Uliza swali lolote linalohusiana na kampuni katika upande wa kodi na usajili

Ahsante sana mwanzilishi wa uzi huu ambao umetoa majibu mengi ya manufaa kwetu wafanyabiashara.
Naomba kuuliza maswali:

1. Kampuni ikiwa imesajiliwa na ikapita miaka miwili bila kuchukua TIN NUMBER wala LESENI na kufanya TAX CLEARANCE, kuna penalties zozote TRA(kikodi) au Brela zinaweza ilima/ikumba kampuni hiyo?

2. Bado kampuni ambazo ni za Kilimo na uchakataji wa mazao ya Kilimo zina VAT ya 0% kwa bidhaa wanazozalisha (zilizo ongezewa virutubisho) au kuna mabadiliko?

3. Kwa ushauri bodi ya wakurugenzi inatakiwa kuwa na watu wangapi kwa kampuni inayoanza?

Natanguliza shukrani.
 
1. Kufanya mabadiliko yoyote katika kampuni kitu cha kwanza kabisa ni kuandaa Board Resolution ambayo itaonyesha Board ilikaa kikao na kupitisha hayo mabadiliko kwa pamoja, hii inasainiwa na Director na Company Secretary

Kwa inshu yenu Mnaweza kuongeza objectives nyengine za shughuli mnazotaka (kama hamkuziweka awali)

Gharama ni 22,000 tu utalipia Brela

Yeah mnaweza kufanya, ila kikubwa muwe mnajua tu jinsi ya kuandaa kwa usahihi hizo documents pamoja na kutumia ORS

2. Kuwa na utitiri wa makampuni ni kuongeza wingi wa kodi na compliances, kama HAUNA SABABU ZA MSINGI ni bora ukawa na kampuni moja ambayo itabeba shughuli zako zote za kibiashara kwa pamoja.
Nashukuru sana Mkuu kwa majibu yako mazuri.
Nyongeza,

1. Mfumo wa ORS bila shaka nitaupata kwente website ya BRELA si ndio?
2. Unaweza kunitajia kwa uchache kuhusu hizo documents kuwa ni ngapi na za aina ipi?
3. Kwa ushauri wako, kwa beginner kama mimi, unashauri nijaze mwenyewe au ni muhimu kumtafuta mtu? Itakuwa rahisi kwangu?
4. Kama si rahisi Je, gharama za kusaidiwa kujaza ni kiasi gani na nani anaweza kunisaidia? Mwanasheria wa kwanza aliyetusaidia kusajili kwa sasa ana majukumu mengi.

Natanguliza shukrani zangu.
 
Ahsante sana mwanzilishi wa uzi huu ambao umetoa majibu mengi ya manufaa kwetu wafanyabiashara.
Naomba kuuliza maswali:

1. Kampuni ikiwa imesajiliwa na ikapita miaka miwili bila kuchukua TIN NUMBER wala LESENI na kufanya TAX CLEARANCE, kuna penalties zozote TRA(kikodi) au Brela zinaweza ilima/ikumba kampuni hiyo?

2. Bado kampuni ambazo ni za Kilimo na uchakataji wa mazao ya Kilimo zina VAT ya 0% kwa bidhaa wanazozalisha (zilizo ongezewa virutubisho) au kuna mabadiliko?

3. Kwa ushauri bodi ya wakurugenzi inatakiwa kuwa na watu wangapi kwa kampuni inayoanza?

Natanguliza shukrani.
Mkuu, ngoja mtaalamu aje. Ila jibu la swali namba 3 ni atleast directors wawili.
 
Ahsante sana mwanzilishi wa uzi huu ambao umetoa majibu mengi ya manufaa kwetu wafanyabiashara.
Naomba kuuliza maswali:

1. Kampuni ikiwa imesajiliwa na ikapita miaka miwili bila kuchukua TIN NUMBER wala LESENI na kufanya TAX CLEARANCE, kuna penalties zozote TRA(kikodi) au Brela zinaweza ilima/ikumba kampuni hiyo?

2. Bado kampuni ambazo ni za Kilimo na uchakataji wa mazao ya Kilimo zina VAT ya 0% kwa bidhaa wanazozalisha (zilizo ongezewa virutubisho) au kuna mabadiliko?

3. Kwa ushauri bodi ya wakurugenzi inatakiwa kuwa na watu wangapi kwa kampuni inayoanza?

Natanguliza shukrani.

1. Kwa upande wa TRA huwa busara zinatumika endapo kama hukuwahi kuchukua TIN kabisa, naposema busara namaanisha za kibinadamu maana kwa sasa hivi sheria inasema unaposajili kampuni mpya unapaswa ukachukue TIN bila kuchelewa..

ila sasa kwa kampuni za zamani unaweza kuongea nao ili wasikulime penalty za huko nyuma, but as I said uwe hukuchukua TIN kabisa, kama ulichukua na kukimbia hapo hakuna namna penalty zitakuhusu

Upande wa Brela Penalty utazikuta tu haziyokua na ujanja wa kuepuka, uzuri penalty zake ni ndogo na unaweza kuzimudu. Maana Brela kwa mwaka unalipia 22,000 na penalty ni 2500 zidisha miezi yote uliyochelewa mpaka sasa

2. Kama kuna mabadiliko basi sijayasikia/sijayafahamu maana na mimi mpaka mara ya mwisho najua kuwa ni 0%

3. Angalau wakurugenzi wawili wanahitajika wakati kampuni inapoanzishwa
 
Nashukuru sana Mkuu kwa majibu yako mazuri.
Nyongeza,

1. Mfumo wa ORS bila shaka nitaupata kwente website ya BRELA si ndio?
2. Unaweza kunitajia kwa uchache kuhusu hizo documents kuwa ni ngapi na za aina ipi?
3. Kwa ushauri wako, kwa beginner kama mimi, unashauri nijaze mwenyewe au ni muhimu kumtafuta mtu? Itakuwa rahisi kwangu?
4. Kama si rahisi Je, gharama za kusaidiwa kujaza ni kiasi gani na nani anaweza kunisaidia? Mwanasheria wa kwanza aliyetusaidia kusajili kwa sasa ana majukumu mengi.

Natanguliza shukrani zangu.

1. Yes, au kwa urahisi zaidi ingia hapa www.ors.brela.go.tz

2. Board Resolution na Consolidated Form.. kama utabadilisha objectives basi pia unaweza kufanya ammendment ya memorandum yako

3. Kila jambo lina utaalam wake, masuala ya kampuni yanahitaji ufahamu zaidi ya kutumia internet.. kama huelewi au unataka kujifunza sikushauri ujifundishie kwenye kampuni yako, utasumbuka.. bora upate mtaalam

4. Kama ukihitaji mtu wa kukusaidia namba hii hapa ya Section Twenty, 0714499248 ipo kawaida na whatsapp. Karibu
 
Ukiingia kwenye website ya Brela kuna form 14b ambayo hii inasainiwa na Declarant (Director au Company secretary) na inagongwa mhuri wa mwanasheria. Ina page 1 tu.

So ondoa hiyo 14b ya Beneficial Owner halafu weka hiyo 14b nyengine. Ukikwama kuiona nitext whatsapp 0714499248 nikutumie
Sawa nashukuru nmeipata
 
1. Yes, au kwa urahisi zaidi ingia hapa www.ors.brela.go.tz

2. Board Resolution na Consolidated Form.. kama utabadilisha objectives basi pia unaweza kufanya ammendment ya memorandum yako

3. Kila jambo lina utaalam wake, masuala ya kampuni yanahitaji ufahamu zaidi ya kutumia internet.. kama huelewi au unataka kujifunza sikushauri ujifundishie kwenye kampuni yako, utasumbuka.. bora upate mtaalam

4. Kama ukihitaji mtu wa kukusaidia namba hii hapa ya Section Twenty, 0714499248 ipo kawaida na whatsapp. Karibu
Ahsante sana Mkuu.
 
1. Kwa upande wa TRA huwa busara zinatumika endapo kama hukuwahi kuchukua TIN kabisa, naposema busara namaanisha za kibinadamu maana kwa sasa hivi sheria inasema unaposajili kampuni mpya unapaswa ukachukue TIN bila kuchelewa..

ila sasa kwa kampuni za zamani unaweza kuongea nao ili wasikulime penalty za huko nyuma, but as I said uwe hukuchukua TIN kabisa, kama ulichukua na kukimbia hapo hakuna namna penalty zitakuhusu

Upande wa Brela Penalty utazikuta tu haziyokua na ujanja wa kuepuka, uzuri penalty zake ni ndogo na unaweza kuzimudu. Maana Brela kwa mwaka unalipia 22,000 na penalty ni 2500 zidisha miezi yote uliyochelewa mpaka sasa

2. Kama kuna mabadiliko basi sijayasikia/sijayafahamu maana na mimi mpaka mara ya mwisho najua kuwa ni 0%

3. Angalau wakurugenzi wawili wanahitajika wakati kampuni inapoanzishwa
Mkuu Ahsante kwa majibu.

1. Okay, kwa Brela nimekuelewa ila kwa TRA bado sijaelewa; ningependa kujua ufafanuzi juu ya faini zilizopo kwa kuchelewa kuchukua TIN NO. : ni kiasi gani cha fedha, maana hakuna makadirio yoyote ya kikodi nimezungumza na TRA hapo awali.

2. Lakini pia kwa wale ambao biashara zinahusu uchakataji mazao, leseni bado zinatokea wizara ya viwanda? kama ndiyo; utaratibu umekaaje?

1. Sheria inasema unapoanza biashara unapaswa kuchukua TIN ndani ya siku 15 tu tangu biashara yako ianze, kama hujachukua TIN na wala kufanya cjochote ipande wa TRA adhabu yake ni sh 1.5M

Hiyo nimekupa hapo ni base ya kisheria, lakini ukirejea maelezo yangu ya awali kuwa hayo mambo yanaongeleka ni suala tu la kueleweshana na Tax Officer kwamba kwanini hadi leo hujachukua TIN na wala hujafanya makadirio wakati usajili wa kampuni umeshafanya (na pengine biashara umeshaanza)

2. Utaratibu wa kuchukua leseni wizara ya viwanda na biashara ni kuandaa documents zifuatazo

A. Certificate of Incorporation
B. TIN
C. Memorandum
D. Tax clearance
E. Mkataba wa pango
F. Vitambulisho vya madirector

Maombi yanafanyika kwa njia ya mtandao (Online) kupitia Business Portal ya serikali
 
Mkuu, naomba kujua iwapo tutaamua ku-upgrade mtaji wetu kwenye MoU kutoka 5M to 100M. Je, kuna impact yoyote kwenye masuala ya kodi ama gharama nyingenezo?
 
Kuupgrade mtaji mnalipia tu Brela Registration Fee ya mtaji husika.

Mfano mtaji wenu wa milioni 5 mlilipa almost 247k, mnataka kupanda mpaka mtaji wa milion 100 ambao regostration fee yake ni 440k.

Kimahesabu hapa utatoa 440k-247k jibu utalopata ndio kiasi utachoongezea, halafu utaongeza na sh 22,000 ya filling fee

Kikubwa uandae Board Resolution na ujaze form no 66 ya kuongeza mtaji
 
Thanks Mkuu, hakuna implications zozote upande wa kodi TRA?
 
TRA kodi ya kampuni (corporate tax) huwa inakatwa kwenye faida, so zoezi la kuongeza mtaji halina madhara ya moja kwa moja upande wa Tra
 
Gharama ya kusajili limited company huwa inategemea na share capital yake, nakuainishia kila kundi la share capital na gharama yake hapa chini

Mtaji Gharama za usajili
1. 20k-1M - 167,200
2. 1M-5M- 247,200
3. 5M-20M- 332,200
4. 20M-50M- 362,200
5. 50M mpaka mwisho 512,200
Niko ughaibuni nimemtumia ndugu yangu kusajili kampuni ya ujenzi.
Naye ni director . Kampuni ina wakurugenzi 3
Ila gharama alinambia ni 1,988,500.

Kwa gharama hizo ulizo ainisha maana yake amenipiga na kitu kizito?
 
Mkuu nilikuwa na Biashara niliifunga na kwenda masomoni.Ila sikujua taratibu lazima uandike barua TRA kuwajilisha?
 
Yeah ni muhimu ufanye hivyo, na endapo ulishafanya makadirio ya kodi kwa mwaka huu basi andika barua ya kufunga biashara then chukua na barua ya serikali ya mtaa ya uthibitisho kwamba biashara imefungwa na kodi zilizobakia (za mwaka huu) hautozilipa.. na kama una leseni ya biashara pia andika barua ya kufunga leseni yako
 
Back
Top Bottom