Umasikini wa Watanzania chanzo chake ni kupenda kujenga nyumba ya kuishi kwanza badala ya kuanzisha biashara

Umasikini wa Watanzania chanzo chake ni kupenda kujenga nyumba ya kuishi kwanza badala ya kuanzisha biashara

Kwani mkuu kama una biashara, hip biashara so itaendelea kulea familia.Kama unanyumba ukfa familia itaanza kuyumba hela za matumizi.Jambo la kwanza duniani ni kula,kuvaa mwisho kulala.kwa nini tusijenge misingi ya uhakila wa kula kabla ya kulala.Kama hujala utahesabu kenchi mpaka asubuhi.
Ni either hujui biashara ni nini au huna akili. Either of the two.
 
Kwa hiyo akipata uhamisho huyo.mtumishi wa umma anayejitambua kila anakohamishiwa inabidi ajenge nyumba ya kuishi?
Yes, kama uwezo unaruhusu ni kujenga tu ya kwako mzee! Pia uhamisho wa siku hizi una taratibu zake sio kama miaka ya nyuma kila mkiingia mwaka mpya mnakuta barua kibao za uhamisho alafu hakuna malipo mpaka badae sana lakini siku hizi hayo mambo yamepungua hata walimu waliokuwa wakihamishwa hovyo sasa hivi wanadumu sana vituo vyao vya kazi labda wenye matatizo ya kinidhamu au ukiukwaji wa mikataba yao!
 
Una hoja. Changamoto ni ya mfumo/utamaduni mzima wa maisha yetu. Wakati unasoma, kijiji kizima kinasubiri umalize, umchukue mtoto/watoto wa kijijini uwasomeshe/uishi nao.
Kila mwezi utume pesa..
Kiasi kinachobaki ni kidogo, inakuchukua muda mrefu kukusanya mtaji.. BTW, mtaji wenyewe haukusanyiki.
Kuna mengi ya kuandika but All in all, hoja yako ina mashiko sana.
Tukiweza kufikia huko, itatusaidia mno.
Nyakati zimebadilika sana, huwezi kuchukua ndugu/jirani waje kuishi kwako Mjini ili kutafuta maisha, utakua unawapotezea muda, kwa sasa wasaidie kwenda Shule au chuo, kwani huo ndio msaasa kwa sasa. Nyakati hizo watu walikua wanafanya hivyo kwa sababu palikua hakuna shule za kutosha.
 
Sio wote hawajafanikiwa mimi nina kazi na Nina biashara Pamoja na nyumba za kupangisha. Nimeridhik
Inaelekea hujaelewa uzi, Nyumba ya kupangisha na ya kuishi ni tofauti na kuanza kujenga Nyumba ya kuishi mara tu unapoanza kazi ni makosa ambayo 99.9% wanayafanya. Ni somo gumu kulielewa kama huna taaluma ya Biashara.
 
Ni either hujui biashara ni nini au huna akili. Either of the two.
Wewe ndio huna akili, unachokiwaza wewe wenye akili waliwaza karne zilizopita. Wewe unawaza biashara kufilisika wenzio wanawaza biashara kuendelea kunawiri hata kama wamekufa. Endelea kuwaza katika negative energy utavuna unachopanda.

Yani mimi nipande heka zangu mia za minazi tuwe tuwe na wewe uliejenga bangaloo la milioni 100 kwa ajili ya usingizi. Kweli wewe una akili sana endelea hivyo hivyo nunua na Mercedes Benz upark pale kwenye uwa wa jumba lako.
 
Inaelekea hujaelewa uzi, Nyumba ya kupangisha na ya kuishi ni tofauti. na kuanza kujenga Nyumba ya kuisha mara tu unapoanza kazi ni makosa ambayo 99.9% wanayafanya. ni somo gumu kulielewa kama huna taaluma ya Biashara.
Babu zetu walijenga nyumba za kulala, baba zetu wamejenga nyumba za kulala na sisi tunaendelea kurithi akili ile ile, japo pamoja na kuona hali ngumu ya hao wazazi waliokuwa wanamiliki hizo nyumba bado tunakosa ubunifu. Huwezi sikia mtu anawaza kuanzisha kampuni au investment endelevu.

Yaani mtanzania akiugua mwaka Kwisha habari yake kwa sababu anategemea active income badala ya passive income. Ukiugua au ukafukuzwa kazi nyumba ya kulala itakulisha? Au utakuwa ombaomba.
 
Kingine nenda benki kaombe mkopo waambie hauna nyumba ila una bness ya milioni100 km huo mkopo watakupa kwa sababu gani..? Wanajua bness inaweza ikaporomoka na wakaingia deni ila ukiwa na nyumba yenye thamani hiyo watakupa mkopo koz wanajua ukifilisika nyumba ipo kufidia deni...
SI KILA MKOPAJI HUWEKA DHAMANA NYUMBA WENGINE HUTUMIA FIXED DEPOSIT ZAO KAMA DHAMANA LIJUMBA NALO LAWEZA LISIUZIKE UKIWA NA NYUMBA SIO GUARANTEE KUWA WAWEZA PEWA MKOPO
 
Kujenga sio tatizo , tatizo linakuja ni kujenga Kwa hela ya Kula , ...hiii kitu inakera Sana , unakuta mtu watoto wanakula michicha na ugali kisa Baba anadunduliza hela ya kujenga , huu ni upopoma wa Hali ya juu Sana , hela ya kujenga inakujaga Tuu unajenga Kwa step zinazoeleweka , kiwanja+ Msingi+ boma + kupaua+ madirisha na milango + rangi n.k lakn hii ya kujenga tofali mistari miwili rangi fulan mistar miwili rangi nyingine , nyumba ishabadilishiwa mafundi Zaid ya kumi kisa delay of money , mi hapana kabisa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ..Mambo ya kuforce mabaya sana
 
Mkubwa .. nakubaliana kwa [emoji817][emoji109][emoji110][emoji109]
Itoshe kusema unaupeo mkubwa mnoo... Nashindwa kuelewa wanaokupinga ..wanawaza kwa kutumia nini
 
Hakuna watu wanapenda kujenga nyumba za kuishi duniani kama Watanzania.

Ndoto kuu ya kwanza ya Mtanzania yeyote ngozi nyeusi ni kuwa na kwake hivyo akipenda vihela huvipeleka site kujenga nyumba ya kuishi hapa ndio siri ya umasikini wa Watanzania ngozi nyeusi kuanzia.

Wenzetu Wahindi hupanga hata miaka arobaini pesa zake akiweka na kukuza biashara yake. Wazo lake la kwanza huwa nikipata pesa natafuta nyumba ya bei rahisi ya kupanga halafu hela inayobaki naanzisha biashara. Wote mashahidi Wahindi matajiri hasa lakini maisha yote wanaishi nyumba za kupanga za National Housing. Sisi Waswahili tunashindana kujenga nyumba za kuishi za kulala na kuamka za mamilioni.

Waswahili hatushindani kwenye uwekezaji tunashindana kwenye nani kujenga nyumba kali kuliko mwingine! Hata waswahili wakiudhiana wakianza kutukanana isi mojawapo huwa kwani wewe una nini? Mimi Nina kwangu nimejenga nyumba za kuishi moja hapa mjini ingine kijijini

Nchi ziliizoendelea watu huwaza kuwekeza kwanza kama ndoto ya kwanza akipata pesa.

Hapa ndio siri ya umaskini wa waswahili ilipo.ndoto za kwanza ni kwenye vitu visivyozalisha pesa hasa nyumba ya kulala na kuamka.

Usijidanganye kwa kuwa tu umejaribu kudunduliza hela ya kujenga ukashindwa na kuamua kujifichia kwenye kichaka cha wahindi. Suala la wahindi kutojenga Africa /Tz asili yake ni kukosa uhakika wa makazi kutokana na instability ya serikali za kiafrica yaani hawajui lini wataondolewa kama alivyofanya Iddi Amini 1970's . FYI hata hela wahindi hawaweki kwenye local banks wananunua madini na nyingine wanaweka kwenye benki zao ( BoA)

Katika maisha mahitaji muhimu ya binadamu ni Chakula, Makazi na Malazi. Ukikosa uhakika wa makazi jua wewe bado ni maskini tu, ndo maana hata ukienda kuomba mkopo bank unaulizwa mali isiyohamishika sio unafanya biashara gani.
 
Kwani mkuu kama una biashara, hip biashara so itaendelea kulea familia.Kama unanyumba ukfa familia itaanza kuyumba hela za matumizi.Jambo la kwanza duniani ni kula,kuvaa mwisho kulala.kwa nini tusijenge misingi ya uhakila wa kula kabla ya kulala.Kama hujala utahesabu kenchi mpaka asubuhi.

Pata picha umepiga pamba kali , umeshiba vizuri halafu huna pa kulala mwenye nyumba kakutolea vitu nje
 
Assets: kitu kinachoingiza pesa mfukoni mwako mfano ardhi, shamba
liability:kitu kinachutoa pesa mfukoni kwako mfano nyumba ya kuishi gari la kutembelea ni liability


source: financial IQ kutoka kwa robert kiyosaki
 
Kila binadamu ni Mfanyabiashara ?

Ushauri fanya kile unachopenda ndio maana ya kuishi (Life is for Living) kwahio sio unahangaika kutafuta sijui unachokitafuta ni kwa faida ya nani unakipata by the time unaitwa marehemu....

Kufanikiwa sio kwa kupata material things, bali kufanikisha kile ulichokianza.... / ulichokusudia....

Ingawa labda point yako ungesema kwamba nyumba / kujenga sio necessarily an asset, inaweza ikawa ni mzigo
 
[emoji16][emoji16][emoji16]acha kupotosha watu sisi dar tuna nyumba zaidi ya 4 lakin upiga kwa mwaka hela tunayo chukua si chini ya milion 16 na nikufumbue katika biashara ambayo haina hasara ni nyumba ni bonge la biashara watu kila siku wanakuwa wanahitaji kuishi maisha yao hapo kwenye nyumba bado ujaja kwenye hustle zetu wenywe huku tumetulia tunajua nyumba zipo miezi ikifika hela zinaingia ila upate mpangaji mzuri anae lipa kodi kwa wakati siyo kichefu chefu wa kupiga calenda
 
Yes, kama uwezo unaruhusu ni kujenga tu ya kwako mzee! Pia uhamisho wa siku hizi una taratibu zake sio kama miaka ya nyuma kila mkiingia mwaka mpya mnakuta barua kibao za uhamisho alafu hakuna malipo mpaka badae sana lakini siku hizi hayo mambo yamepungua hata walimu waliokuwa wakihamishwa hovyo sasa hivi wanadumu sana vituo vyao vya kazi labda wenye matatizo ya kinidhamu au ukiukwaji wa mikataba yao!
Wale mawizara waliohamia Dodoma toka Dar wakajenge nyingine Dodoma?
 
Sijui nani ameturoga sisi......mbona kila kitu tunajidharau tu
 
Najua umri wako ni mdogo na unaongea hivi kwa kuwa hujui kuwa muda ni suala la kutilia sana maanani. Unavyochelewa utakuta uwezi kujenga kabisa kwa kuwa ujenzi unahitaji timing sana.

Mie nilianza kujenga nyumba ya kawaida sana at my early 30 nyumba ya milioni kama 30 hivi na baadae nikajenga nyingine ya kama milioni 40 eneo lilikuwa kubwa 860 square meters. Baada ya hapo nilipokaribia 40 ndio nikaanza kujenga dream house ambayo imenigharimu like 250 million ambayo ndio ninaishi kwa sasa. Baada ya kuona utamu wa kodi niliamua kujenga nyumba ndogo ndogo za kisasa (vyumba viwili na sebule) maeneo mbalimbali jijini ambayo kwangu ni biashara nzuri na rahisi nakusanya kodi kwenye nyumba nyingine najenga mpya mdogo mdogo.

Kwa kukushauri usifikirie sana kujenga nyumba kubwa sana bali jenga ambayo una uwezo nayo ila akikisha iwe nzuri sana kwa ramani madirisha makubwa na isiwe fupi na unapojenga mapema hamia na kama pesa ipo ndipo ufikirie kujenga nyumba kulingana na uwezo wako kipindi hicho. Kwenye ujenzi usijifananishe na mtu. Ujenzi una awamu zake. Waliojenga kipindi cha awamu ya nne simenti elfu 11 ni tofauti na wanaojenga sasa hivi simenti elfu 17 mpk 20. Kwa sasa utateseka zaidi so ni bora ujenge unachokiweza leo.

Nimeshauri kutokana na niliyopitia mie ambayo nahisi ni njia sahihi ukilinganisha na wenzangu wengi wenye kazi na biashara kama zangu ila walikosea tu timing
Milioni 280?

It's okay..thank you[emoji120]
 
Back
Top Bottom