Mkuu zaganza ..nina tatizo la kuwashwa mwili ..hasa wakati wa jua, mwili unakuwa kama una sisimka alafu na hali flani kama ya kuchoma choma hutokea.
Au nikinywa chai au kitu chochote cha moto au mwili ukipata joto tu mf nikiwa natembea haraka na mwili kupata joto basi hiyo hali hunipata.
Kama ni allergy mkuu plizi nisaidie namna ya kuisha.
Moja ya matatizo ya kiafya yanayowasumbua watu wengi duniani na kuwanyima raha ya maisha, ni tatizo la mwili kuwasha baada ya kuoga.
Muwasho baada ya kuoga unaweza kujitokeza mwili mzima au unaweza kuhusisha baadhi ya sehemu za mwili. Pia, hali hii inaweza kuendelea kwa muda wa dakika chache au inaweza kuchukua muda mrefu na kwa baadhi ya watu hili linaweza kuwa tatizo sugu.
Ingawa tatizo hili la kiafya ni kama matatizo mengine, lakini baadhi ya watu kwa kukosa taarifa sahihi hulihusisha na imani potofu. Ukweli wa mambo ni kwamba kuna sababu nyingi zinazochochea kutokea kwa tatizo hili na baadhi hazina madhara makubwa lakini sababu zingine zinaweza kuwa hatarishi kwa maisha.
Miongoni mwa sababu za kutokea kwa muwasho wa mwili baada ya kuoga ni za kimazingira na sababu zingine zinahusiana na hitilafu za urithi wa vinasaba vya kijenetiki katika mfumo wa kinga ya mwili wa mhusika.
Wakati mwingine tatizo hili linaweza kuwa dalili muhimu inayoonyesha baadhi ya magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza kama vile matatizo ya figo, ini, tezishingo, matatizo ya mfumo wa damu, kisukari, saratani ya mitoki na msongo wa mawazo.
Baadhi ya tafiti zinabainisha kuwa sababu za kimazingira ni pamoja na uchafuzi wa mazingira ya hewa kwa kemikali zenye sumu zinazopatikana katika moshi wa tumbaku na mifuko ya plastiki, dawa za kufanyia usafi majumbani, dawa za kuuwa wadudu waharibifu, mabaki ya wadudu, mavumbi ya ndani ya nyumba yanayobeba vimelea vya magonjwa pamoja na uchafuzi wa hewa kwa moshi wa magari na ule unaozalishwa na viwanda katika maeneo ya mijini.
Vitu hivi huufanya mwili kuathirika na kutengeneza mazingira ya ndani ambayo yanachochea kutokea kwa muwasho, pindi mwili unapopata msisimko, hali ambayo hujulikana kama mzio.
MUHIMU: Kapime vipimo hivyo kisha tuwasiliane