Umasikini wa Watanzania chanzo chake ni kupenda kujenga nyumba ya kuishi kwanza badala ya kuanzisha biashara

Umasikini wa Watanzania chanzo chake ni kupenda kujenga nyumba ya kuishi kwanza badala ya kuanzisha biashara

Baba hapo kwenye asset na liability umewapiga watu kamba [emoji16][emoji16][emoji16].
Jengo lisilo generate income ni liability sababu linakusubiri upate income sehemu zingine Litafune income yako pia gari ya kutembelea nyumba ya kulala na kuamka zote ni liability zinatafuna tu income toka other sources unapata ni wadai wako kwenye personal finance nyumba ya kulala na kuamka na gari ya kutembelea sio Asset!!! Don't just think of company financial reports prepare your own personal financial reports kukariri !!! Prepare your own personal financial reports !!! Sio unakomaa tu za kampuni jiongeze
 
Hata hao wahindi kwao wana nyumba wamejenga. Huwezi kuwa unaishi say Afrika Kusini ukafikiria kujenga huko. Utapanga na kufanya biashara au shughuli yoyote halali. Hii dhana ndio ipo kwa wahindi, hapa wahindi sio kwao. Kwa baadhi wenye fedha nyingi sana uwa wanajenga maeneo kama masaki, upanga n.k na wengi uwa wananunua apartment.

Halafu kujenga sio umasikini, kumiliki nyumba ni jambo bora sana katika maisha maana nyumba ni kitu ambacho kinakupa mengi sana ikiwepo kukupunguzia gharama za kodi, kukuondolea stress za kutokuwa na kwako na pia hata ukipata tatizo la kiuchumi unakuwa na pa kuanzia.

Nyumba ni kitu ambacho hata ukiondoka duniani ghafla familia yako inakuwa na sehemu ya kuanzia kuliko ukiwa huna nyumba.

Nyumba ni muhimu katika ukuaji wa miji na Taifa kwa ujumla. Unavyoona nje yale majengo ni kwamba watu wamewekeza ndio maana kunapendeza. Na sisi tujenge majengo kukuza nchi yetu. Tuachane na wahindi wale hapa sio kwao ndio maana hawajengi. Tena si wahindi tu hata wazungu hawajengi hapa kwa kuwa si kwao hapa watachuma tu ila kujenga wataenda jenga kwao
Point.
 
Hakuna watu wanapenda kujenga nyumba za kuishi duniani kama Watanzania.

Ndoto kuu ya kwanza ya Mtanzania yeyote ngozi nyeusi ni kuwa na kwake hivyo akipenda vihela huvipeleka site kujenga nyumba ya kuishi hapa ndio siri ya umasikini wa Watanzania ngozi nyeusi kuanzia.

Wenzetu Wahindi hupanga hata miaka arobaini pesa zake akiweka na kukuza biashara yake. Wazo lake la kwanza huwa nikipata pesa natafuta nyumba ya bei rahisi ya kupanga halafu hela inayobaki naanzisha biashara. Wote mashahidi Wahindi matajiri hasa lakini maisha yote wanaishi nyumba za kupanga za National Housing. Sisi Waswahili tunashindana kujenga nyumba za kuishi za kulala na kuamka za mamilioni.

Waswahili hatushindani kwenye uwekezaji tunashindana kwenye nani kujenga nyumba kali kuliko mwingine! Hata waswahili wakiudhiana wakianza kutukanana isi mojawapo huwa kwani wewe una nini? Mimi Nina kwangu nimejenga nyumba za kuishi moja hapa mjini ingine kijijini

Nchi ziliizoendelea watu huwaza kuwekeza kwanza kama ndoto ya kwanza akipata pesa.

Hapa ndio siri ya umaskini wa waswahili ilipo.ndoto za kwanza ni kwenye vitu visivyozalisha pesa hasa nyumba ya kulala na kuamka.
Point.
 
Kodi ya nyumba ni kati ya vitu vinavyotafuna mtaji wa biashara kuliko maelezo..umepanga nyumba ya wastani ya laki nne kila mwezi. Kutoa kiasi hiki kama kodi ya nyumba toka kwenye pato la biashara ni pesa nyingi sana. Usipokuwa makini unaweza ukayumba hata kibiashara. Kumbuka bado biashara ina gharama zake za uendeshaji ikiwemo kodi ya ofisi, mishahara, etc.

Usipo kuwa makini utajikuta milioni inachomoka kila mwezi kwaajili ya kodi pekee.....haina afya kibiashara.

Kingine ni swala la kukopesheka na taasisi za fedha. Biashara haiwezi kusimama bila mikopo, na hakuna mkopo bila dhamana. Siku hizi hawapokei tena eneo lisiloendelezwa kama dhamana ya mkopo. Wanahitaji nyumba. Huna nyumba utatumia muda mwingi sana kusimama kibiashara.

Vijana jengeni....nyumba ni asset.
Kijana mtoa mada inaonyesha bado ni mwanafunzi au pengine ni graduate wa mwaka jana. Hana biashara wala hajui gharama za ku rent nyumba kwaajili ya familia.
 
kumbuka mahitaji muhimu matatu katika maisha "nyumba "ni mojawapo. Mtoa uzi sikuelewi.
 
Asset ni property that generates income wewe utakuwa mhasibu uliyesoma kwa kukariri hata kama una CPA unarekodi hata jengo bovu kama Asset wachumi hakuna ujinga wenu huo wa kujua asset ni any property hata kama ni useless property wahasibu huripoti kama Asset wajinga wakubwa ndio maana sio rahihisi kukuta managing director wa kampuni mhasibu ni wajinga fulani hivi

Kiuchumi Liability is any property that does not produce income wajinga wahasibu liability ni madeni unayodaiwa!!! Kwa wahasibu wajinga tena wenye CPA nyumba ya kulala na kuamka ni Asset!!!! Ina generate income gani ? Ndio maana mhasibu akitengeneza hesabu zake zinatakiwa zipelekwe kwa wachumi wanaojua kufanua analyisis

Wahasibu ni makarani tu wa financial data
Mkuu hizi definition za asset na liability umenukuu kutoka conceptual framework gani ya uhasibu?
 
Hakuna watu wanapenda kujenga nyumba za kuishi duniani kama Watanzania.

Ndoto kuu ya kwanza ya Mtanzania yeyote ngozi nyeusi ni kuwa na kwake hivyo akipenda vihela huvipeleka site kujenga nyumba ya kuishi hapa ndio siri ya umasikini wa Watanzania ngozi nyeusi kuanzia.

Wenzetu Wahindi hupanga hata miaka arobaini pesa zake akiweka na kukuza biashara yake. Wazo lake la kwanza huwa nikipata pesa natafuta nyumba ya bei rahisi ya kupanga halafu hela inayobaki naanzisha biashara. Wote mashahidi Wahindi matajiri hasa lakini maisha yote wanaishi nyumba za kupanga za National Housing. Sisi Waswahili tunashindana kujenga nyumba za kuishi za kulala na kuamka za mamilioni.

Waswahili hatushindani kwenye uwekezaji tunashindana kwenye nani kujenga nyumba kali kuliko mwingine! Hata waswahili wakiudhiana wakianza kutukanana isi mojawapo huwa kwani wewe una nini? Mimi Nina kwangu nimejenga nyumba za kuishi moja hapa mjini ingine kijijini

Nchi ziliizoendelea watu huwaza kuwekeza kwanza kama ndoto ya kwanza akipata pesa.

Hapa ndio siri ya umaskini wa waswahili ilipo.ndoto za kwanza ni kwenye vitu visivyozalisha pesa hasa nyumba ya kulala na kuamka.
Una akili ndefu sana mkuu, kuna ndugu zangu huwa nakosana nao sababu ya hii tabia ya kukusanya hela na kuzitupa ardhini kwa kigezo cha nyumba kwanza ilihal wahindi vizazi na vizazi wamepanga kariakoo na wana hela kuliko sisi wakimbilia majumba
 
Hata hao wahindi kwao wana nyumba wamejenga. Huwezi kuwa unaishi say Afrika Kusini ukafikiria kujenga huko. Utapanga na kufanya biashara au shughuli yoyote halali. Hii dhana ndio ipo kwa wahindi, hapa wahindi sio kwao. Kwa baadhi wenye fedha nyingi sana uwa wanajenga maeneo kama masaki, upanga n.k na wengi uwa wananunua apartment.

Halafu kujenga sio umasikini, kumiliki nyumba ni jambo bora sana katika maisha maana nyumba ni kitu ambacho kinakupa mengi sana ikiwepo kukupunguzia gharama za kodi, kukuondolea stress za kutokuwa na kwako na pia hata ukipata tatizo la kiuchumi unakuwa na pa kuanzia.

Nyumba ni kitu ambacho hata ukiondoka duniani ghafla familia yako inakuwa na sehemu ya kuanzia kuliko ukiwa huna nyumba.

Nyumba ni muhimu katika ukuaji wa miji na Taifa kwa ujumla. Unavyoona nje yale majengo ni kwamba watu wamewekeza ndio maana kunapendeza. Na sisi tujenge majengo kukuza nchi yetu. Tuachane na wahindi wale hapa sio kwao ndio maana hawajengi. Tena si wahindi tu hata wazungu hawajengi hapa kwa kuwa si kwao hapa watachuma tu ila kujenga wataenda jenga kwao
Kwani mkuu kama una biashara, hip biashara so itaendelea kulea familia.Kama unanyumba ukfa familia itaanza kuyumba hela za matumizi.Jambo la kwanza duniani ni kula,kuvaa mwisho kulala.kwa nini tusijenge misingi ya uhakila wa kula kabla ya kulala.Kama hujala utahesabu kenchi mpaka asubuhi.
 
Mkuu hizi definition za asset na liability umenukuu kutoka conceptual framework gani ya uhasibu?
Mkuu hata mm naamini anavyoamini huyu chief ila hakuna uhasibu unaofundisha hivyo.....hakuna mtaala unaotaja asset km mali inayogenerate income ila tu hyo ni applicable zaidi kwa wajasiriamali na nafikiri muasisi wa hii kitu ni Robert Kiyosaki ktk kitabu chake cha RICH DAD POOR DAD
 
Inaanza kwanza shughuli itakayokuingizia kipato maana nyumba inajengwa kwa hela ambazo umeshachuma na zinaendelea kuingia. Hakikisha kabla hujafika 40 au watoto hawajaanza sekondari uwe na kwako otherwise itasumbua sana kufanikiwa
Exactly...mada ileweke hvyo wadau msitumie nguvu kubwa kama ww una 8ml jenga patapo kustir na inayobaki anza Biashara
 
Jengo lisilo generate income ni liability sababu linakusubiri upate income sehemu zingine Litafune income yako pia gari ya kutembelea nyumba ya kulala na kuamka zote ni liability zinatafuna tu income toka other sources unapata ni wadai wako kwenye personal finance nyumba ya kulala na kuamka na gari ya kutembelea sio Asset!!! Don't just think of company financial reports prepare your own personal financial reports kukariri !!! Prepare your own personal financial reports !!! Sio unakomaa tu za kampuni jiongeze

Mkuu an asset kitafsiri kwa maana ya present economic resources zenye potential ya economic benefits. Economic benefits haziko limited to income tu, kuna savings hapo n.k

Na hiyo tafsiri ya asset haina exceptions zozote.

Whether ni personal asset au corporate asset, bado asset inabakia na tafsiri ile ile.

Whether ni personal financial report au corporate financial report, zote zinajumuisha asset zenye tafsiri ile ile.

Whether ni personal asset au corporate asset zote lazima zihudumiwe ili ziendelee kusapoti uzalishaji.

Establishing kwamba personal asset zinakula income huenda katika muktadha wa pale zinapohudumiwa in terms of improvement, repair, maintenance and any other capital and operating cost, this does not justify kuwa sio an asset hivyo basi ni liability.

Asset ni liability to the extent that, which source of finance was used to acquire such an asset.

Liability of an asset haiwi determined na whether hiyo asset inakutia hasara ama laah!

Muamuzi ni chanzo cha mapato(internal or external) ulichotumia kupata asset husika.

Pia lazima tuelewe hakuna asset isiyo na potential economic benefit. Ila kuna uwezekano wa economic benefits kuzidiwa na gharama ya kununua na kuendesha asset.

Mtu anaweza kuwa na mali binafsi lakini inasapoti uzalishaji wake au ana save significantly kuliko ambavyo angekuwa anatumia usafiri wa umma au amepanga.

Cha kuzingatia kabla ya kununua asset fanya cost benefit analysis ya asset husika then uamue kununua.
 
Mkuu hizi definition za asset na liability umenukuu kutoka conceptual framework gani ya uhasibu?
SIO CONCEPT YA KIUHASIBU NI YA KIUCHUMI

Mhasibu hata gari bovu liliolokuwa grounded kwenye vitabu vyake anaripoti kama ASSET!!!!!!!!!!
 
Tusipangiane ujue.
Lakini mkuu ujue tunafanya vitu vinavyo tupa amani na heshima. Na ndio maana ng'ombe kwa mfugaji ni kitu cha thamani wakati kwa mkulima ni nonsonse
 
SIO CONCEPT YA KIUHASIBU NI YA KIUCHUMI

Mhasibu hata gari bovu liliolokuwa grounded kwenye vitabu vyake anaripoti kama ASSET!!!!!!!!!!
According to accounting standard, ukiacha asset ya land na building, asset zingine kama magari, mashine n.k huwa zinashuka thamani, na standard inataka huku kushuka kwa thamani impact yake ionyeshwe kwenye balance ya asset.

Na asset ikifika point ya kuwa useless ina kuwa derecognized kwa maana ya kufutwa kwenye list ya asset zinazomilikiwa institution husika.

Kama kuna muhasibu ana recognize asset isiyo na thamani ni matatizo yake binafsi, lakn sio kweli accounting standard inaruhusu.
 
Hakuna mtu asiyependa kuwa na kwake,hao wahindi wangekuwa wazawa wangejenga tu fatilia wahindi wote wenye asili ya Tz wana nyumba zao,hivi kwa wenye nyumba wa Nchi ifike January anataka kodi yake wewe unataka ukamlipie mtoto ada atakuelewa..? Watu wanajenga kwanza awe huru na kukimbizana na kelele za wenye nyumba zisizokuwa na maana yoyote.. Sasa mimi nipo kwenye hatua ya rinta then nitafungua bness...
 
Kingine nenda benki kaombe mkopo waambie hauna nyumba ila una bness ya milioni100 kama huo mkopo watakupa kwa sababu gani..? Wanajua bness inaweza ikaporomoka na wakaingia deni ila ukiwa na nyumba yenye thamani hiyo watakupa mkopo koz wanajua ukifilisika nyumba ipo kufidia deni...
 
Back
Top Bottom