Umalaya ni mbaya sana! Ewe mwanaume mwenye familia, itunze


Tafuta kazi ya kufanya, this is very judgemental
 
Hao watoto kirundo tena kwa maisha tough tuliyonayo kipindi hiki wanakuletea faida gani wewe kama wewe?
Maisha tough kivipi mashamba mifugo ipo na elimu ni bure nayo sio ya lazima sana
 
Zinaa ni 1 ya matendo yanayo mkasirisha Mungu, lkn binadamu wanazani zambi za zinaa ni mpaka ufe ndio upate adhabu zake, kumbe ukweli ni kuwa hata kabla hujafa unaweza ukakumbana nazo hpahpa juu ya ardhi.
 
Yaap nimejifunza Jambo hapa
 
Mzee wangu wewe sio Malaya?
 
Hiki ni kitu muhimu sana. Tafuta mwanamke mwenye hadhi kama umeshavuka kiwango fulani cha elimu na uchumi. Pia hata kama unachepuka, weka mbali mchepuo wako na familia yako.

Inasikitisha
Hii imenigusa sana mkuu. Sina mengi ya kusema ila umesema ukweli mtupu, kifupi hawa wanawake wa hovyo wanatumia sana ndumba so unakuwa kama zuzu marafiki zako wanabaki kukushangaa maana unakuwa haushauriki, siku akili zinakurudia unakuwa uko totally destroyed na umefirisika
 
Jamaa tulianza naye biashara miaka hiyo pamoja na akina Brasto Makundi yule mwenye gari za BM pamoja na kaka yake ambaye ana ukwasi mkubwa kwa sasa.

Yeye akajiingiza kwenye umalaya usio.na maana. Haambiliki wala hashauriki. Sio kwa Baba yake wala kaka yake wala wadogo zake au sisi rafiki zake. Tumemuacha tunamuangalia ila kilichoniuma ni kushindwa kuwatengenezea watoto wake maisha ya baadaye kwa ajili ya wanawake.

Wakati dunia ya sasa tunawaza kupeleka watu kuishi Mars pamoja na mwezini na tukiwa tunawaza competition ijayo kwa watoto wetu, we mwanao anaenda kuwa mlinzi wa mtoto wa Mwigulu Nchemba na Abdul Samia.

Inasikitisha sana.
 
Zinaa ni 1 ya matendo yanayo mkasirisha Mungu, lkn binadamu wanazani zambi za zinaa ni mpaka ufe ndio upate adhabu zake, kumbe ukweli ni kuwa hata kabla hujafa unaweza ukakumbana nazo hpahpa juu ya ardhi.
Ni kweli. Unaleta mikosi, umaskini na magonjwa kwenye familia. Mungu awasaidie vijana.
 
Ila ingetakiwa mumsaidie na siyo kumwacha, mara nyingi anakuwa siyo yeye. Ukiishiwa ndiyo akili zinarudi maana wanakukwamisha hawakutaki tena kwani huna faida unabaki kuwa mzigo kwa mkeo na familia kwa ujumla
 
Inawezekana nimekukwaza, nisamehe katika hilo ila katika kitu ambacho sitaruhusu wanangu kufanya hata akiwa na miaka 100 ni kazi za kuajiriwa.

Kwanza Baba nimepambana kwa ajili yao. Nina watoto 4 na mkubwa wao anamaliza Muhimbili degree yake. Wengine wapo Advance na O Level wa mwisho ni Primary. Wote nawasomesha kama baba yao. Ndoto yangu ni watoto wawe na maisha mazuri kwa kujiamini.

Huyo wa Muhimbili nitamfungulia duka la madawa ya kibinadamu au kahospitali kadogo au kamaabara kadogo. Mtaji wa 10-20M au hata 50m kama mzazi sikosi ila sio awe askari polisi, magereza au JWTZ, ualimu n.k

Hizo ni kazi za watorwatoto a maskini. Samahani kwa hilo.
 
Enyi wanaume wenzangu, tulieni na wake zenu. Mnaharibu familia na ndoto za watoto wenu. Leo anampeleka mwanaye kweli awe Polisi? Inasikitisha sana.
Hata uwe na pesa kiasi gani ukishajiingiza kwenye Umalaya zitaisha tu.

Obama hakuwa mjinga kubaki na Mke mmoja pamoja na kwamba ana Influence of Money and Power.

Kinyume na hapo pesa zitaisha na utakapolazimisha ubaki juu utajikuta unaenda kwa Pididy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…