Uliwahi kupata mikasa gani kwa kuishi kwa ndugu?

Mme wa shangazi naye vipi akisema mnaniletea mizigo! Labda sio wajita ninao wajua mimi walivyo wabinafsi atamfukuza mchana kweupe
 
Kwenye shida ndugu zako Mara nyingi hukupenda na kukuomba msaada Tena watakuona Kama mfalme au malkia wao. [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Siku ukiishiwa au kupata shida unabaki na mkeo uliyekuwa unampuuza na kuwaona ndugu ndiyo namba moja mke namba 3.
 
Sijawahi ishi kwa mtu toka nimezaliwa. Ila tumeishi na ndugu wa Baba, Mama na Jamaa.

Nilochojifunza

Kila mtu aishi kwao
Kuna makabila wanapenda kusukumia watu watoto wao sijui wapoje, bora mtu aliyekuwa anakuja kutafuta maisha si kupeleka mtota akasomee hapo afadhali ukae na wanao usaidiwe kama ni ada basi.
 
Kuna makabila wanapenda kusukumia watu watoto wao sijui wapoje, bora mtu aliyekuwa anakuja kutafuta maisha si kupeleka mtota akasomee hapo afadhali ukae na wanao usaidiwe kama ni ada basi.
Kila mtu na aishi kwao.
Watu hawana shukurani, ataishi nawe akiondoka ataenda sema alikuwa anateswa
 

Sitoleta mikasa hapa maana ni mingi mnooo
Ila nashauri kitu kimoja NDUGU TUWASAIDIE PALE TUNAPOWEZA NA MISAADA IWAFIKIE KULEKULE WALIKO!
Sio uwalete kwako, hapanaaaa
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] hawa ndio wale wenzangu na mimi mafridge wameyakuta ukubwani kwa hiyo mle ndani ya fridge anapaona kama peponi hivi
Tulikuwa tuna fungiwa fridge na funguo! Tv mnatizamia dirishani enzi za mchezo wa Tausi loh Mama alikuwa mchoyo yule j2 Ndiyo mtakula milo 3 akiwepo Mshua na ni Dr nawaza hao wagonjwa huko mhhh ila aliachika[emoji3]
 
Nilifika kwa ndugu yangu na katika kukaa pale ikatokea Hela shilingi Elfu 20 imepotea.

Mama mwenye nyumba akaanza maneno, Tabia hii ya Wizi haikuwepo kabisa hapa nyumbani sijui nani ameiletea [emoji848][emoji849]

Na ndio nilikuwa na siku moja tu, tangu kufika hapo.
 
Hahahhahah mbwa hawanaga mazoea,wangekupalura
 
Siyo tu kuishi kwa ndugu, hata kusafiri na kufikia kwa ndugu, jamaa ama rafiki ni shughuli pevu.

Kama huna sababu kuishi/kufikia kwa ndugu ama jamaa EPUKA KABISA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…