Tetesi: Umakamo wa Urais Zanzibar ni Joto

1. Unauhakika ni kauli tu? Kina saa Nane kupotea na kina Lissu kutandikwa risasi mchana kweupe ni sababu ya nini zaidi ya kauli tu zilitozotolewa majukwaani? Ama kutandikwa wapinzani wa Serikali haiwi security concern? Kwanini tuna selective hivi na double standards?

2. Ni vizuri umekiri hujui motives za serikali maana ni zaidi ya uonevu kuwaweka watu mahabusu wakati ushahidi hautoshi! Kwanini msiwaachie kwa probation kuliko kuwasweka ndani bila fair hearing?

Hakuna mtu aliyewatetea Uamsho bali watu wanataka HAKI itendeke.... Kma ushahidi hamna waachiwe otherwise ushahidi uwekwe wafungwe tujue moja... that's all watu wanataka sio Kingine.

Haya masuala mnaweza tetea ila siku ukibambikiwa kesi alafu ikaenda miaka 10 ndio ikajulikana huna hatia... Ndio utaelewa jinsi uendeshaji kesi Tz ulivyo na kero
 
Kuna mtu anaitwa Hamad Masoud japo siku hizi hasikiki sana lakini jamaa naye ni miongoni mwa watu wanaokubalika sana Zanzibar hususani kisiwani Pemba

Tunataka mtu anae kubalika kite visiwani
 
Acha upotoshaji, mtu amefikia mpaka kuwa AG wa serikali halafu unakuja na santuri zako za kuungaunga. Inamaana serikali haikumfanyia vetting kabla ya kumteuwa? Mbona unataka kudhalilisha serikali wewe?!
 
Zanzibar kwa sasa tunamuhitaji mtu kama Othman, tunajuwa dhamira yake kwa Zanzibar ni njema, ni mtu mwenye vision, ni mtu anaependa maridhiano, kama hujuwi maridhiano ya sasa yeye ana mchango mkubwa katika kufanikiwa kwake. Si mtu mfia chama ni mtu anaweka maslahi ya nchi mbele na maamuzi yake siku zote yanalenga maslahi mapana ya nchi. Musiompenda Othman tunazijuwa sababu kwa nini hamumpendi...
 
Hii ni fitna na inshaAllah hamtafanikiwa na fitna zenu.
 
Haswaaaaaa!
 
Like I said ‘Othman Masoud’ is tactical anafahamu change is not abrupt it requires adjustment kuuma na kupuliza mpaka kufikia lengo. For him is to come out of the union.

Lakini kama ni swala autonomy na devolution ya Zanzibar kujiamulia kwa asilimia kubwa, serikali ya muungano imefanya vya kutosha Zanzibar kujiendesha kwa aspects za mahitaji yake bila ya serikali kuu.

Maana yake nini sasa wanaopinga muungano ni watu wanaosukumwa na xenophobia za interaction ya watu wa bara na visiwani; na hilo jambo aliwezi chekewa.
 
Duni hamna kitu. Zanzibar inahitaji kwenda mbele, Hata Mwinyi atamhitaji Othman Masoud. Kuwapa nafasi hiyo watu kama Juma Duni, na akina Ismail Jussa ni kuchagua kurudi nyuma.

Ila wahafidhina ndani ya CCM sidhani kama CCM watamhitaji Othman.
Nami naona hilo likitatokea la ccm kumkataa mteuliwa
 
Hizi ndio siasa zinazo waponza you ppl don’t evolve mnatunga mambo mitandaoni ya kujifurahisha wenyewe or issues which society have forgotten about na kudhani zinasaidia ku mobilise support kila siku mnarudia rudia ujinga ambao watanzania awau elewi.

Hata mimi Ben Saanane kaniuma sana he was so clever, eclectic and young; ni kijana ambae angekuwa kiongozi muhimu wa taifa kwa leo regardless ya upande wake. Muhimu ni ability and his vision of politics.

But life goes on tunaomjua uwezo wake ni JF members, kurudia x 2 uwezo wake won’t bring him back; na serikali imesha move on sasa hivi ipo kwa ajili ya kuwainua watanzania waliochini.

That’s life and things happen
 
Umemaliza,hafai [emoji16]
Othman ndie anaetufaa, labda hafai kwa mujibu wa siasa za CCM Bara na wahifidhina wachache Zanzibar za kulazimisha kuitawala Zanzibar kwa maslahi yao binafsi.

Kwa wazanzibari wengi wana muelekeo mmoja na muelekeo ni kupata mamlaka kamili ya nchi yao! Hili haijalishi kama wengine wasiokuwa wazanzibari wanalipenda au hawalipendi. Jaji Warioba alishalieleza hili kwa urefu kabisa. Sote tunajuwa kwamba hakuna nchi inayotawalika kimabavu katika karne hii, ni suala la muda tu. Hilo ambalo mnaliogopa ndilo litalotokea. Kama hamtaki muungano uvunjike, cha kufanya pekee ni kuruhusu kulijadili hili kwa uwazi na kuruhusu maoni ya wahusika wenyewe. Ingawa hili la kukusanywa maoni lilifanyika ila kwa sababu matokeo ya maoni hayo hayakuwaridhisha mkaamua kufanya yenu kuvuruga mchakato mzima wa katiba!

Kwa ufupi ni hivi, kama wazanzibari hawatapata mamlaka kamili kwa maana ya serikali tatu, tusitegemee muungano kudumu. Na hata ukidumu hautakuwa na mafanikio wala maridhiano. Mivutano hii iliopo itazidi na hali inaweza kuwa mbaya zaidi!
Sasa akili vichwani mwenu!
 
Wampe mzee wa kifo cha mende Babu duni
Na Duni nae hana msimamo tofauti na Othman na wazanzibari wengine. Kama mnataka kujuwa what is common between them ni kwamba wote wanataka mamlaka ya Zanzibar. Kwa hio like Duni like Othman. Labda itakuwa mnauogopa uwezo mkubwa wa akili wa Othman!
 
Sawa, kama zipo wazi nini kimeshindikana kuhukumiwa?
Do you know katika makosa yao kuna mengine wakipatikana na hatiya, adhabu yake ni kunyongwa?

Sasa serikali azifikirii ovyo kama unavyodhani, pamoja na ushahidi walionao kutokana na social context za kiusalama; kuna makosa mengine bora wacheleweshe kesi ili wahusika wa reform, kuliko kuwahukumu for social cohesion purposes.

Kazi ya kuongoza nchi sio rahisi kama mnavyodhani; otherwise those old reprobates kwa sheria za Tanzania ambazo hazijawi tumiwa makosa yao ni kunyonga kwa mujibu wa katiba.

Sio kila mara serikali inaposema aijakamilisha ushahidi uiamini sometimes wana sababu zao za national security concerns.

Cha muhimu ni wewe kuelewa uamsho ni enemies of the state.
 
Nani ametunga? Lissu si alisema hadharani kwamba wanataka kumuua what happened next? Saa Nane alisema pia kwamba anafuatiliwa kuuawa na hata vitisho viliwahi kupostiwa humu nini kilifuata?
Vile vitisho vingetolewa na UAMSHO kwa mawaziri wa CCM hvi pangekalika? Mbona una double standards mkuu
.But life goes on tunaomjua uwezo wake ni JF members, kurudia x 2 uwezo wake won’t bring him back; na serikali imesha move on sasa hivi ipo kwa ajili ya kuwainua watanzania waliochini.

That’s life and things happen
Ila kwa Uamsho life doesn't move on hta kma serikali kwa sasa "ipo kwa ajili ya kuwainua waTZ waliochini"? Ama ina move on pale tu maslahi yake yasipoguswa?
 
Ndugu hakuna kitu kigumu kuthibitisha mahakamani kama ‘actus reus’ and ‘mens rea’ za GBH especially katika mazingira ya Lissu.

Anachoongea ni ku entertain tu audience yake ya watu kama nyie it is not straight forward as he potrays; but then Lissu is not a criminal lawyer by trade.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…