Uliwahi kutamkiwa neno gani baya na Mwalimu wako?

Baadhi ya walimu kuanzia Shule ya Awali na Msingi,Sekondari na hadi Chuo wamekuwa na tabia ya kutamkia watoto maneno makali na yenye kukatisha tamaa.

Mojawapo ya Maneno hayo ni kama โ€œHutaweza kufanikiwa hata siku mojaโ€.

Wakati mwingine maneno hayo huwafanya wanafunzi kujiona wanyonge na kukata tamaa katika masomo yao na kusababisha baadhi yao kushindwa kutimiza ndoto zao.

Lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida wanafunzi wengi wakimaliza masomo baadhi yao hufanikiwa na kuajiriwa katika Taasisi, idara, Mashirika na sehemu nyingine kama hizo.

Walimu hufika kuhitaji msaada na kuwakuta wanafunzi wao waliowatamkia maneno makali wakitoa huduma katika sehemu hizo.

Wakati mwingine husaidiwa lakini pia wakati mwingine hukutana na Vikwazo kutokana na yale waliyoyatenda nyuma.

Walimu tujifunze tuache kuwa wakatili na kutoa kauli kali kwa Mtoto ili kesho yenu iwe Bora zaidi.
Mimi niliwahi kuambiwa na mwalimu wa kiswahili....... "ww ni ushuzi wa bata"

Mpaka leo hili neno limenikaa
 
Ndo maana wamedumaa kimaisha sababu ya midomo yao, mtoto wa miaka 11-15 unampaje adhabu ya kuita mvua nyakati za kiangazi! Au kuchimba kisiki akishindwa unaanza kujifanya nabii eti jambazi wewe, umeshindikana, acha waendelee kudoda
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mengi sana ila kwa uchache.

Mwalimu wa fizikia kidato cha 2-4
Baada ya matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha pili aliniponda mbele ya walimu wenzake kuwa.
"amebahatisha tu huyo hana akili ya kupata distinction"

Ashukuriwe Mungu aliye juu, miaka miwili iliyopita nimefanikiwa kumaliza shahada yangu bila ya supplimentary ya kozi yoyote ile enzi za ujana wangu, sa hivi nipo zangu mtaani naokota chupa za maji!
 
Wakati nipo f4 madam wa civics aliniambia
โ€œHutafanikiwa kumaliza f4 na kufauluโ€

Tulikua tunasoma na mtoto wake wa kiume na alikua mpenzi wangu na alifahamu baada ya kumaliza f4๐Ÿ˜„

Matokeo yalitoka nikafaulu mtoto wake alifeli, kasoma kwa kuunga unga lakini hajafika chuo kikuu, na nipo na mwanae mpaka leo. Mama yule wa kichagga ananionea aibu tu.๐Ÿ˜‚
 
๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜… Hongereni kwa kuwa pamoja hadi leo.
 
Baadhi ya walimu kuanzia Shule ya Awali na Msingi,Sekondari na hadi Chuo wamekuwa na tabia ya kutamkia watoto maneno makali na yenye kukatisha tamaa.

Mojawapo ya Maneno hayo ni kama โ€œHutaweza kufanikiwa hata siku mojaโ€.

Wakati mwingine maneno hayo huwafanya wanafunzi kujiona wanyonge na kukata tamaa katika masomo yao na kusababisha baadhi yao kushindwa kutimiza ndoto zao.

Lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida wanafunzi wengi wakimaliza masomo baadhi yao hufanikiwa na kuajiriwa katika Taasisi, idara, Mashirika na sehemu nyingine kama hizo.

Walimu hufika kuhitaji msaada na kuwakuta wanafunzi wao waliowatamkia maneno makali wakitoa huduma katika sehemu hizo.

Wakati mwingine husaidiwa lakini pia wakati mwingine hukutana na Vikwazo kutokana na yale waliyoyatenda nyuma.

Walimu tujifunze tuache kuwa wakatili na kutoa kauli kali kwa Mtoto ili kesho yenu iwe Bora zaidi.
Babu wa siasa, Mr mbago alishawah kuniambia "hio pesa wazazi wako wanalipia ada ni Bora wakanunue mkaa ukapikia nyumbani"
 
Back
Top Bottom