Uliza swali lolote kuhusu wanyamapori wetu na tabia zao utajibiwa

Uliza swali lolote kuhusu wanyamapori wetu na tabia zao utajibiwa

Chui unaweza kulala naye juu ya mti usijue halafu ye akakuona akakuacha tu mpaka kuna kucha unafungua macho anakupita miguuni anaelekea kwenye mishe zake.

Kuna wanyama nuksi yani hata kama limeshiba likikukuta litapata tamaa kutaka kukuua likufanye akiba ya msosi wa kesho
Wew ndio Yule jamaa uliekua unatuadisia move shulen[emoji1787][emoji1787]
 
Nataka kujua simba wa familia moja(pride) wanawezaje kujitofautisha na familia nyingine wakati wanafanana kila kitu? Hili nimeuliza kwa sababu ikitokea familia moja ikaingia kwenye eneo(territory) ya familia nyingine hutokea ugomvi mkubwa sana hasa majike.
 
Kuna mnyama anaitwa Fungo (kama sijakosea)... ni kweli kwamba anajisadia sehemu moja tu..!!? Kwamba kama sehemu ya kujisaidia ipo Mbeya, akibanwa na haja akiwa Mwanza anatoka mbio hadi Mbeya kwenda kujisaidia?
Aisee
 
TWIGA.
ndio mnyama mrefu kuliko wote duniani.
ana urefu w futi13.urefu wa watu wazima 2.
ni mnyama aliye na mwendo wa kipekee yaani AMBLING movement.akitembea au kukimbia utahisi ni muvi ya kimgandisho.twiga maisha milele halali analala siku amefariki tuu.anabeba mimba kwa miez15 mtoto anazaliw na kg100.teke lake ni uzito wa kg200 one blow can kill a lion instantly.ingawa ni mrefu lakin ajabu uti wake wa mgongo una pingiri(vertrbrae)idadi sawa na za binadamu.twiga anajulikana kama mama mbaya kuwahi kutokea sababu anasau kama ana mtoto sababu ya [emoji3]urefu(bad mother).ulimi wao ni mrefu hadi fut2 na una gundi sababu ya kula majani palipo na miba mingi(acacia).ni katika wanyama waliwahi kukutwa wakila nyama sababu ya kuongeza madini flani mwilini haswa calcium.
nimeweka machache kama una maswali uliza
Sasa wakiwasahau watoto wao inakuwaje wakitaka kunyonya au watoto wanajiongeza wenyewe?
 
Nataka kujua simba wa familia moja(pride) wanawezaje kujitofautisha na familia nyingine wakati wanafanana kila kitu? Hili nimeuliza kwa sababu ikitokea familia moja ikaingia kwenye eneo(territory) ya familia nyingine hutokea ugomvi mkubwa sana hasa majike.
wanajuana kwa harufu.hata wakitenganishwa wakiwa watoto wakikutana ukubwana hutambuana kwa harufu
 
....black panther nae ana nini cha kustaajabisha??.....
black panther ni jaguar wametofautiana rangi tuu.na hawa hupatikana nchi zisizo africa.hivyo ni jamii ya chui kabisa isipokuwa jaguar ana mwili mkubwa kidogo.niongeze kwamba kuna mambo hutokea kwa mnyama akawa mweusi au mweupe(albinism)kwa mfano twiga wako albino na wapo ambao rangi nyeusi inazidi kuliko rangi ingine hili suala huchangiwa(melanin)unakuta pigments ya rangi fulani inazid hivyo mnyama anatoka na melanin nyingi.
 
Kwanin mbuzi anamkia mfup?
ni mazingira tuu ya kila mnyama alivyo.kiboko ana mkia mfupi lakini upo kwa ajili ya kusambaza kinyesi kinapotoka yaani mkia unamsaidia kukata gogo lisiwe refu.ila kwa mbuzi sijui wala kondoo kwann mafuta yawepo mkiani.kama duma mkia wake ndio humsaidia kukata kona.hivyo kuna wanyama hawana shida ya kuwa na mkia mrefu km hana kaz nao.mfano chui angekuwa hana mkia mrefu ni rahisi kwa watoto wake kupotea sababu hufuata mkia wa mama kila anapokwenda!!
 
Mkuu [emoji120][emoji120][emoji120] [emoji119][emoji119]
 
Unailezeaje ile habari ya kwamba mbwa akimuona chatu huwa anajipeleka kwenyewe kwa chatu?
Tunaambiwa kwamba hata ukijaribu kumzuia mbwa huyo huwa na hali ya kulazimisha kwenda kwa chatu. Je, kuna ukweli gani juu ya hili jambo?
cc: adden
 
Back
Top Bottom