Umasikini ni matokeo ya fikra na sio matokeo ya mazingira

Masikini Wana smartphone lakini majority wanazimiss use zaidi wanaangalia visivyotija kwao zaidi ya kufurahisha ubongo tu via smartphone kuna masoko ya kuziona fursa
 
Kwa kigezo cha kumudu kupata mahitaji yake na ya ziada, unamaanisha Chakula, mavazi na malazi?
Mahitaji yanategemeana na kipato na mazingira.

Lazima tukubali kuwa mazingira huathiri fikra na hivyo hali ya kiuchumi kwa ujumla! Kuna levels za utajiri kulingana na mazingira, huwezi kuwa bilionea wa Africa Kama biashara yako imebase nanjilinji huko
 
Asilimia kubwa ya matajiri wana conglomerated company. Wengi wanauza teknolojia, mafuta, madini.
Kwa afrika Sina hakika mazingira ni secured kias gan katika angle hizo mana sekta hizo dominated na foreigners
 
Nakazia hapo kwenye umaskini ni laana, Aseeh umaskini ni laana
 
Jamani😃😃😃
 
Mtizamo wako ni sahihi na lakini pia sio sahihi. Na huu ndio mtizamo wangu.

Mazingira yanaweza kuwa sababu ya kushindwa kubarikiwa au kufanikiwa. Kuna mazingira yanakufunga na kukuzuia kupiga hatua.

Kwa wasomaji wa Biblia na waamini wa Yesu Kristo mtakubaliana nami kua.

Mungu alipotaka kumbariki Abrahamu alimuhamisha kutoka Nchi ya wazazi wake au mahali alikozaliwa.

Isaka pia naye ilikua hivyo hivyo sawa na Yakobo wote Mungu aliwaagiza kuondoka mahali walipokuwepo na ndipo walipopata mafanikio yao.

Au kwa nini Yusuph alienda kubarikiwa Misri na si kule nyumbani kwa Baba yake Yakobo alikozaliwa? Au pia kwa nini Israeli taifa teule la Mungu wasifanikiwe kulekule Misri ila iliwabidi waondoke waende Nchi ya ahadi ndio wabarikiwe?

Mkuu suala la kimafanikio kwanza linaanzia Rohoni. Na nikuambie Mazingira yanaweza kua kikwazo kikubwa sana katika mafanikio ya Mtu.

Kifupi hili ni somo pana sana….
 

Unataka ufanye biashara au investment na savings zako?hapo hakuna utajiri,wewe sio risktaker
 
Bila nyota au kibali utoboi,utajiri uanzia rohoni.
pesa ni roho ndio maana Ina nguvu ya kufanya jambo.
Ukiitwa tu Dili la Hela lazima furaha yako iongzeke

Kwani nyota au kibali ni nini?Tunazaliwa wote na nyota Vipi wengine wawe na nyota wengine wasiwe na nyota?
 
Sijabase kwenye ubilionea hio ni another factor,base kwenye basic needs na ziada
 
Sasa Nina swali hapo: Naona watu wengi wanafanikiwa Kwa Shetani na majini , je mtu akimtumainia Mwenyezi Mungu tu bila kushirikisha chochote anaweza toboa?

Anaweza kutoboa imani yake ikiwa dhahiri
Watu wanao amini shetani na majini wengi wana imani kali kuliko wanao amini Mungu
Kumbuka Lakini ni imani+matendo sio imani peke yake
 
Unatumia milioni moja kulima shamba la matikitiki karibia heka 5 halafu unauza laki mbili- soko hamna, hapa tunasema shida ni nini?

Hahah hapa sababu ni nyingi
Hujatupa maelezo vizuri
Ila si unatakiwa kujua msimu upi una demand ya zao lako hivyo kilimo chako kiendane na demand
Pia kwa milion moja heka tano nina wasiwasi na hicho kilimo,hapo mazao yako yanaweza yasiwe na ubora
Japo hujaelezea vizuri ila kwa haraka tu shida ni wewe hapo jipange upya fanya utafiti ikibidi
 
Nyie, msiwaonage Watu wamefanikiwa mkadhani Ni rahisi, kuwa tajiri Ni shughuli pevu Sana watu wanapitiaga mengi Sana.

Kufanya kazi kwa bidii pekee hakuwezi mfanya mtu awe tajiri maana Kama ingekuwa hivo watu wengi wangekuwa Ni matajiri.

Kwenye kila utajiri nyuma Yake Kuna uchafu ambao umefunikwa na kaniki nyeusi usionekane.
 
Umasikini ni matokeo ya akili kufungwa yaani kutoruhusu au kutafuta taarifa mpya zitakazokusaidia kuyachakata mazingira yako uone fursa.
ni rahisi kwa mtoto wa tajiri kuwa masikini case study zipo nyingi.
toa data
 

Ukiendelea kuamini hivi subconscious yako Inakariri inamaana wewe kufanikiwa kwako itabidi uwe mshirikina ndio imani yako ilipo lala
 
subjective vs objective
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…