Tukio La kwanza Nilipika wali ukaiva kabisa sasa wakati nahesabu dakika niutoe jikoni nikakumbuka sijaweka chumvi yaani hata punje moja....Maza alisafiri nilibaki mzee.nikaenda kumuita shangazi akauweka sawa baada ya hapo nilipigwa BAN na mzee kupika chakula.
Tukio la pili Mimi na dada yangu tulipika ugali kujaribu kama umeivaa tulikuwa tunatupia ugali ukutani ukinasa hujaiva Sasa kila tukitupa unanasa(yani hujaiva ),sister akaniambia kamwangalie Kaka kama anakuja(ili tupike mwengine) nilivyoenda kumuangalia nikamkuta anakuja ,nakaenda kumpa taarifa sister akesema tukajifiche chini ya uvungu wa kitanda.
bro alivyorudi ana njaa katuka jikoni kumepikwa kufunua msosi hakuna na kumbe aliniona wakati na mchungulia alivyo ingia ndani akatuona tumejificha chini ya uvungu sister aliniweka mbele(chambo) bro akaniambia toka chini huko na sister akatoka katuonyesha jikoni na ukutani mmefanya Nini hapa ,tujitetea kwamba tumepika Sasa tukawa tunajaribu kama umeivaa kauliza na ugali uko wapi (tuliutupa ) sister akachezea kofi mm nimejikunyata pembeni bro alimwambia Yani na ukbwa wako huu hujui kupika unaharibu unga si ungeenda kumuomba shangazi akusaidie......
Nilipigwa fimbo tatu yeye ndio alichezea nyingi zaidi
Tukio LA tatu nilivyokuwa chuo ,geto na washkaji nakumbuka ilikuwa mwaka mpya tukasema oya tusipite hivi hivi tukanunua nyama kilo mbili mchele kilo 4 Mimi ndio stelingi jikoni...loooh mboga iliiva Lkn wali he he he ulikuwa hujaiva ,umeungua na umetoka boko boko yaani wahuni walikuwa wananung'unika huku wanakula yaani mwanangu utanulisha wali na mchele..uzuri sisi geto tuliwekeana Sheria kwamba hakuna aliyemuoa mwezie humu ukiona chakula kibaya kale hotelini so kilo nne zote ziliisha