Uliwahi kutamkiwa neno gani baya na Mwalimu wako?

Mimi niliwahi kuambiwa na mwalimu wa kiswahili....... "ww ni ushuzi wa bata"

Mpaka leo hili neno limenikaa
 
Ndo maana wamedumaa kimaisha sababu ya midomo yao, mtoto wa miaka 11-15 unampaje adhabu ya kuita mvua nyakati za kiangazi! Au kuchimba kisiki akishindwa unaanza kujifanya nabii eti jambazi wewe, umeshindikana, acha waendelee kudoda
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mengi sana ila kwa uchache.

Mwalimu wa fizikia kidato cha 2-4
Baada ya matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha pili aliniponda mbele ya walimu wenzake kuwa.
"amebahatisha tu huyo hana akili ya kupata distinction"

Ashukuriwe Mungu aliye juu, miaka miwili iliyopita nimefanikiwa kumaliza shahada yangu bila ya supplimentary ya kozi yoyote ile enzi za ujana wangu, sa hivi nipo zangu mtaani naokota chupa za maji!
 
Wakati nipo f4 madam wa civics aliniambia
β€œHutafanikiwa kumaliza f4 na kufaulu”

Tulikua tunasoma na mtoto wake wa kiume na alikua mpenzi wangu na alifahamu baada ya kumaliza f4πŸ˜„

Matokeo yalitoka nikafaulu mtoto wake alifeli, kasoma kwa kuunga unga lakini hajafika chuo kikuu, na nipo na mwanae mpaka leo. Mama yule wa kichagga ananionea aibu tu.πŸ˜‚
 
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… Hongereni kwa kuwa pamoja hadi leo.
 
Babu wa siasa, Mr mbago alishawah kuniambia "hio pesa wazazi wako wanalipia ada ni Bora wakanunue mkaa ukapikia nyumbani"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…