Uliwahi kuzingua kwenye mapishi, iwe ni mara ya kwanza unapika ama ukiwa mzoefu tayari?

Hahahhaa...!
Ukaweka maji mpaka juu..?? Hebu niacheni jamani..!!
 
Daaah umenikumbusha mbaliii kuna siku nilikua home mwenyewe nikaamua nijipikie ugali maana nilikua na ubao nikasema nipike bonge la ugali basi nikaingia zangu jikoni nikapika ugali ulivyokua mtepe sasa duuuh nikajisemea kimoyo moyo huu nitaugonga mpaka uishe ile nimetenga tu nasikia mother anagonga hodi kufungua namkuta kaja na rafiki zake daaaaaah mpaka kijasho kikanitoka nao wakajisemea wamefikia pazuri[emoji849] basi nikawanawisha vizuri wakaja mezani kula ile wanamega tu [emoji2363]nikaskia wanaguna [emoji2303]hata hawakuendelea walipiga tonge mbili mbili wakajisemea wameshiba huku mimi nikiwa bize nashusha matonge ya adabu[emoji23]
 
Nimecheka wakatukana na kuumaliza ugali
 
Mimi ugali mpaka leo inatokea bahati utoke mzuri kama hujatoka na mabuje basi hauivi
Mkuu ukitaka kuwa mpishi mzuri wa ugali bila kuharibu na kuweka yale mabuje, kuna mbinu ipo hivi:
Ukibandika maji jikoni weka unga kidogo (nusu kikombe au kikombe cha chai kutegemeana na size ya ugali unaopika) kisha koroga huo uji ukiwa jikoni mpaka uanze kutokota, hapo utajikoroga wenyewe wakati wa kutokota. Uache kama dakika 7 hadi kumi ili uive vizuri. Ukishaiva huo uji chukua unga anza kusonga, usiweke unga mwingi sana, anza na kiasi kidogo ili kucontrol ugumu wa ugali, kwa sababu si kila mtu anapenda ugali mgumu sana, au mlaini sana. Kadiria unga huku unasonga. Then unakuwa unasonga huku unauacha kidogo kwa sekunde chache ili uive pande zote. Utasikia tu harufu nzuri ya ugali, hapo umeiva.
Happy Eating Mkuu.
 
Hahahaa..
Nisivyopenda aibu walaqhi'..!
Ile hodi ya kwanza, ningeutupia huo ugali huko chini ya meza jamani..!
 
Dahh nimefurahi sana leo mm sijawahi sumbuliwa pika chakula kikatoka Vby Napika kalbia vyakula vyt pendwa Ugali wali pilau Mtori na vngn vng japo wa kiume Nimejuwa kupika hivyo vyt kwa sbb nimelelewa na watu tofaut so ukiwa kwao lazm upike siunajuwa 50'/50 sio pow kipindi iko
 
Hongera sana..! Wewe umebahatika.! Wengine tumepambana mpaka akili zikatukaa.!!
 
Nimezingua sana kupika keki hakika mwanzo ni mgumu , ni vile kutumia mikaa ndo maana inasumbua , siku hizi napika tu endapo nitakuta oven otherwise bora nikununue kwenye bakery.
 
Nimezingua sana kupika keki hakika mwanzo ni mgumu , ni vile kutumia mikaa ndo maana inasumbua , siku hizi napika tu endapo nitakuta oven otherwise bora nikununue kwenye bakery.
Kama ulizingua ukiwa mwenyewe si mbaya sana.. Mbaya ni ile hukuwa mbele za watu..! Watu waanze kata keki tuleee.! Wanakata wanakuta vitu vimeshikana..
 
Kama ulizingua ukiwa mwenyewe si mbaya sana.. Mbaya ni ile hukuwa mbele za watu..! Watu waanze kata keki tuleee.! Wanakata wanakuta vitu vimeshikana..
Hahaha, mimi imenikuta mbele ya ndugu zangu sema ni washikaji tu .... Haha kama ni sherehe bora ununue kutoka Bakery ..

Tena wanakuta na imeungua juu mara upande huu haujaiva , dah tutafute hela tu .
 
Hahaha, mimi imenikuta mbele ya ndugu zangu sema ni washikaji tu .... Haha kama ni sherehe bora ununue kutoka Bakery ..

Tena wanakuta na imeungua juu mara upande huu haujaiva , dah tutafute hela tu .
Hahahhaa..!
Jamani nyieeeh'...!
Hivi honestly utaambia nini watu.! Hapo ndiyo habari zimetapakaa mjini mpishi wa cake anafahamika na ulitia na mbwembwe, unajikuta umekuwa mdogo aibu inakuzidi uzito.!
 
Hahahhaa..!
Jamani nyieeeh'...!
Hivi honestly utaambia nini watu.! Hapo ndiyo habari zimetapakaa mjini mpishi wa cake anafahamika na ulitia na mbwembwe, unajikuta umekuwa mdogo aibu inakuzidi uzito.!

Mimi nakimbia aiseeh ... Hiyo aibu ni noma
mambo mengine haya tuwaachie wapishi wa keki wanaoweza ..
mimi napika keki za kula tu na familia , kujifanya mpishi mashuhuri ndo nn [emoji1787][emoji1787].
 
Mimi nakimbia aiseeh ... Hiyo aibu ni noma
mambo mengine haya tuwaachie wapishi wa keki wanaoweza ..
mimi napika keki za kula tu na familia , kujifanya mpishi mashuhuri ndo nn [emoji1787][emoji1787].
Hahaha..!
Kajisemeaga zake Madame B bora ategue sufuria limwagikie huko kuliko hiyo fedheha.! Sasa sijui nawe ungeigusa bahati mbaya iporomokee.!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…