Uliza swali lolote linalohusiana na kampuni katika upande wa kodi na usajili

Ninarun business name, nataka ibadili iwe kampuni kamili sasa. Utaratibu ukoje hapa??
Namaliza ORS online tu au lazima kwenda brela?

Inawezekana, hakuna haja ya kwenda Brela unamaliza kila kitu kwenye ORS.. Utaratibu uko hivi

Unachotakiwa kufanya kabla hujaanza usajili wa kampuni inabidi ufunge kwanza jina la biashara hilo ambalo umelisajili, Huduma hii inaitwa "Ceasation of business name" na inalipiwa sh 10,000 tu. Kuna fomu utapaswa kujaza (form no 7 upande wa business name) na kuiwasalisha kwa njia ya mtandao (ORS)

Wakati wa kufunga hilo jina la biashara itabidi utoe sababu kuwa unalifunga ili uweze kutumia jina hilo katika kampuni.

Baada ya kukamilisha kufunga jina la biashara sasa hatua inayofuata ni kuanza usajili wa kampuni, Hapa itabidi uanze kuandaa kwanza Memorandum

Katika sehemu ya kuweka objectives(shughuli ambazo unazifanya au unatarajia kuzifanya) hakikisha objective no 1 itakua ni kutake over hilo jina la biashara na shughuli zake zote ziwe katika kampuni.

Baada ya hapo taratibu za kawaida za usajili wa kampuni zitaanza.
 
Bila kuwa na uelewa unaweza ukashangaa hata wao wanakaa kimya tu, Ndio maana inashauriwa kampuni iwe na Auditor au Consultant ili ikitokea TRA hawajakuambia vitu kama hivyo basi mtu wako akusaidie kupunguza mzigo wa kodi.
Kuna mtu huwa nafanya nae kazi,mara nyingi huwa analipa yeye withholding tax,sasa kuna kazi ilikuwa tumeanza kufanya,nikatoa na risiti kabisa,baadae akaisitisha ile kazi,hapo tra atailipa ile withholding tax?nafanyaje kuonesha sijaifanya hiyo kazi?
 
Kipindi unatoa risiti alikua amelipa kidogo au hakulipa kabisa!?

kama hakulipa kabisa njia rahisi (kama haujapita muda mrefu) iandikie barua hiyo risiti kuwa imekosewa and then TRA wataitoa kwenye hesabu zao hivyo haitakatiwa kodi yoyote ile, muhimu ni kuitunza tu hiyo barua.
 
Inawezekana, hakuna haja ya kwenda Brela unamaliza kila kitu kwenye ORS.. Utaratibu uko hivi

Unachotakiwa kufanya kabla hujaanza usajili wa kampuni inabidi ufunge kwanza jina la biashara hilo ambalo umelisajili, Huduma hii inaitwa "Ceasation of business name" na inalipiwa sh 10,000 tu. Kuna fomu utapaswa kujaza (form no 7 upande wa business name) na kuiwasalisha kwa njia ya mtandao (ORS)

Wakati wa kufunga hilo jina la biashara itabidi utoe sababu kuwa unalifunga ili uweze kutumia jina hilo katika kampuni.

Baada ya kukamilisha kufunga jina la biashara sasa hatua inayofuata ni kuanza usajili wa kampuni, Hapa itabidi uanze kuandaa kwanza Memorandum

Katika sehemu ya kuweka objectives(shughuli ambazo unazifanya au unatarajia kuzifanya) hakikisha objective no 1 itakua ni kutake over hilo jina la biashara na shughuli zake zote ziwe katika kampuni.

Baada ya hapo taratibu za kawaida za usajili wa kampuni zitaanza.
Shukrani Kiongozi
 
Kipindi unatoa risiti alikua amelipa kidogo au hakulipa kabisa!?

kama hakulipa kabisa njia rahisi (kama haujapita muda mrefu) iandikie barua hiyo risiti kuwa imekosewa and then TRA wataitoa kwenye hesabu zao hivyo haitakatiwa kodi yoyote ile, muhimu ni kuitunza tu hiyo barua.
1.Mkuu Nina swali mfano mi mtoto wangu kwa Sasa ana miaka 5 sasa nahitaji hata kama hajafikisha umri wa miaka 21 kwa badaye aje kuwa mkurugenzi kwenye kampuni yangu ila shida kwa Sasa hajafikisha huo umri Kuna nafasi labda inayobaki ili akija kufikisha hiyo miaka aje kuwa mkurugenzi na amiliki share zake....???

2.Na kwenye kampuni mtu mmoja kwenye share anaweza kumiliki share kubwa kuanzia mwisho ngapi...???

3.mfano mi nahitaji iwe hivi
Mimi 60%,wife 10% na mtoto 30% itakubalika kwa upande wa share za kampuni...???
Na hapo kwenye mtoto hizo share zinaweza kusubiria Hadi aje afikishe huo umri wa 21 ili aje kuzimiliki...???
 
Najibu kama ulivyouliza

1. Kama unahitaji kwa baadae inawezekana, soma vizuri jibu no 3 nimeelezea kwa kina

2. Mtu mmoja anaweza kumiliki hadi 99% ya share zote za kampuni, kitu kisichokubalika kisheria ni kwa mtu mmoja kumiliki 100% ya share za kampuni

3. Unachotakiwa kufanya kwa kuwa mtoto bado mdogo basi hiyo 10% ya share mtaiacha ibaki kwenye kampuni (reserved)

Yaani wewe chukua 60% na wife mpe 30% halafu hiyo 10% iweke tu pembeni mpaka pale mtoto atapokua mtafanya kitu kinaitwa “allotment of shares” ambapo hizo 10% zilizokua reserved mtaziallot kwa huyo mtoto sasa (ambae at that time atakua mtu mzima)
 
Vipi kama ukiamua kubadili jina la Kampuni, hizo penati hazifutiki automatically?

HAPANA!
Unapobadili jina la kampuni haupewi Certifcate of Incorporation mpya bali unapewa Certificate of Change of name ambayo inakua inaonesha jina la zamani na la sasa yaan mfano kampuni iliokua inaitwa ABC Limited sasa inaitwa XYZ Limited..[emoji2] Tabu itabaki palepale
 
Naomba kuukiza kwa mara nyingine.

Nimeanza na kampuni yangu ina M30 na inamilikiwa na watu wawili kama ilibyoandikwa kwenye memorandum.
Ikiwa nuwekezaji mpya ameingia na anataka kuongeza kushare shares zako. utaratibu zinakuwaje ili kupata umiliki wa kampuni na utambukike brela kampuni ina watu wa 3.

Swali lingine, kwenye memorandum tumesema mfano mteja wetu ni M30 baada ya kufanya biashara mtaji unakuwa M100, hivi tutaenda brela kubadili memorandum au tunafanyaje ili kampuni itambulike kwasasa inamiliki M100.

Mwisho, kampuni yangu nilioeozesha shuguli zake zote ambazo itajishughilisha, lakini kwa kwasasa naona ni bora zile shughuli nilizoweka ziwe zinaendeshwa kama kampuni ambayo inamilikiwa na kampuni mama, nataka kujua ikiwa kama kampuni inataka kufungua kampuni nyingine, natumia memorandum mpya au ni hile ya kampuni mama kwa vile shughuli imeshaelezwa ya kampuni mpya iko ndani ya kampuni mama.

Asante
 
1. Kuna njia 2 kuu za mtu kuingia kwenye kampuni kama shareholder

Njia ya kwanza ni kufanya allotment of shares (hii inafanyika endapo kampuni wakati inasajiliwa iliacha baadhi ya shares zake pembeni hazikua na mtu, hivyo mtu mpya anapoingia anapewa hizo shares kwa kujaza allotment form (Form no 55a) ya Brela

Njia ya pili ni Transfer of shares kutoka kwa mtu A kwenda kwa B. Process hii huwa inaanzia TRA na kumalizikia Brela

Ni ndefu kidogo na ina utaratibu na gharama zake pia.

2. Kisheria inaruhusiwa kuongeza mtaji wa kampuni, na hii ni Process ya Brela. Unachotakiwa kufanya ni kuandaa Board Resolution pamoja na kujaza form no 66 (Increase of Authorised Share Capital)

Note: Unapoongeza Shares, kubadilisha shareholder au Directors Memorandum ya kampuni huwa haibadiliki, inabaki vile vile.. Ila popote pale utapoipeleka itabidi uambatanishe na Official Search ya kampuni ambayo itaonyesha hayo mabadiliko

3. Kampuni ni Entity inayosimama yenyewe kisheria, japo inawezeka kwa kampuni A kuwa mmiliki wa kampuni, au tuseme kwa urahisi kampuni inaruhusiwa kumiliki kampuni nyengine kisheria kama wewe unavyomiliki kampuni yako sasa hivi. So utapotaka kufungua kampuni nyengine itabidi uandalie Memorandum na Documents nyengine zote za usajili kama kawaidia halafu kwenye sehemu ya shareholder ndipo utaiweka hiyo Kampuni nyengine sasa kama ndio mmoja wa wamiliki wa kampuni hii
 
Kwakweli majibu Yako ni Ya Kitaalam sana na Yaliyoshiba haswa Sichoki kuyasoma. Swali langu ni Elimu hii umeipata Darasani tu au Umeongeza na Experience ya Miaka Mingi katika Field Hiyo?
 
Shukurani sana mkuu nimekuelewa mpaka hapo.

Endelea kutupa ujuzi maana bado tuna mengi ya kuuliza.

Hivi ni sahihi mtu akiniuliza kampuni yako ni ya aina gani, Nikamjibu ni Services business Company, hii inaeleweka. maana imebased kutoa huduma mbali mbali, kama shughuli za techology, migahawa, Usafirishaji nk..Na kila huduma itakuwa na jina lake.

2. Naomba kujua watu ambao ni muhimu(wanaostahili kuwepo) kuendesha kampuni kila siku na majukumu yao.

3. nataka kampuni yangu au huduma zinazotolewa na kampuni yangu ziwe kwenye nominate kwenye tunzo mbali mbali, hiii nafanyaje, au namna ya kuomba kuwepo kwenye tunzo hizo. yaani namna ya kuwaandikia wahusika wakuweke kwenye tunzo zao na kuna njia gani zingine kuwezesha kampuni yako hiwe kwenye nominate mabli mbali.( maana nasikia mambo haya kampuni zinazotambulika ,najiuliza kutambulika vipi au ndo hii ya kutambulika mtaani, lakin nakuwa na shaka, maana nyingi ni maarifu lakini huzisikii kwenye mambo ya tunzo)

Asante.
 
Darasa kidogo lakini experience ya miaka kadhaa kwenye field hii ndio msingi mkuu. Maana darasani hawafundishi kila kitu na haupati ule uhalisia wenyewe wa mambo yanavyokua huku nje.
 
Shukurani sana mkuu nimekuelewa mpaka hapo.

Endelea kutupa ujuzi maana bado tuna mengi ya kuuliza.

Hivi ni sahihi mtu akiniuliza kampuni yako ni ya aina gani, Nikamjibu ni Services business Company, hii inaeleweka. maana imebased kutoa huduma mbali mbali, kama shughuli za techology, migahawa, Usafirishaji nk..Na kila huduma itakuwa na jina lake.

2. Naomba kujua watu ambao ni muhimu(wanaostahili kuwepo) kuendesha kampuni kila siku na majukumu yao.

3. nataka kampuni yangu au huduma zinazotolewa na kampuni yangu ziwe kwenye nominate kwenye tunzo mbali mbali, hiii nafanyaje, au namna ya kuomba kuwepo kwenye tunzo hizo. yaani namna ya kuwaandikia wahusika wakuweke kwenye tunzo zao na kuna njia gani zingine kuwezesha kampuni yako hiwe kwenye nominate mabli mbali.( maana nasikia mambo haya kampuni zinazotambulika ,najiuliza kutambulika vipi au ndo hii ya kutambulika mtaani, lakin nakuwa na shaka, maana nyingi ni maarifu lakini huzisikii kwenye mambo ya tunzo)

Asante.

1. Ni sahihi ingawa huwa tunapenda zaidi kuziita kampuni za aina hiyo kama “General Commercial Company” means kunakua na biashara za kutoa huduma kama ulivyoainisha hapo juu. So inakua nzuri zaidi ukiita General Commercial Company japo hata hivyo ulivyosema pia ni sahihi

2.kisheria kabisa kampuni inabidi iwe na watu watatu muhimu ili kuanzishwa, ambao ni Director, Shareholder na Company secretary (Mkurugenzi, mmiliki na mtendaji mkuu wa kampuni) hapo unakua umemaliza na kampuni inaruhusiwa kufanya kazi

Ila kibiashara sasa hapa inategemea na aina yako ya biashara ila watu wa muhimu zaidi ukiondoa hao hapo juu unaweza kuweka Consultant/Auditor/Lawyer ambae huyu atakuongoza kwenye masuala ya kodi,usajili, vibali, leseni n.k (sio lazima umuajiri bali unaweza mkawa mnalipana kwa kazi)
Then mhasibu wa kampuni kwa ajili ya kutunza mahesabu ya day to day business operation.
Baada ya hapo sasa position nyengine itategemea na aina ya kampuni na biashara unazofanya

3. Fanya kazi vizuri, tangaza huduma zako, gusa watu wengi na tuzo zitakuja tu. Ingawa kila taasisi inayoandaa tuzo wanakua na utaratibu wao ambao mimi binafsi siwezi kuwasemea, ila kuwa mfuatiliaji mzuri tu huwa zinatangazwa na utaratibu wake wa kuomba (japo kampuni nyingi zinajali zaidi kufanya biashara na kupata faida kuliko kupata hizo tuzo)
 
Asante mkuu, nashukuru kwa hili.
 
Remove for 14b for beneficial owner, that form should be submitted after having obtain incorporation number.

Naomba msaada nmekwama kwenye brela system wamenipa haya marekebisho nifanye ila hio form 14b kila nikiiondoa system inagoma kuendelea
 
Mkuu,

1. Mie naomba kufahamu namna ya kufanya mabadiliko ya MoU & company articles. Nimeshasajili na kampuni ina operate tayari. Sema nataka niongezee baadhi ya huduma. Mfano, sisi tulisajili kampuni ya usafi, ila jina la kampuni ni general kwa maana hali- reflect kazi za usafi pekee na tunataka kujipanua tufanye na kazi nyingine mfano ' General supplies' n.k

Je taratibu za kubadili zikoje na gharama kwa ujumla zikoje?
Tunaweza fanya wenyewe online tukapunguza gharama za wanasheria?

2. Je, zipi ni faida za kuweka kazi nyingi chini ya kampuni moja ukilinganisha na kusajili kila kampuni na kazi zake specific ?, yaani unakuwa na kampuni zaidi ya moja badala ya kuwa na kampuni moja tu ukaipa kazi zote.

## Ahsante. Natanguliza shukrani.
 
Ukiingia kwenye website ya Brela kuna form 14b ambayo hii inasainiwa na Declarant (Director au Company secretary) na inagongwa mhuri wa mwanasheria. Ina page 1 tu.

So ondoa hiyo 14b ya Beneficial Owner halafu weka hiyo 14b nyengine. Ukikwama kuiona nitext whatsapp 0714499248 nikutumie
 
Mkuu,

1. Mie naomba kufahamu namna ya kufanya mabadiliko ya MoU & company articles. Nimeshasajili na kampuni ina operate tayari. Sema nataka niongezee baadhi ya huduma. Mfano, sisi tulisajili kampuni ya usafi, ila jina la kampuni ni general kwa maana hali- reflect kazi za usafi pekee na tunataka kujipanua tufanye na kazi nyingine mfano ' General supplies' n.k

Je taratibu za kubadili zikoje na gharama kwa ujumla zikoje?
Tunaweza fanya wenyewe online tukapunguza gharama za wanasheria?

2. Je, zipi ni faida za kuweka kazi nyingi chini ya kampuni moja ukilinganisha na kusajili kila kampuni na kazi zake specific ?, yaani unakuwa na kampuni zaidi ya moja badala ya kuwa na kampuni moja tu ukaipa kazi zote.

## Ahsante. Natanguliza shukrani.

1. Kufanya mabadiliko yoyote katika kampuni kitu cha kwanza kabisa ni kuandaa Board Resolution ambayo itaonyesha Board ilikaa kikao na kupitisha hayo mabadiliko kwa pamoja, hii inasainiwa na Director na Company Secretary

Kwa inshu yenu Mnaweza kuongeza objectives nyengine za shughuli mnazotaka (kama hamkuziweka awali)

Gharama ni 22,000 tu utalipia Brela

Yeah mnaweza kufanya, ila kikubwa muwe mnajua tu jinsi ya kuandaa kwa usahihi hizo documents pamoja na kutumia ORS

2. Kuwa na utitiri wa makampuni ni kuongeza wingi wa kodi na compliances, kama HAUNA SABABU ZA MSINGI ni bora ukawa na kampuni moja ambayo itabeba shughuli zako zote za kibiashara kwa pamoja.
 
Back
Top Bottom