Uliwahi kuonesha jeuri ya pesa hata kama huna, ili kulinda heshima?

Uliwahi kuonesha jeuri ya pesa hata kama huna, ili kulinda heshima?

Ukiwa na uwezo wa kusema Hapana, maisha hayatakuwa magumu kamwe.

Sio lazima ujilazimishe uonekane tajiri wakati huna uwezo, utaishia kuaibika mwenyewe rohoni.

Kama kitu sina uwezo nako, naondoka kimya kimya mambo yasiwe mengi.
Mi huwa nina mtindo wa kuuliza bei ya kitu kabla sijakinunua.
Kama bei kubwa naondoka.
Kuna sehemu sitaki hata uliza bei
 
Siku nipo zangu JNIA nimetoka Istanbul, kuna dada nilimuona Airport na Transit Cairo nilimsalimia mara zote mbili ila akanyuti..

Basi tulipotimba Daslam majira ya saa tisa unusu to kumi alfajir, baada ya kuzoazoa mabegi tukafika ukaguzi belt tukaambiwa tuingie room ya TRA mmoja baada ya mwingine.

Tulijikuta tumefika wakati mmoja, yeye kaanza kaingia, baada ya muda anatoka na bill huku analalama hana pesa, ananiangalia kwa huruma.

Nikaingia, nikamsomesha afisa pale, nilishaanda mpango wa how ningeshushaba bei.

Nikatoka kiroho safi kuelekea NMB ya ndani,kufanya malipo namkuta manzi anatia huruma kama anataka kuniongelesha, nikarudi kwa afisa kukabidhi risiti, ile nataka kutoka manzi akaja kuniomba nimsaidie njuruku zimepungua, blah blah za kulalalama.

Nikamuuliza ilikuwaje, kumbe kajimwambafai pale kwa afisa, kataja mabei makubwa makubwa bila ya risiti wakati pochi ya 100$ tunasema hata 10$.

Nikamwambia tatizo hamsalmii watu, nikampa pesa ya kuongezea kama 50$,nikachukua namba nikawekeza..
 
Wakati fulani mwaka juzi nikawa na safari ya kikazi Musoma. Sikuwahi kufika Musoma kabla kwa hiyo sikuwa mwenyeji wa maeneo nilitegemea boda.

Nikashuka stend nikamwambia boda nipeleke lodge nzuri nzuri. Baadae nikaona nisichemke ngoja nimshirikishe mwenyeji wangu. Mwenyeji wangu sikuwa nafahamiana naye wala kuonana. Kwa vile alijua ile kazi ni ya kibosi sana akaamini natakiwa kulala hotel yenye hadhi. Akamwelekeza boda pa kunipeleka.

Kufika daaah, nakuta hotel kali ghorofq kadhaa nje napokelewa na mabendera ya nchi mbalimbali.

Nikamwambia bodaboda mmenileta cha kike. Muhudumu mrembo kabisa akaja kunipokea nikiwa mchavu vumbi na kabegi mgongoni kama nimetoka kuchimba mitaro.

Nikamwambia boda usiondoke lolote linaweza kutokea. Tayari muhudumu akawa amenihukumu kwamba sina uwezo wa kulala pale. Akaniambia lakini kaka hata chumba ni kuanzia elfu 50!

Nikamwambia mimi sijauliza bei nimeuliza chumba. Kufika reception kila mtu anaonyesha wasiwasi huyu mteja kapotea. Basi nikamwambia nataka chumba cha juu.

Akanijibu tuangalie tu vya chini kule juu ni kuanzia elfu 70. Nikaona aaaahhhh japo nilitaka chumba cha 20 ila hapa inabidi niweke heshima tu bila kujali chochote.

Nikachukue chumba cha 70. Nikarudi mapokezi kwenye watu wengi walionitilia mashaka. Nikaanza kulipa bills kwa sauti.

Nikawaambia sikilizeni, ninakaa siku 2 nitalipa 140,000 yote, halafu dada chukua buku 10, mlipe boda buku ya nauli na buku 4 ya kunisubiri. Halafu elfu 5 baki nayo umenipokea vizuri, lakini mwambie boda naomba namba yake.

Ndugu msomaji yote hayo niliyafanya kulinda heshima dhidi ya wajinga wachache ambao walinihukumu kwa mwonekano.

Lakini pia kujitabiria mambo makubwa mbeleni kwamba ipo siku nitakaa meza moja na wakuu, nitakula na wakuu na nitalala lodge moja na wakuu.

Je, ulishawahi kufanya jeuri ya pesa hata kama huna kingi, ili kulinda heshima yako au kujitabiria ukuu?!!
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Daaahhh, nimecheka hatari, nimeisoma huku nikivuta taswira jinsi walivyokuchukulia halafu ukawageuzia kibao
 
subiri kidogo

Nakumbuka kuna mchizi wangu aliambia kuna demu kamtongoza halafu siku hiyo amempa mwaliko wa Birthday party viwanja flani town so mchizi wangu aliomba scot yangu.

kilichotokea niliondoka na huyo demu wake baada birthday kuisha na urafiki ukaisha hadi leo

ilikuwa hivi baada ya kufika pale mimi nilikuwa pembeni pembeni tu kwasababu sina ninaemjua ukiacha nilivyotambulishwa kwa shem mwenye party yake tu basi so, mchizi wangu akawa yupo bize na demu wake tu

Ghafla kukawa kuna vikao vya dharula huku sura za waalikwa Azi-relate na tukio husika kumbe bwana yule demu mwenye ile party kuna rafiki yake alimpa pesa kwa ajili ya lile eneo la shughuli kakimbia na hela na party imeanza mwenye ukumbi anasema siwajuhi ondokeni kabla sijaita polisi😅😅😅😅 wapuuzi wakumbwa

ghafla tukajikuta tupo watatu mimi na jamaa wangu na shem sasa ikapelekea niulize swali maana yule jamaa wangu ni ROFAA tu watu wa vijiweni vijiweni wale ... NI KIASI GANI CHA PESA YA UKUMBI KINAHITAJIKA HAPA ? shemu akajibu ni laki na 80 tu na hapa mimi nina elfu 50 tu.

Mwanaume nikaona mbona ni hela chumvi tu nikamwabia JAMES [ mwanangu ] mimi nalipia unasemaje ? daah mwanangu we lipia tutajua cha kufanya. nikatoa wallet nikatoa mia hamsini cash nikampa james huku demu Anaona Si-unajua sisi watoto wa mjini atutembei kama MAITI.... kimoyomoyo hapo nasema..🥴🥶🥶

itaendelea

kiukweli yule demu alikuwa ni mtamu sana sijapata kuona alikuwa analia vilio vyote halafu ni mdogo mdogo nilijilia vyangu usiku ule siwezi kusahau
Alaa alaa!
 
Yule demu aliponipa mzigo tako tatu wadhungu hao. Nikasingizia sijala ngoja nile nimpe show za WWE John cena you can't see mee. Nikala chips ndizi mishikaki. Nikampq romance kupima oil naona huyu kashaiva nikachomeka kupiga take tatu wajapan hao. Nikaona sasa hapa mbona kazi sana. Nikaona ngoja nizuge zuge kuangalia vipindi vya wanyama kwenye TV. .

Alipoamka nikaona nitumie nafasi hii kumuonyesha show ya kibabe. Kupiga tako nyingine tani aisee wazee hawajakosea siku ya kufa nyani kweli miti yote huteleza. Kupiga tako nikajikaza yani kufika tako ya tano tu tena nimejikaza nikawa na uma na meno wahindi haoo. Aisee what an embarrassing day.

Kurudi kwenye mada, ili kurudisha heshima nikamuliza demu hivi unaishi wapi? Akajibu magomeni nimepanga chumba elfu 70. Nikaanza kujiongelesha hapa inabidi upange sinza chumba laki na hamsini. Nataka nikukipie kodi ya miezi kumi. Kwanza kabla sijasahau shika hii laki. Ukifika nyumbani nakutumia hela nyingine ununue vitu vya nyumbani hiyo laki ni nauli tu. Hata samsung unayotumia sio simu ya maana nakununulia iphone.

Alipoondoka na laki yangu nikatupa line nikasajili line nyingine kwa mpita njia. Huyu dada tulikutana kwenye mwendokasi. Hata mwendokasi sipandi tena nawasiwasi naweza kukutana nae huko [emoji51][emoji51][emoji51]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Daaahhh
 
Siku moja majuzi hapa umeme umekatika salasala nzima kuangalia mpira vibanda umiza haiwezekani ikabidi nijivute sehemu moja hivi nikakadilia pale soda moja itakua buku au buku jero kufika nikaagiza sprite nikampa muhudumu noti ya elfu 5 nashangaa narudishiwa chenchi elfu 2 sasa jirani yangu aliagiza kinywaji nae pia ile chenji aliyorudishiwa akashtuka akauliza bei akaambiwa soda elfu 3 akaomba arudishiwe hela yake akasepa mzee mzima kulinda heshima ikabidi nitulizane kama vile kwangu sio ishu ila iliniuma kinoma
Dah... Mkuu salasala chimbo gani hilo soda aftatu Aiseee... mimi huku ndo home.. nipe code nikaweke heshima!! Au ulishuka chini kule mitaa ya lamada?
 
Wakati fulani mwaka juzi nikawa na safari ya kikazi Musoma. Sikuwahi kufika Musoma kabla kwa hiyo sikuwa mwenyeji wa maeneo nilitegemea boda.

Nikashuka stend nikamwambia boda nipeleke lodge nzuri nzuri. Baadae nikaona nisichemke ngoja nimshirikishe mwenyeji wangu. Mwenyeji wangu sikuwa nafahamiana naye wala kuonana. Kwa vile alijua ile kazi ni ya kibosi sana akaamini natakiwa kulala hotel yenye hadhi. Akamwelekeza boda pa kunipeleka.

Kufika daaah, nakuta hotel kali ghorofq kadhaa nje napokelewa na mabendera ya nchi mbalimbali.

Nikamwambia bodaboda mmenileta cha kike. Muhudumu mrembo kabisa akaja kunipokea nikiwa mchavu vumbi na kabegi mgongoni kama nimetoka kuchimba mitaro.

Nikamwambia boda usiondoke lolote linaweza kutokea. Tayari muhudumu akawa amenihukumu kwamba sina uwezo wa kulala pale. Akaniambia lakini kaka hata chumba ni kuanzia elfu 50!

Nikamwambia mimi sijauliza bei nimeuliza chumba. Kufika reception kila mtu anaonyesha wasiwasi huyu mteja kapotea. Basi nikamwambia nataka chumba cha juu.

Akanijibu tuangalie tu vya chini kule juu ni kuanzia elfu 70. Nikaona aaaahhhh japo nilitaka chumba cha 20 ila hapa inabidi niweke heshima tu bila kujali chochote.

Nikachukue chumba cha 70. Nikarudi mapokezi kwenye watu wengi walionitilia mashaka. Nikaanza kulipa bills kwa sauti.

Nikawaambia sikilizeni, ninakaa siku 2 nitalipa 140,000 yote, halafu dada chukua buku 10, mlipe boda buku ya nauli na buku 4 ya kunisubiri. Halafu elfu 5 baki nayo umenipokea vizuri, lakini mwambie boda naomba namba yake.

Ndugu msomaji yote hayo niliyafanya kulinda heshima dhidi ya wajinga wachache ambao walinihukumu kwa mwonekano.

Lakini pia kujitabiria mambo makubwa mbeleni kwamba ipo siku nitakaa meza moja na wakuu, nitakula na wakuu na nitalala lodge moja na wakuu.

Je, ulishawahi kufanya jeuri ya pesa hata kama huna kingi, ili kulinda heshima yako au kujitabiria ukuu?!!
Ujinga mtupu.
 
Mimi ndo nipo nasumbua ndugu hapa wanikopeshe walau alfu kumi.

Hii ni baada ya kulipia bili za watu wote niliowakuta mgahawani jana
Kwa tsh 86500.

Ni stori ndefu kidogo lakini tu kiufupi dharau zinaumiza sana.
Teh teh...
 
Hii inakubalika kabisa, Mimi nilikua Kasulu, nikawa na mazoea kwenda Bar kuangalia mpira, Kila nikienda pale naagiza maji, basi wahudumu wakawa wananipotezea. Hawana mzuka wa kunihudumia.

Basi, nikarudi Tena nakumbuka ilikua game ya Simba, wakagoma kunipa hata Kiti, akanihudumia Dada mmoja hakua na makuu, kwa hasira nikaagiza Castle Light 20. Nikamwambia Kaa hapa, hizi ni za kwako na yule mwenzio aliyenihudumia Jana.
Hahahahaha 🤪 sometimes you got to fight to prove you're a Man (Kenny G)
Castle lite 20 ni Tsh elfu 30.
 
Mimi ilikuwa sio kuleta heshima ila ilikuwa sifa.iko hivi nilienda dodoma kwenye harusi ya sista nilikaa meza moja na pisi kali 2 ukafika muda wa kuchangia bibi harusi kulikuwa na phase mbili,phase ya kwanza ilikuwa kikapu kinapita kwenye kila meza yoyote anaweka alichonacho'muda ule nilikuwa nipo tungi balaa kutaka kuonyesha sifa mfukoni nilikuwa na laki 8 nikawa naweka narusha rusha elfu 10 kwenye kapu mpaka laki 8 yote ikaisha.
Baadae wale wadada wakaniambia weee kaka pesa zote umetoa wapi mbona umechangia hela nyingi hivyo!! Nikawaambia kawaida kisha nikawapotezea.
Ikaja phase 2 kwenda kumtunza bibi harusi pale mbele ili kuonesha sifa nikaenda ATM nikatoa mil 1.5 pisi kali moja ikanishauri sana nisiende kuchangia tena pesa nilizotoa awali zinatosha.
Baada ya harusi kuisha asubuhi nikajikuta nipo room yenye muonekano kama hostel kumbe yule sista nilivyozima alinikokota mpaka chuoni kwao alikuwa ni mwanafunzi wa udaktari md5 akanikabidhi pesa yangu 1.5mil alizitunza coz nilikuwa tungi sana..kifupi huyo dada ndio mke wangu hivi sasa..sifa zilinisaidia kupata mke bora aliyekuwa yupo sealed
Very interesting
 
Dah mi nakumbuka kuna mwanangu alinialika kigamboni tupate bia mbili tatu nikatimba asee apo ni camp joint,nikakuta kimewaka yuko na jamaa zake kama nane wanamalizia malizia bia zao namimi nkapiga kama mbili hivi nilizozikuta tukahamia the Giant asee ile siku nikijikuta natumia laki tatu ila kuendana nao make jamaa yangu alikua ananitambulisha kama mtu mkubwa fulani hivi bas namimi sikuwaangusha ila nilipata homa kwa hasara ile.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
2016 nikiwa mtumishi wa taasisi fulani hivi,ilitokea tu nikawa sina smartphone,sasa kijiweni ninaposhinda nikawa nagongea simu,kuingia jf,twitter insta nk,mpaka kubeti.
Siku moja nadhani mwenye simu alifikwa hapa(waswahili wanasema)akaropoka[emoji28][emoji28].
Aisee wewe ni mtumishi smart imekushindaje bana??daily unagongea simu yangu inachemka[emoji28],aisee wengine njia ya kupokea taarifa mbaya za ghafla huwa tuna tabasamu.
Kinyoonge asishtuke kama nimekwazika,nikamwambia tulia namalizia ishu moja,nakupa.
Kesho yake ilibidi nivunje kibubu kwa hasira kwa mara ya kwanza nikaenda kujitwisha iphone ya kwanza kutoka shop(iphone 6plus) ikiwa bado inafuka moshi kipindi hicho 1.6mln.asubuhi nafika pale anashangaa nina simu yenye bei mara 5 ya kwake,akatoa macho tu na kuanza kujaribisha camera.

Binaadam wanatia hasira lakini tunawashukuru maana wamefanya wakati mwingine kwa kauli zao,tuondoke kwenye comfort zone zinazotulemaza.
 
Back
Top Bottom