Bukyanagandi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2009
- 11,061
- 16,753
Baada ya kufariki Makamo wa kwanza Maalim seif sharif Hamad, Kumekuwa na minong’ono ya hapa na pale kuhusu ni nani atakae weza kuvaa viatu japo nusu, vya marehemu Maalim Seif, mpaka sasa majina ni mawili, Juma Duni na Othman Masoud Ambae aliwahi kuwa mwanasheria mkuu wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar wakati wa DR Shein.
Othman Masoud alitumbuliwa kutokana na misimamo yake ya kutetea katiba ya Zanzibar na maslahi ya Zanzibar katika bunge la katiba mpya.
Bwana Othman hakujali maslahi yake binafsi na kuweka uzalendo zaidi, sikiliza mahojiano yake juu ya serikali ya umoja wa kitaifa akitoa maoni yake.
Mimi binafsi namkubali huyu kijana mwenzangu, kwanza ni msomi wa kweli, mzalendo na yupo tayari kutetea maslahi ya Zanzibar, naamini kama atapata fursa ya kuwa makamo ataweza kumshauri Mwinyi na kumsaidia katika kuwaletea maendeleo wazanzibari.
Mwenye msimamo thabiti na ambae haogopi kitu ni Mh. Juma Duni - huyo ndiye mwakilishi hasa wa misimamo ya marehemu Maalimu Seif- tulimuona wakati wa kampein alikuwa ng'ang'ari kabisa - sasa siasa za Zanzibar zilivyo si ajabu akatafutiwa sababu/kisingizio cha kumzima ili hasipewe wadhifa wa the late Maalimu - yetu macho.