Umalaya ni mbaya sana! Ewe mwanaume mwenye familia, itunze

Inasikitisha, jamaa akashindwa kumpa mwanaye mtaji hata wa 10M dogo afungue duka la viatu Moro. Yeye anapambana na uchi tu. Yaani mzee mzima mwenzangu mwenye miaka 50's anakuwa ndio kama anaanza balehe.

Inasikitisha. Mungu amsaidie.
Tofautisha kipaumbele mkuu😅
 
Duh,paliponifikirisha ni hapo uliposema eti "alishauriwa na Sheikh wa Bakwata amloge Mkewe".
 
Hiki kisa kimenisikitisha sana.

Kuna jamaa yangu na rafiki yangu kitambo toka 1980's kule Morogoro na tulianza biashara naye za kuuza/kuchukua Sigara kwenye treni kipindi hiko.

Mambo yakatunyookea tukaanza kufanya biashara za Mahindi kwenye mikoa ya Songea na Morogoro. Mwaka 1997 jamaa alioa nami niliona mwaka 1999 kwa kuwa tulikuwa na familia ikabidi kila mtu kuendelea na maisha yake japo mara nyingi huwa tunawasikliana na kushauriana mambo mbalimbali ya kimaisha.

Jamaa aliendelea kiuchumi na kufikia hatua ya kumiliki malori 10 yaliyokuwa yanabeba/safirisha mizigo toka Bandari ya Dar kwenda Zambia, Kongo na nchi nyingine za jirani. Baada ya kutajirika, akaanza tabia ya Umalaya.

Changamoto kubwa aliyokuwa nayo ni kutembea na wanawake wa kawaida yaani wasio wa hadhi yake. Ki kawaida, kwa mwanaume jama umeshindwa kutulia na mkeo. Basi tafuta mwanamke mwenye hadhi sio kuhangaika na wanawake wasio na kipato. Hii ilipelekea kuanguka kiuchumi kwani wanawake waliona ana mali so wakawa wanazaa naye. Sasa ana watoto 15 kwa wanawake 4 tofauti. Yule wa kwanza ana watoto naye wawili tu ila haonwengine ni wanawake wa Kiswahili wa pale Morogoro.

Hata kama dini yake inamruhusu, hakuna mwanamke anayekubali kuolewa mitara na hili alinishirikisha mwenyewe kuwa alishauriwa na shehe mmoja wa BAKWATA Morogoro kuwa anatakiwa amroge nankumshika akili mke yule wa mwanzo ili akubali aone mwanamke mwingine.

Ni kweli alifanikiwa kumshughulikia yule mama wa kichaga kwani amekuwa zumbukuku japo anasema yule mama hajakubali jamaa aone mwanamke mwingine ila yule mama hajitambui na anafanya vitu vya ajabu sana.

Sasa hivi, jamaa kafirisika na amekaa ndani analia tu. Wanawake wamemfirisi kwani alioa mwanamke mmoja polisi na mwingine mama wa nyumbani tu. Hao wote walitaka awajengee nyumba na jamaa aliniambia aliwanunulia kiwanja Morogoro Mjini na kuwajengea nyumba kwa gharama za milioni 60 kila mmoja. Kingine kilichomfanya aukwae umaskini ni gharama kubwa ya ada kwa watoto kwani analipa ada si chini ya milioni 30 kwa mwaka kwa shule asomeshazo watoto na kuna binti mwingine alizaa nje anamsomesha Law school.

Alinieleza hayo akaniomba ushauri na msaada ni kwa namna gani atalipa mkopo wa Tsh 150M toka CRDB ambao aliuchukua kama mkopo wa Kilimo na huko shambani kaambulia gunia 6000 tu za Mpunga ambazo nyingi ni madeni ya watu wengine waliomkopesha.

Enyi wanaume wenzangu, tulieni na wake zenu. Mnaharibu familia na ndoto za watoto wenu. Leo anampeleka mwanaye kweli awe Polisi? Inasikitisha sana.

Mi mwenyewe pamoja na kuuza kwangu madafu, siwezi na sitaruhusu mwanangu awe Polisi.

Dah Inasikitisha sana. Umalaya mbaya sana. Mungu atusaidie.
Kwa hiyo hutaki mwanao awe hata IGP?
Na hapo umemhukumu rafiki yako kuwa ni malaya kwa vile tu kazalisha wanawake watano.
Watano tu!
Ndio unamwita mwenzio malaya? Wewe haujatembea na wanawake zaidi ya 10, kwa umri ulio nao, hata kama hawajazaa?
 
Umetumwa kuijaza dunia acha au unataka ukaonane na Pdidy?
Kuna kujaza dunia na kitu uchumi wa dunia ulivyosimama saiv uspende kuropoka kwenye vitu vya mantiki pdiddy kaingiaje hapa, unataka story za kejeli za kfrwa ziletwe hapa?
Emmbu pima basi kauli,
Zaa watoto hata kumi na mkeo ila kuzaa nje ni tatizo kwa watanzania wengi nini hujaelewa hapo, mamyo wewe
 
Kwa hio wewe kwa sababu uchumi umesimama pdidy anakwambia panda ghorofani na wewe unapanda?
 
Naunga mkono hoja!!

Kwa hiyo mkuu zerominus10 na wengine,je mnapinga content ya uzi,mnampinga mleta uzi au makosa yaliyojitokeza kwenye uzi?

Wekeni msimamo wenu wazi tujue:-
1.Umalaya ni mbaya/mzuri?
2.Kuzaa zaa zaa ovyo na mwanamke yeyote ni sawa?
3.Kuzaa hata watoto Mia fresh tu?
4.Kuzaa na mwanamke mmoja tu ni sawa na kujipeleka kwa PDiddy?

ELEWEKENI!!
 
Usiharibu uzi wa mwenzako. Acha ligi zisizo na maana. Jamaa kasema umeshinda, basi achana nae tajiri.
Ni kweli lengo ni kuharibu tu uzi wa mwenzake wakati ndani ya huu uzi kuna ujumbe mkubwa kwa wengine.
Kwa kweli kuna points nyingi sana nimezinote humo.
 
Hiki kisa kimenisikitisha sana.

Kuna jamaa yangu na rafiki yangu kitambo toka 1980's kule Morogoro na tulianza biashara naye za kuuza/kuchukua Sigara kwenye treni kipindi hiko.

Mambo yakatunyookea tukaanza kufanya biashara za Mahindi kwenye mikoa ya Songea na Morogoro. Mwaka 1997 jamaa alioa nami niliona mwaka 1999 kwa kuwa tulikuwa na familia ikabidi kila mtu kuendelea na maisha yake japo mara nyingi huwa tunawasikliana na kushauriana mambo mbalimbali ya kimaisha.

Jamaa aliendelea kiuchumi na kufikia hatua ya kumiliki malori 10 yaliyokuwa yanabeba/safirisha mizigo toka Bandari ya Dar kwenda Zambia, Kongo na nchi nyingine za jirani. Baada ya kutajirika, akaanza tabia ya Umalaya.

Changamoto kubwa aliyokuwa nayo ni kutembea na wanawake wa kawaida yaani wasio wa hadhi yake. Ki kawaida, kwa mwanaume jama umeshindwa kutulia na mkeo. Basi tafuta mwanamke mwenye hadhi sio kuhangaika na wanawake wasio na kipato. Hii ilipelekea kuanguka kiuchumi kwani wanawake waliona ana mali so wakawa wanazaa naye. Sasa ana watoto 15 kwa wanawake 4 tofauti. Yule wa kwanza ana watoto naye wawili tu ila haonwengine ni wanawake wa Kiswahili wa pale Morogoro.

Hata kama dini yake inamruhusu, hakuna mwanamke anayekubali kuolewa mitara na hili alinishirikisha mwenyewe kuwa alishauriwa na shehe mmoja wa BAKWATA Morogoro kuwa anatakiwa amroge nankumshika akili mke yule wa mwanzo ili akubali aone mwanamke mwingine.

Ni kweli alifanikiwa kumshughulikia yule mama wa kichaga kwani amekuwa zumbukuku japo anasema yule mama hajakubali jamaa aone mwanamke mwingine ila yule mama hajitambui na anafanya vitu vya ajabu sana.

Sasa hivi, jamaa kafirisika na amekaa ndani analia tu. Wanawake wamemfirisi kwani alioa mwanamke mmoja polisi na mwingine mama wa nyumbani tu. Hao wote walitaka awajengee nyumba na jamaa aliniambia aliwanunulia kiwanja Morogoro Mjini na kuwajengea nyumba kwa gharama za milioni 60 kila mmoja. Kingine kilichomfanya aukwae umaskini ni gharama kubwa ya ada kwa watoto kwani analipa ada si chini ya milioni 30 kwa mwaka kwa shule asomeshazo watoto na kuna binti mwingine alizaa nje anamsomesha Law school.

Alinieleza hayo akaniomba ushauri na msaada ni kwa namna gani atalipa mkopo wa Tsh 150M toka CRDB ambao aliuchukua kama mkopo wa Kilimo na huko shambani kaambulia gunia 6000 tu za Mpunga ambazo nyingi ni madeni ya watu wengine waliomkopesha.

Enyi wanaume wenzangu, tulieni na wake zenu. Mnaharibu familia na ndoto za watoto wenu. Leo anampeleka mwanaye kweli awe Polisi? Inasikitisha sana.

Mi mwenyewe pamoja na kuuza kwangu madafu, siwezi na sitaruhusu mwanangu awe Polisi.

Dah Inasikitisha sana. Umalaya mbaya sana. Mungu atusaidie.
Kuwa Polisi kwako ni ujinga au ni jinai?

Nilitegemea utoe ushauri watu wafanye kazi halali na wasomeshe watoto wao.

Hayo ya kusema mwanangu asifanye kazi hii na hii, wakati kazi hiyo ni halali na kijana alishavuka utoto, 18 yrs+ ni kujidhihirisha ulivyo na uwezo mdogo wa kutafakari, kufikiri na kuamua!
 
Ukiwa malaya usipokuwa mjanja utaishia kubaki mikono mitupu ama la utaishia kuondoka na magonjwa ama vyote kwa pamoja. Hakuna faidia yoyote inayopatikana kwa umalaya.
 
Hakuna faida wakati unakuwa una socialize na watu tofauti tofauti
 
Back
Top Bottom