Uliza ujibiwe kuhusu madini, gesi na mafuta

Hongera sana ruby garnet kwa kupambana na kutumia elimu yako kuishi! Nimekuwa napitia uzi wako huu - ni wa 2017! Tafadhali tupe hali ilivyo sasa (2022) katika sekta ya uchimbaji, ununuzi na uuzajia wa dhahabu (uuzaji kuanzia kwa wachimbaji wadogo , brokers hadi kwa Dealers na kama wapo MASTER DEALERS.
 
A
Acid gani
 
Dhahabu mbichi ni ipi hiyo?
 
Asante, nina swali la nyongeza kwa ufafanuzi zaidi. Yaani ni ile ambayo bado ina udongo na mawe, ambayo haijatenganishwa na "uchafu" huo? Kama ni hiyo, inauzwaje sasa kwa hao masonara au ndiyo mpaka waichome wenyewe? Hili likoje vidmate?
Inakuwa ishasafishwa na wachimbaji ila inachomwa na moto mdogo wa kawaida ambao hauwezi kuchoma uchafu wote hivyo dealer mkubwa anaichoma na gesi mpaka inayayuka kama mshumaa then inapimwa gold purity % na purity ndiyo itakayoamua bei utakayopewa kwa kila gram
 
Nitafanya uchambuzi kwa utulivu Kisha nipost Mkuu. Asante kwa kuomba Hilo umenipa swala mhimu la kutazama masoko yetu
 
Asante, nina swali la nyongeza kwa ufafanuzi zaidi. Yaani ni ile ambayo bado ina udongo na mawe, ambayo haijatenganishwa na "uchafu" huo? Kama ni hiyo, inauzwaje sasa kwa hao masonara au ndiyo mpaka waichome wenyewe? Hili likoje vidmate?
Kunauchomaji wa Aina 3. 1. Kuchoma kwa Moto wa kawaida ili kutoa Mercury 2. Kuchoma kwa gas is uchafu wa wakawaida(physical uchafu) utoke na dhahabu ikae pekeyake hii ni kuchoma mpaka gold inayeyuka na Kuwa Kama uji kabisa.
3. Uchomaji wa kusafisha gold ili ipande asilimia ya purity, hii huitwa gold purification. Ndiyo huisafisha gold Hadi kufikia asilimia 99.99%
 
Mkuu kwa hio tukianza kuzika watu wetu katika mass graves tunaweza ongeza uwezekano wa kuzalisha mafuta mengi kutoka na masalia ya viume binadamu?
 
Ooh ndio maana nikienda kwenye masoko mengi ya dhahabu naona mitungia ya gesi ni kwa ajili ya kuchoma sio
 
Ooh ndio maana nikienda kwenye masoko mengi ya dhahabu naona mitungia ya gesi ni kwa ajili ya kuchoma sio
Ndiyo kwa ajiri ya kuchoma Kama nilivyoeleza katika namba 2
 
Mkuu kwa hio tukianza kuzika watu wetu katika mass graves tunaweza ongeza uwezekano wa kuzalisha mafuta mengi kutoka na masalia ya viume binadamu?
Mafuta na gas za Sasa zimejitengeneza zaidi ya 16million years ago hasa Kati ya 100-250 million years ago. Hivyo siyo swala la muda mfupi. Pia Kuna mazingira yanayohitajima mmea au mnyama kufunikwa na udongo Kisha akaweze Kuwa mafuta ama gasi. Mazingira haya yanahitajika kwenye maji au mazingira yenye majimaji kwa muda mrefu Kama vile bahari, ziwa ama sehemu za chemichemi za maji nyingi Sana
 
Yaaah hata mimi najua lazima ichomwe sana na kupata purity then biashara ainaendelea; lakini hawa big dealers, huwa wana nunua chini ya bei ya dhahabu ya siku hiyo! Wana nunua kwa kutumia bei ya dhahabu ya 20K au 22K! Kwa nini sijui!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…