Uliwahi kuonesha jeuri ya pesa hata kama huna, ili kulinda heshima?

Hiyo inaitwa kuwa na "siku mbaya kazini"
 
Kutoka kunyonyoa kuku mpaka sponsor,balaa
 
Mimi miaka kama 10 iliyopita nilitumwa dawa za 250,000/= za famasi, duka wamefunga nikawaambia home dawa hadi kesho wakasema hela nikae nayo hadi kesho, jioni saa moja nimeenda Bar ya kibosi kuangalia mpira Wa arsenal,Ghafla nakuta warembo wawili wabishi watoto wa mjini na jezi zao za the Gunners,tunafahamiana nikasema usinitanie,zikaanza gambe pombe na Ng'ombe,kabla dakika 90 hela imeisha..hah hata hela ya bodaboda sina,,nikatembea ki Bob marley..nikazima simu siku mbili ili home wasinisumbue...tangu hapo sijwahi kutumwa dawa...
 
Tutunzie heshima wana JF mkuu
 
Umenikumbusha leo wife amenipa stori ya kijijini kwao kuna ndugu anaumwa kalazwa hospitali. Anko wake akatumwa akauze ng'ombe hela ya matibabu ipatikane. Kauza laki 5 halafu akazima simu siku 3. Wakamsaka wanakuja kumkuta na laki 1 tu nne zote kapiga pombe na kuhonga
 
Haha huyo anko mimi,,me wake wapo Town ila wanaduka la dawa kijijini
 
Hii ilikuwa komesha
 
Dah!..uliokota embe dodo chini ya mpera.... hongera
 
Siku moja majuzi hapa umeme umekatika salasala nzima kuangalia mpira vibanda umiza haiwezekani ikabidi nijivute sehemu moja hivi nikakadilia pale soda moja itakua buku au buku jero kufika nikaagiza sprite nikampa muhudumu noti ya elfu 5 nashangaa narudishiwa chenchi elfu 2 sasa jirani yangu aliagiza kinywaji nae pia ile chenji aliyorudishiwa akashtuka akauliza bei akaambiwa soda elfu 3 akaomba arudishiwe hela yake akasepa mzee mzima kulinda heshima ikabidi nitulizane kama vile kwangu sio ishu ila iliniuma kinoma
 

Hii huwa ipo sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…