Umalaya ni mbaya sana! Ewe mwanaume mwenye familia, itunze

Umalaya ni mbaya sana! Ewe mwanaume mwenye familia, itunze

Nini maana ya kimwenje?😀😀😀 nafikiri nimekosea kuku quote mkuu. Sikumaanisha hivyo. Niwie radhi kwa hilo mkuu.
unalijua kuti la mnazi? sasa hua likikatwa sawa kuna vile vijani vya mwisho juu huku vikibakia hua havina kazi ndio huitwa kimwenje
 
Mnapenda kutusingizia wanawake,hayo malori kawahonga hao wanawake??watu wana mi hela yao ya manyokanyoka wakishindwa masharti mahela yote yanaondoka nyie mnasema wanawake...
Kama biashara ziliwapa utajiri kiasi hicho wewe binafsi ulinunua malori mangapi?
 
Mnapenda kutusingizia wanawake,hayo malori kawahonga hao wanawake??watu wana mi hela yao ya manyokanyoka wakishindwa masharti mahela yote yanaondoka nyie mnasema wanawake...
Kama biashara ziliwapa utajiri kiasi hicho wewe binafsi ulinunua malori mangapi?
Umalaya na kuendekeza wanawake ndio chanzo cha anguko la jamaa. Sasa analia tu ndani.

Mi sina malori, mi na madafu tu ninayoyauza hapa Ikulu. Karibu uniungishe dafu basi.
 
Hiki kisa kimenisikitisha sana.

Kuna jamaa yangu na rafiki yangu kitambo toka 1980's kule Morogoro na tulianza biashara naye za kuuza/kuchukua Sigara kwenye treni kipindi hiko.

Mambo yakatunyookea tukaanza kufanya biashara za Mahindi kwenye mikoa ya Songea na Morogoro. Mwaka 1997 jamaa alioa nami niliona mwaka 1999 kwa kuwa tulikuwa na familia ikabidi kila mtu kuendelea na maisha yake japo mara nyingi huwa tunawasikliana na kushauriana mambo mbalimbali ya kimaisha.

Jamaa aliendelea kiuchumi na kufikia hatua ya kumiliki malori 10 yaliyokuwa yanabeba/safirisha mizigo toka Bandari ya Dar kwenda Zambia, Kongo na nchi nyingine za jirani. Baada ya kutajirika, akaanza tabia ya Umalaya.

Changamoto kubwa aliyokuwa nayo ni kutembea na wanawake wa kawaida yaani wasio wa hadhi yake. Ki kawaida, kwa mwanaume jama umeshindwa kutulia na mkeo. Basi tafuta mwanamke mwenye hadhi sio kuhangaika na wanawake wasio na kipato. Hii ilipelekea kuanguka kiuchumi kwani wanawake waliona ana mali so wakawa wanazaa naye. Sasa ana watoto 15 kwa wanawake 4 tofauti. Yule wa kwanza ana watoto naye wawili tu ila haonwengine ni wanawake wa Kiswahili wa pale Morogoro.

Hata kama dini yake inamruhusu, hakuna mwanamke anayekubali kuolewa mitara na hili alinishirikisha mwenyewe kuwa alishauriwa na shehe mmoja wa BAKWATA Morogoro kuwa anatakiwa amroge nankumshika akili mke yule wa mwanzo ili akubali aone mwanamke mwingine.

Ni kweli alifanikiwa kumshughulikia yule mama wa kichaga kwani amekuwa zumbukuku japo anasema yule mama hajakubali jamaa aone mwanamke mwingine ila yule mama hajitambui na anafanya vitu vya ajabu sana.

Sasa hivi, jamaa kafirisika na amekaa ndani analia tu. Wanawake wamemfirisi kwani alioa mwanamke mmoja polisi na mwingine mama wa nyumbani tu. Hao wote walitaka awajengee nyumba na jamaa aliniambia aliwanunulia kiwanja Morogoro Mjini na kuwajengea nyumba kwa gharama za milioni 60 kila mmoja. Kingine kilichomfanya aukwae umaskini ni gharama kubwa ya ada kwa watoto kwani analipa ada si chini ya milioni 30 kwa mwaka kwa shule asomeshazo watoto na kuna binti mwingine alizaa nje anamsomesha Law school.

Alinieleza hayo akaniomba ushauri na msaada ni kwa namna gani atalipa mkopo wa Tsh 150M toka CRDB ambao aliuchukua kama mkopo wa Kilimo na huko shambani kaambulia gunia 6000 tu za Mpunga ambazo nyingi ni madeni ya watu wengine waliomkopesha.

Enyi wanaume wenzangu, tulieni na wake zenu. Mnaharibu familia na ndoto za watoto wenu. Leo anampeleka mwanaye kweli awe Polisi? Inasikitisha sana.

Mi mwenyewe pamoja na kuuza kwangu madafu, siwezi na sitaruhusu mwanangu awe Polisi.

Dah Inasikitisha sana. Umalaya mbaya sana. Mungu atusaidie.
Habari za huko mkoa wa "Songea"?🤔
 
Umalaya na kuendekeza wanawake ndio chanzo cha anguko la jamaa. Sasa analia tu ndani.

Mi sina malori, mi na madafu tu ninayoyauza hapa Ikulu. Karibu uniungishe dafu basi.
Mwambie akupeleke makete kuna mtu anaitwa Mwakipande,utapata Caroline na wewe😉😉
 
Mwenzako ana watoto 15+1 na wote anasomesha hajawatelekeza halafu unamcheka aisee! You can't be serious

Halafu mbona hueleweki kuhusu hao wanawake? Mara useme kawaoa mara uwaite malaya mara... Sikia wewe muuza madafu feki, ikiwa hii stori yako ni ya kweli HUYO JAMAA KAMA HAO WANAWAKE ALIOA BASI NAMPA BIG UP SANA NA MOLA AMUONGOZE INSHAALLAAH

Mjinga ni huyo aliyeshauri uchawi!
 
Wewe mlengo wako sio tu kushuka kwa maisha ya rafiki yako halafu wewe sio rafiki kwa maelezo yako wewe ni adui wa huyo jamaa na hapo ulipo unafurahia anguko lake nyoka kabisa wewe
Atakuwa mchawi huyu Muuza Madafu Wanaume Hatuwi Na Chuki za Ajabu Ajabu Amefilisika ni yeye wewe inakuuma nini? Au alikuwa anakuhonga?
 
Ila sio kwa kushindana na uchi mkuu. Hata mi nitaweza filisika ila sitafilisiwa na tundu la mwanamke. Hayo mambo yana umri ndugu yangu. Kwenye miaka yetu hii 50's unasumbuliwa na wanawake tena mwanamke Polisi mwenye miaka 30's na mvuta bangi? Tulimshauri sana ila dah.

Inasikitisha, byee. Ngoja nikapambanie wanangu.
Polisi walikufanya nini mbona unawachukia sana?
 
Au alipigwa dawa maana sikuhizi hawakulogi ufe, unarogewa kitu kitakachomaliza hela yako.
Ili ukishafilisika uteseke wakikushuhudia, ila qum....ah zimewaangusha wanaume wengi sana, kuna mzee anaumwa sana saiv lakini hata watoto hawako organized sababu ni alizaa kwa wamama 6 tofauti, mke alienae ni yule wa kumtunza uzeeni, hajali kitu, basi ni mateso tu anatia huruma sana ila unaambiwa enzi zake hizo jeuri zake sio za kitoto pesa ilikuwepo mke alihenya vilivyo ikafikia hatua yakamshinda na walizaa watoto zaidi ya 10😢😢
 
Back
Top Bottom