Iceberg9
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 24,893
- 47,768
Hakikanyumba ndio biashara yenyewe hio, tujenge nyumba tupangishe
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakikanyumba ndio biashara yenyewe hio, tujenge nyumba tupangishe
Ni either hujui biashara ni nini au huna akili. Either of the two.Kwani mkuu kama una biashara, hip biashara so itaendelea kulea familia.Kama unanyumba ukfa familia itaanza kuyumba hela za matumizi.Jambo la kwanza duniani ni kula,kuvaa mwisho kulala.kwa nini tusijenge misingi ya uhakila wa kula kabla ya kulala.Kama hujala utahesabu kenchi mpaka asubuhi.
Yes, kama uwezo unaruhusu ni kujenga tu ya kwako mzee! Pia uhamisho wa siku hizi una taratibu zake sio kama miaka ya nyuma kila mkiingia mwaka mpya mnakuta barua kibao za uhamisho alafu hakuna malipo mpaka badae sana lakini siku hizi hayo mambo yamepungua hata walimu waliokuwa wakihamishwa hovyo sasa hivi wanadumu sana vituo vyao vya kazi labda wenye matatizo ya kinidhamu au ukiukwaji wa mikataba yao!Kwa hiyo akipata uhamisho huyo.mtumishi wa umma anayejitambua kila anakohamishiwa inabidi ajenge nyumba ya kuishi?
Nyakati zimebadilika sana, huwezi kuchukua ndugu/jirani waje kuishi kwako Mjini ili kutafuta maisha, utakua unawapotezea muda, kwa sasa wasaidie kwenda Shule au chuo, kwani huo ndio msaasa kwa sasa. Nyakati hizo watu walikua wanafanya hivyo kwa sababu palikua hakuna shule za kutosha.Una hoja. Changamoto ni ya mfumo/utamaduni mzima wa maisha yetu. Wakati unasoma, kijiji kizima kinasubiri umalize, umchukue mtoto/watoto wa kijijini uwasomeshe/uishi nao.
Kila mwezi utume pesa..
Kiasi kinachobaki ni kidogo, inakuchukua muda mrefu kukusanya mtaji.. BTW, mtaji wenyewe haukusanyiki.
Kuna mengi ya kuandika but All in all, hoja yako ina mashiko sana.
Tukiweza kufikia huko, itatusaidia mno.
Inaelekea hujaelewa uzi, Nyumba ya kupangisha na ya kuishi ni tofauti na kuanza kujenga Nyumba ya kuishi mara tu unapoanza kazi ni makosa ambayo 99.9% wanayafanya. Ni somo gumu kulielewa kama huna taaluma ya Biashara.Sio wote hawajafanikiwa mimi nina kazi na Nina biashara Pamoja na nyumba za kupangisha. Nimeridhik
Wewe ndio huna akili, unachokiwaza wewe wenye akili waliwaza karne zilizopita. Wewe unawaza biashara kufilisika wenzio wanawaza biashara kuendelea kunawiri hata kama wamekufa. Endelea kuwaza katika negative energy utavuna unachopanda.Ni either hujui biashara ni nini au huna akili. Either of the two.
Babu zetu walijenga nyumba za kulala, baba zetu wamejenga nyumba za kulala na sisi tunaendelea kurithi akili ile ile, japo pamoja na kuona hali ngumu ya hao wazazi waliokuwa wanamiliki hizo nyumba bado tunakosa ubunifu. Huwezi sikia mtu anawaza kuanzisha kampuni au investment endelevu.Inaelekea hujaelewa uzi, Nyumba ya kupangisha na ya kuishi ni tofauti. na kuanza kujenga Nyumba ya kuisha mara tu unapoanza kazi ni makosa ambayo 99.9% wanayafanya. ni somo gumu kulielewa kama huna taaluma ya Biashara.
SI KILA MKOPAJI HUWEKA DHAMANA NYUMBA WENGINE HUTUMIA FIXED DEPOSIT ZAO KAMA DHAMANA LIJUMBA NALO LAWEZA LISIUZIKE UKIWA NA NYUMBA SIO GUARANTEE KUWA WAWEZA PEWA MKOPOKingine nenda benki kaombe mkopo waambie hauna nyumba ila una bness ya milioni100 km huo mkopo watakupa kwa sababu gani..? Wanajua bness inaweza ikaporomoka na wakaingia deni ila ukiwa na nyumba yenye thamani hiyo watakupa mkopo koz wanajua ukifilisika nyumba ipo kufidia deni...
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ..Mambo ya kuforce mabaya sanaKujenga sio tatizo , tatizo linakuja ni kujenga Kwa hela ya Kula , ...hiii kitu inakera Sana , unakuta mtu watoto wanakula michicha na ugali kisa Baba anadunduliza hela ya kujenga , huu ni upopoma wa Hali ya juu Sana , hela ya kujenga inakujaga Tuu unajenga Kwa step zinazoeleweka , kiwanja+ Msingi+ boma + kupaua+ madirisha na milango + rangi n.k lakn hii ya kujenga tofali mistari miwili rangi fulan mistar miwili rangi nyingine , nyumba ishabadilishiwa mafundi Zaid ya kumi kisa delay of money , mi hapana kabisa
Hakuna watu wanapenda kujenga nyumba za kuishi duniani kama Watanzania.
Ndoto kuu ya kwanza ya Mtanzania yeyote ngozi nyeusi ni kuwa na kwake hivyo akipenda vihela huvipeleka site kujenga nyumba ya kuishi hapa ndio siri ya umasikini wa Watanzania ngozi nyeusi kuanzia.
Wenzetu Wahindi hupanga hata miaka arobaini pesa zake akiweka na kukuza biashara yake. Wazo lake la kwanza huwa nikipata pesa natafuta nyumba ya bei rahisi ya kupanga halafu hela inayobaki naanzisha biashara. Wote mashahidi Wahindi matajiri hasa lakini maisha yote wanaishi nyumba za kupanga za National Housing. Sisi Waswahili tunashindana kujenga nyumba za kuishi za kulala na kuamka za mamilioni.
Waswahili hatushindani kwenye uwekezaji tunashindana kwenye nani kujenga nyumba kali kuliko mwingine! Hata waswahili wakiudhiana wakianza kutukanana isi mojawapo huwa kwani wewe una nini? Mimi Nina kwangu nimejenga nyumba za kuishi moja hapa mjini ingine kijijini
Nchi ziliizoendelea watu huwaza kuwekeza kwanza kama ndoto ya kwanza akipata pesa.
Hapa ndio siri ya umaskini wa waswahili ilipo.ndoto za kwanza ni kwenye vitu visivyozalisha pesa hasa nyumba ya kulala na kuamka.
Kwani mkuu kama una biashara, hip biashara so itaendelea kulea familia.Kama unanyumba ukfa familia itaanza kuyumba hela za matumizi.Jambo la kwanza duniani ni kula,kuvaa mwisho kulala.kwa nini tusijenge misingi ya uhakila wa kula kabla ya kulala.Kama hujala utahesabu kenchi mpaka asubuhi.
Wale mawizara waliohamia Dodoma toka Dar wakajenge nyingine Dodoma?Yes, kama uwezo unaruhusu ni kujenga tu ya kwako mzee! Pia uhamisho wa siku hizi una taratibu zake sio kama miaka ya nyuma kila mkiingia mwaka mpya mnakuta barua kibao za uhamisho alafu hakuna malipo mpaka badae sana lakini siku hizi hayo mambo yamepungua hata walimu waliokuwa wakihamishwa hovyo sasa hivi wanadumu sana vituo vyao vya kazi labda wenye matatizo ya kinidhamu au ukiukwaji wa mikataba yao!
Milioni 280?Najua umri wako ni mdogo na unaongea hivi kwa kuwa hujui kuwa muda ni suala la kutilia sana maanani. Unavyochelewa utakuta uwezi kujenga kabisa kwa kuwa ujenzi unahitaji timing sana.
Mie nilianza kujenga nyumba ya kawaida sana at my early 30 nyumba ya milioni kama 30 hivi na baadae nikajenga nyingine ya kama milioni 40 eneo lilikuwa kubwa 860 square meters. Baada ya hapo nilipokaribia 40 ndio nikaanza kujenga dream house ambayo imenigharimu like 250 million ambayo ndio ninaishi kwa sasa. Baada ya kuona utamu wa kodi niliamua kujenga nyumba ndogo ndogo za kisasa (vyumba viwili na sebule) maeneo mbalimbali jijini ambayo kwangu ni biashara nzuri na rahisi nakusanya kodi kwenye nyumba nyingine najenga mpya mdogo mdogo.
Kwa kukushauri usifikirie sana kujenga nyumba kubwa sana bali jenga ambayo una uwezo nayo ila akikisha iwe nzuri sana kwa ramani madirisha makubwa na isiwe fupi na unapojenga mapema hamia na kama pesa ipo ndipo ufikirie kujenga nyumba kulingana na uwezo wako kipindi hicho. Kwenye ujenzi usijifananishe na mtu. Ujenzi una awamu zake. Waliojenga kipindi cha awamu ya nne simenti elfu 11 ni tofauti na wanaojenga sasa hivi simenti elfu 17 mpk 20. Kwa sasa utateseka zaidi so ni bora ujenge unachokiweza leo.
Nimeshauri kutokana na niliyopitia mie ambayo nahisi ni njia sahihi ukilinganisha na wenzangu wengi wenye kazi na biashara kama zangu ila walikosea tu timing