sana mana pale pesa yangu ilikua 70k tu,zingine zilikua za boss wake dogo alimuagiza mchele tunaporudui dar.na hiyo 70 ilikua ya nauli ya kurudi dar.ilibidi tuombe mchele kwa ndugu na kudandia fuso wakati wa kurudi dar
Sent using
Jamii Forums mobile app