Niko na toto la Nai tunapigiana simu tu tukaahidiana tu meet easter holiday, zile skukuu zinaongozana siku kama nne hvi, sasa nikakata zangu ticket presisheni ya go pekeake ilikua kama laki saba hivi, kurudi nitarudi zangu na tahmeed sio kesi,
Basi siku ya safari imefika naenda zangu airport kwa mbwembwe huku na ma whasap video kalling na mchuchu, naye alikua ndio yuko saluni anatengeneza nywele a bling bling aje kunipokea Jomo kenyata ashawapanga na mabeshte zake,
ile kufika airport tu mda wa check inn ulishapita na milango ishafungwa, mzee baba full kupanik omba sana wakaniambia ni amend ticket nipande ndege nyingine, nikamweleza mchuchu akaniambia nisimuongeleshe ye anachojua mi nafika leo yaani alishajikoki, Mzee nikatoka kwa nje pale mpaka kaunta ya presesheni na mkuta mdada, akaangalia akaniambia ndege ipo ya saa moja ila nafasi ilikuepo ni bizness klass!
Dooh nikacheki na mchumchu akaniambia yaani nisimuongeleshe kitu chochote na atashika simu tu nikiwa kwa ndege,
Mzee baba nikamuuliza niongeze ngapi dada mhudumu akajibu laki saba Halahaulaaaa!
Kulinda heshima nikaenda palekuna magari magari ya atm nikatoa akiba yangu nilioweka inilinde nikirudi nikavurua nikakata, ikabidi niisubirie palepale imagin toka saa tisa hadi saa kumi nambili!