Umasikini wetu ni wa kujichagulia. Je! Inaleta maana yoyote? Bara lenye ardhi yenye rutuba, idadi kubwa ya vijana, madini adimu kuwa maskini? Hapana!

Umasikini wetu ni wa kujichagulia. Je! Inaleta maana yoyote? Bara lenye ardhi yenye rutuba, idadi kubwa ya vijana, madini adimu kuwa maskini? Hapana!

Status
Not open for further replies.

Hisha Sorel

Senior Member
Joined
Dec 27, 2017
Posts
192
Reaction score
140
Je! Inaleta maana yoyote kwamba Bara lenye ardhi yenye rutuba, idadi kubwa ya vijana, madini adimu, na maji tosha; kuwa masikini zaidi ulimwenguni. Umasikini wetu ni ule wa kujichagulia, Afrika inapaswa kutafakari tena mfumo wake wa uchumi na metriki za kupima mafanikio.

Wengi wenu bado hamjanipata, kwani mnawezadhani kuwa ninawauliza: “kwanini mataifa haya wasiuze rasiliamali vao kwa faida kubwa?”

Hiyo sio lengo langu:

Fikiria: Hauwezi kula kompyuta, huwezi kunywa begi la thamani, huwezi kuzalisha machine kwa fikra na mipango peke yake. Kimsingi, vitu hivyo vyote havina thamani bila vifaa vya msingi: Ardhi, maji, watu (Kazi).

Haya ndio mahitaji ya kimsingi ambayo ndio chanzo cha utajiri wote duniani, na tunayo tele.

Sasa Kwanini sie ndio maskini zaidi?

Kwa maoni yangu, ukoloni na vipaumbele vya kiuchumi vilivyopotoka ndo sababu.

Sisi Waafrika tumechagua kufafanua mafanikio ya kiuchumi kwa masharti ya magharibi bila sababu nzuri: vitu kama: Skyscrapers, viwanja vya ndege, barabara, na kompyuta n.k., zinafafanua mtazamo wetu wa utajiri.

Hatuwezi kuzalisha chochote kati ya hivi kwa kujitegemea, hivyo tunadai msaada wa magharibi. Haishangazi pale kampuni za kigeni zinapodai pesa za kigeni, zikidai zetu hazina thamani kulingana na zao.

Kulingana na wao; madini, Ardhi, na kazi-hatarishi (hard labour) ndio kitu pekee ambacho huanza kulingana na thamani ya matunda ya kazi zao; na sie tunakubali na kutoa.

Kukataa kunajibiwa kwa kuaibishwa kama maskini (waandishi wao wa habari: BBC Swahili), kutengwa (Zimbabwe, Cuba), na hata uvamizi (Libya), kwa hivyo hofu na maslahi ya wachache (wanasiasa) husukuma kukubalika kwa faida ndogo.

Ugavi na mahitaji (supply and demand) yadaiwa kuwa sababu ya kusukuma swala hili, sasa kwanini, ukizingatia kwamba ulimwengu hauwezi kujimudu bila malighafi ya Afrika; thamani ya malighafi za nchi zake zipo chini sana.

Hatujawahi kuhoji mfumo huu wa kuthamini na ivyo tumegeuza mataifa yetu kuwa mashamba ya magharibi na uwanja wa madini.

Pointi za ziada:
Mtu anaweza kuuliza: je, vitu hivyo ambavyo umevitaja ni utajiri wa kweli?
Kwani huwezi kumtibu mtoto wako na dhahabu, ivyo mtu anahitaji dawa kutoka magharibi na maarifa yake.

Hapana! huu kwakweli ni mtego wa mzunguko (circle):

Dawa kwa mfano; angalia magonjwa tunayotibu, idadi kubwa yao ililetwa kwetu na mfumo huo huo.

Ugonjwa wa kisukari husababishwa na utumiaji wa sukari iliyosindikwa (fructose). Ikiwa Waafrika wangeshikilia lishe yao ya asili, wasingepata kisukari.

Cholera, Ebola, Typhoid, na milipuko mingine husababishwa na kuishi kwa watu katika nafasi finyu mijini. Msongamano wa watu mijini unasababishwa na watu kulazimishwa kuhama kwa idadi kubwa kwenda mijini kupata pesa kwa kuuza kazi.

Malazi duni na miundombinu husababisha wakaazi hawa wa jiji wasio na uzoefu na miji, kusambaza magonjwa ambayo wasingekuwa nayo vijijini.

Ugonjwa wa moyo, ugonjwa wa figo, ugonjwa wa ini; zote husababishwa na ulaji wa bidhaa zenye sumu: Pombe, sigara, uchafuzi wa mazingira, na kemikali zingine ni chanzo kikubwa cha shida hizi.

Simu za rununu, Magari, na vifaa vingine vya mawasiliano mara nyingi ni muhimu kwa sababu ya mpangilio wa maisha watu wanalazimishwa kuingia kwenye mchakato wa kuuza kazi yao. Kijadi, Waafrika wamekaa karibu na mahitaji yao na hivyo kuondoa hitaji la zana za mawasiliano za masafa marefu

Wakati gharama na mazingira ya kazi yanatenganisha familia, simu huwa chaguo pekee kwa mawasiliano. Wakati mtu anaishi masaa 1-2 kutoka mahali pa kazi, magari ndiyo njia pekee ya kusonga mbele.

Vitu vyote vilivyotajwa hapo juu vinahitaji uwekezaji zaidi. Dawa kwa mfano lazima iambatane na shule za matibabu, hospitali, na aina zingine za miundombinu ili kuhudumia mahitaji. Na hizi mara nyingi zinahitaji msaada wa kigeni na sarafu ya kigeni. Hii inamaanisha uuzaji zaidi wa kazi, ardhi, na maliasili nyingine.

Njia ya Mbele
Huu ni mduara, mchezo ambao hatuwezi kushinda.

Afrika inapaswa kutafakari upya mfumo wake wa uchumi kwa kutanguliza watu wake. Kuunda mfumo ambao unalinganisha kimkakati na maslahi yake.

Kwanza, watu wetu wanahitaji chakula, maji, jamii, na makazi. Hatuhitaji kampuni za magharibi kutoa hiyo kama tunayo na wingi wa vitu hivyo vyote.

Jinsi tunavyowasilisha yote hayo yanapaswa kuwa uamuzi wa ndani kwani wanajua sana hali yao.

Kimsingi, tunapaswa kuondoa mtu wa kati na kuwapa watu na jamii mahitaji yao muhimu bila kuwalazimisha kuuza kazi zao kwenye biashara ambazo hazitekelezi malengo hayo.

Vipimo vyetu vya uchumi, badala ya kuzingatia takwimu holela kama Pato la Taifa, inapaswa kulenga dhiki ya kiuchumi kwa lengo la kuitokomeza.

Ndio, tunapaswa kufanya biashara, lakini kwa uangalifu mkubwa.

Uagizaji wa bidhaa au teknolojia zisizo lazima unapaswa kuepukwa. Kimsingi, chochote kinachounda utegemezi wa muda mrefu kinapaswa kupitishwa kimkakati na mpango wa jinsi ya kutoroka matumizi yake.
 
Upvote 4
Nyie shukruni Tu Kwa vile mna mishahara minono au mna Tu viwanda twenu twa bakery..... Mnaona wenzenu wanaotaabika kama wanatania....
Mambo sio rahsi kama unavyofkria
Nani ana mshara mnono hapa?
Common peoples wana discuss uchumi tu..gafla umekuwa emotional.. grow up man.

Tume politicize uchumi.. tumepoliticize investment. Hii ndio failure namba 1.
Lazima turud nyuma tu modify economy stategies or investors watagoma kabisa kuja kuwekeza kwa policy zetu
 
Kwa mataifa ya africa ni ngumu sana kuendelea kwa pace ya dunia inavyoenda, tulishaingizwa "king" kitambo sana, karne zimepita

Hamna utajirj unaokuja kirahisi rahisi, mataifa yote tunayoyaita "tajiri" yali(na)iba rasilimali na kunyonya mataifa dhaifu. Kama ilivyo siyo rahisi mtu mmoja mmoja kuwa tajiri bila makando kando. Na kwa sasa hivi utafanyia wapi piracy, plundering n.k bila kukumbana na mikono ya wenye ulimwengu??paah unapigw kofi la sanctions

Leo hii bado tunahangaika kujenga hospital, miradi ya maji na barabara kwenye ukubwa ambao utanufaisha watu wengi, hatuwezi kwa rasilimali tulizonazo na kwa aina ya viongozi tuliowahi kuwa nao, lazima tukakope WB, world bank wanakuambia huo mradi unaweza kuombwa na kampuni yoyote kutoka katika nchi wanachama, kampuni za nje zinapata kwa kuwa zina uzoefu, hizo hela(almost 75%) zinarudi tena ulaya na unabaki kuwa na deni kubwa la kulipa kwa miaka 20.

Namna pekee ni kutafuta namna ya kukaa na wakubwa kwa adabu ila kwa misimamo, kujipendekeza, kuwapenda kinafiki, kuendelea kujijengea uwezo taratibu, kuheshimu utu wa watu, kutengeneza msingi mzuri wa uwajibikaji kwa viongozi, kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya kuwezesha uvumbuzi n.k
 
Kuwa na kila kitu ukiwa huna teknolojia ni lazima umaskini ukukute

Japani hawana mali ghafi huagiza nje na ni matajiri duniani
 
Kwa mataifa ya africa ni ngumu sana kuendelea kwa pace ya dunia inavyoenda, tulishaingizwa "king" kitambo sana, karne zimepita

Hamna utajirj unaokuja kirahisi rahisi, mataifa yote tunayoyaita "tajiri" yali(na)iba rasilimali na kunyonya mataifa dhaifu. Kama ilivyo siyo rahisi mtu mmoja mmoja kuwa tajiri bila makando kando. Na kwa sasa hivi utafanyia wapi piracy, plundering n.k bila kukumbana na mikono ya wenye ulimwengu??paah unapigw kofi la sanctions

Leo hii bado tunahangaika kujenga hospital, miradi ya maji na barabara kwenye ukubwa ambao utanufaisha watu wengi, hatuwezi kwa rasilimali tulizonazo na kwa aina ya viongozi tuliowahi kuwa nao, lazima tukakope WB, world bank wanakuambia huo mradi unaweza kuombwa na kampuni yoyote kutoka katika nchi wanachama, kampuni za nje zinapata kwa kuwa zina uzoefu, hizo hela(almost 75%) zinarudi tena ulaya na unabaki kuwa na deni kubwa la kulipa kwa miaka 20.

Namna pekee ni kutafuta namna ya kukaa na wakubwa kwa adabu ila kwa misimamo, kujipendekeza, kuwapenda kinafiki, kuendelea kujijengea uwezo taratibu, kuheshimu utu wa watu, kutengeneza msingi mzuri wa uwajibikaji kwa viongozi, kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya kuwezesha uvumbuzi n.k
Unasema points nyingi nzuri. Lakini pia kuna nchi kama UAE, Singapore, South Korea nk ambazo zimeendelea vizuri sana, lakini hawakupitia phases kama hizo za kuiba malighafi kwa nchi maskini ambazo Europe walifanya. Kwa hio inawezekana sana tu. Lakini Africa tatizo KUBWA ni viongozi na sera zao.
 
Umasikini wetu umefanyizwa makusudi kimkakati na watawala eti waweze kuwatawala watu, jiulize why wakoloni kwa mda mfupi tu walituletea maendeleo makubwa sana pande zote afya,elimu,ajira, biashara,nk lkn baada ya Uhuru tumeshindwa Hali wakoloni waliondoka afrika na mabegi yao tu KILA kitu waliacha afrika kuanzia pesa za kuanzia maisha, miradi, miundombinu,mifumo ya uhakika wa masoko lakini tumeshindwa Kila mtawala uingia kwa mbwembwe at the end huwa the same Kama watangulizi wake,wanajigeuzia kikundi cha upigaji mtawala na wapambane wake na familia zao ndo ugeuka wanufaika huku mamilioni ya waafrika wakifa kwa kukosa Panadol, wanafunzi hawana madarasa huku tukitegemea kusaidiwa hata ujenzi wa vyoo huku tukinunua ma v8 na ndege tena kwa cash.
 
Mjerumani katawala miaka 30 katuletea maendeleo makubwa Sana yaliyogusa watu wote,ccm imetawala miaka 60 hata kujenga vyoo Ni Hadi msaada.Soon tutasherekea miaka 100 ya uhuru tukiwa bado tunategemea misaada ya kujengewa vyoo.Kama watu wako wanashindwa kumudu basic needs Hali una KILA kitu kuliko hata huyo anaekupa msaada,huo uhuru una maana gani kwao.
 
JE HOTUBA ALIYOITOA RAISI TRUMP SEPTEMBER 2018 JUU YA AFRIKA KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA NI MATUSI AU NDO UKWELI?

Kumbuka wakati huu karibu nchi 133 za dunia zimekutanika ikiwemo na Tanzania ambayo imewakilishwa na waziri wa mambo ya nchi za nje.
Haya ni mambo yaliyonukuliwa katika hotuba ya Raisi Trump akiongelea bara la Afrika. Naomba usome na utoe maoni yako. Akiwa anawasuta viongozi wa Afrika, Trump anahoji kwamba:
  • lkiwa sasa imefika miaka 50 ya uhuru na bado viongozi wengi wa Afrika wameshindwa kuwa na miundo mbinu thatbiti kwa ajili ya watu wao, je hao viongozi ni binadamu kweli?
  • Anaendelea kusema kuwa ikiwa ninyi viongozi mnakalia dhahabu, almasi, mafuta na uranium na watu wenu wanakosa chakula, je ninyi viongozi wa afrika ni watu kweli?
  • Kama mnakaa kwenye madaraka na kununua silaha kutoka kwa wageni na kuua watu wenu, je ninyi ni binadamu kweli?
  • Kama mnawaza kukaa madarakani mpaka mwisho wa maisha yetu, je ninyi ni binadamu kweli?
  • Ikiwa mnatumia maliasili ya nchi zenu kwa maendeleo ya familia zenu, je ninyi ni watu kweli?
  • lwapo hamjali kuweka miundo mbinu ya afya za watu wenu na badala yake mkiugua mnaenda kutibiwa nchi za nje, Je ninyi ni binadanu kweli?
  • Mtaheshimikaje katika mataifa yenu wakati mnapiga risasi raia wenu kama vile ni mchezo?
*Amemalizia kwa kusema kuwa viongozi wa Afrika wataendelea kuwa kama wanyama hadi watakapo badili mtazamo wao na kuheshimu watu wanaowaongoza.

NB: Hadi kufikia hapo, unadhani Raisi Trump inatakiwa alaumie kutokana na tabia zake za kutukana waafrika, au labda anachosema ni kweli tukubaliane na yeye?
Una maoni gani kutokana na hotuba aliyoitoa huko kwenye kikao cha umoja wa mataifa? Hizi ni dharau za wazungu au kuna ukweli ndani yake?
 
PUTIN: AFRIKA HAITOKAA IWE HURU

"Afrika haitokaa iwe HURU. Waafrika wanawaamini Wazungu, Wamarekani na Wachina zaidi kuliko wanavyojiamini wao wenyewe....hawajiamini wao wenyewe hata kidogo.

Mzungu au mtu mweupe anafanya makosa Afrika tena makosa ya jinai ila hakuna hatua za kisheria zitakazochukuliwa dhidi yake kwa sababu mamlaka za Afrika zinatutazama sisi weupe kama miungu, jambo ambalo liko mbali sana na ukweli.

Mtu mweusi (Mwafrika) anaweza kuteswa, kunyanyaswa na hata kuuawa kinyama Ulaya lakini hakuna mamlaka yoyote ya Afrika inayoweza kuuliza wala kuhoji.

Waafrika wamejikubali na kuamini kuwa wao ni watu DHAIFU wasio na tumaini haswa linapokuja suala la kupambana na Wazungu, Wamarekani na Wachina. Mzungu, Mmarekani au Mchina anaweza kumdhalilisha, kumtukana, kumpiga na hata kumuua Mwafrika katika ardhi ya Afrika tena kwenye nchi yake au nje ya Afrika na Viongozi wa Afrika wataliona hilo na kila mmoja atajiweka kana kwamba hakuona wala kusikia.

Adui wa Mwafrika ni Mwafrika. Mwafrika mpe silaha, pesa au ahadi ya madaraka madogo tu kwa sharti moja tu la kumuua Mwafrika mwenzake, atamuua kinyama kuliko ulivyotarajia. Adui wa Mwafrika sio mzungu, sio Mmarekani wala sio mchina. Adui wa Mwafrika ni AKILI na fikra zake na ndio maana leo Wazungu, Wamarekani, Waarabu na Wachina wameitawala tena Afrika kwa kutumia dini, Elimu, uchumi, teknolojia, siasa na utamaduni.

Waafrika ni watu wanaochukiana na wasioaminiana na ndio maana Afrika haiwezi kuungana na haitokaa iungane kuwa na dola imara. Chuki ya wenyewe kwa wenyewe na utengano ndio inayowapa wakoloni wao nguvu ya kuendelea kunyonya rasilimali za Afrika."

Je unakubaliana na Rais Vladmir Putin?
Je ni kipi unaweza kuongeza kuhusu Afrika?

Quote
 
Kwa mataifa ya africa ni ngumu sana kuendelea kwa pace ya dunia inavyoenda, tulishaingizwa "king" kitambo sana, karne zimepita

Hamna utajirj unaokuja kirahisi rahisi, mataifa yote tunayoyaita "tajiri" yali(na)iba rasilimali na kunyonya mataifa dhaifu. Kama ilivyo siyo rahisi mtu mmoja mmoja kuwa tajiri bila makando kando. Na kwa sasa hivi utafanyia wapi piracy, plundering n.k bila kukumbana na mikono ya wenye ulimwengu??paah unapigw kofi la sanctions

Leo hii bado tunahangaika kujenga hospital, miradi ya maji na barabara kwenye ukubwa ambao utanufaisha watu wengi, hatuwezi kwa rasilimali tulizonazo na kwa aina ya viongozi tuliowahi kuwa nao, lazima tukakope WB, world bank wanakuambia huo mradi unaweza kuombwa na kampuni yoyote kutoka katika nchi wanachama, kampuni za nje zinapata kwa kuwa zina uzoefu, hizo hela(almost 75%) zinarudi tena ulaya na unabaki kuwa na deni kubwa la kulipa kwa miaka 20.

Namna pekee ni kutafuta namna ya kukaa na wakubwa kwa adabu ila kwa misimamo, kujipendekeza, kuwapenda kinafiki, kuendelea kujijengea uwezo taratibu, kuheshimu utu wa watu, kutengeneza msingi mzuri wa uwajibikaji kwa viongozi, kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya kuwezesha uvumbuzi n.k
Na Africa ni wachache ndio wananufaika na utajiri wa nchi...huku nchi ikiendeshwa kama ni mradi binafsi wa mtu kutekeleza yale anayoona ni sawa, pasipo kupingwa. Wakati mengi yanayofanyika yanaumiza nchi na watu wake.
 
Dreamliner moja iliyopaki ni sawa na matreka elf 10 mapya na vifaa vyake tena kwa cash, Kama ni kwa mkopo unapata trekta elf 50 za horse power 75.Trekta moja ulima heka 25 kwa siku kwa speed ya kivivu. Trekta moja utoa ajira kwa vijana 100.
So badala ya dreamliner moja iliyopaki kutoa ajira kwa watu 30 zingekuwa ni trekta zingetoa ajira milioni 5 za moja kwa moja achilia wategemezi wao.Ajira zote zilizonunulia ndege zingenunua trekta laki moja ambazo zingetoa ajira milioni 12 nchi nzima.Ndege ugusa wachache,kilimo ugusa wote.Kama Malaysia waliwekeza kwenye michikichi tu ndo wanailisha dunia mafuta ya kula na bado awajalijaza soko. Soko la mazao ya kilimo duniani ni kubwa hata KILA mtu alime tza hatutoweza kulijaza.Hela zilizotupwa kwenye ndege tilioni moja tungepata matreka laki 2 yangeajiri vijana milioni 12 zingemaliza tatizo la ajira nchini kwa kuwekeza kwenye kilimo mkakati na zingesharudi ndani ya miaka 3 tungepata pesa tosha za kigeni kukamilisha miradi yote bila kutegemea kukopa.Kupitia kilimo tu tungekuwa uchumi wa kati.Kama wakoloni wao waliweza maliza tatizo la ajira nchini why tunashindwa?Tangu Uhuru bado atujapata kiongozi sahihi mwenye uchungu anaeguswa na ugumu wa maisha ya watz,zaidi ya kuyafanya maisha yazidi kuwa magumu.Kwann watumishi wasipewe misamaha ya Kodi Ili wajinunulie magari binafsi kuliko kuwa na utitiri wa magari ya serikali ambayo hayazalishi,hayana faida ni hasara kwa mlipa Kodi V8 moja tu ni sawa na matrekta 10 mapya na jembe zake hapo ni sawa na ajira elf 1.
Tuendelee tu kuwalaumu mabeberu juu ya kushindwa kwetu aliyetupa Mali alitunyima akili. Chagua ccm chagua maendeleo chagua mitano tena ikiisha mitano tena jiandae kwa kumi tena.
 
Au hata kujenga viwanda vya KIMATAIFA. Mfano korosho, hakuna kiwanda cha kimataifa Tanzania cha kuprocess korosho. Au viwanda vya mafuta ya kupikia kikubwa na cha kimataifa etc. Serikali ina uwezo wa kuyafanya hayo KWA HELA YA KODI WANAYOIPATA. Kwa sasa kuna small scale manufacturing ya watu binafsi. Issue ya ndege ilikuwa ni investment yenye makosa sana. Tunge-invest katika vitu ambavyo vitalera ajira, na kuingizia pesa kupitia exports. VIJANA HAWANA AJIRA. Dreamliners zinaleta ajita kiasi gani kulinganisha na viwanda vikubwa?

Na hio sio shida, TATIZO NI PALE AMBAPO MTU UMEKOSEA LAKINI HAUKUBALI KWAMBA ULIKOSEA. Hapo ndio tatizo lililopo sasa hivi. Mungu awaondolee hilo tatizo viongozi wetu. WAONE WANAPOKOSEA, NA WAJIREKEBISHE. Otherwise, hali itazidi kuwa mbaya tu kwa waTz na nchi kwa ujumla.
 
Kwa mataifa ya africa ni ngumu sana kuendelea kwa pace ya dunia inavyoenda, tulishaingizwa "king" kitambo sana, karne zimepita

Hamna utajirj unaokuja kirahisi rahisi, mataifa yote tunayoyaita "tajiri" yali(na)iba rasilimali na kunyonya mataifa dhaifu. Kama ilivyo siyo rahisi mtu mmoja mmoja kuwa tajiri bila makando kando. Na kwa sasa hivi utafanyia wapi piracy, plundering n.k bila kukumbana na mikono ya wenye ulimwengu??paah unapigw kofi la sanctions

Leo hii bado tunahangaika kujenga hospital, miradi ya maji na barabara kwenye ukubwa ambao utanufaisha watu wengi, hatuwezi kwa rasilimali tulizonazo na kwa aina ya viongozi tuliowahi kuwa nao, lazima tukakope WB, world bank wanakuambia huo mradi unaweza kuombwa na kampuni yoyote kutoka katika nchi wanachama, kampuni za nje zinapata kwa kuwa zina uzoefu, hizo hela(almost 75%) zinarudi tena ulaya na unabaki kuwa na deni kubwa la kulipa kwa miaka 20.

Namna pekee ni kutafuta namna ya kukaa na wakubwa kwa adabu ila kwa misimamo, kujipendekeza, kuwapenda kinafiki, kuendelea kujijengea uwezo taratibu, kuheshimu utu wa watu, kutengeneza msingi mzuri wa uwajibikaji kwa viongozi, kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya kuwezesha uvumbuzi n.k

Njia pekee ni kubadili mifumo ya kupata uongozi, tuajiri watu wenye kuweza bila kujali race zao tuwape watuongoze.Na sio hii ya sasa imefeli inapromote kupata wezi, wabinafsi, wanufaika wachache, tutaendelea tu pale tu ambapo walipa kodi watakuwa na nguvu ya kuamua matumizi ya Kodi kwenye vipaumbele vyao na sio watawala vipaumbele vya watawala.Nchi inapogeuzwa ni shamba binafsi la wapigaji wachache na familia zao plus wapambe hayo maendeleo yatoke wapi.Kodi inataka ikachochee uzalishaji na sio pasipotija.
 
Au hata kujenga viwanda vya KIMATAIFA. Mfano korosho, hakuna kiwanda cha kimataifa Tanzania cha kuprocess korosho. Au viwanda vya mafuta ya kupikia etc. Ni small scale manufacturing ya watu binafsi. Issue ya ndege ilikuwa ni investment yenye makosa sana. Tunge-invest katika vitu ambavyo vitalera ajira, na kuingizia pesa kupitia exports. Na hio sio shida, TATIZO NI PALE AMBAPO MTU UMEKOSEA LAKINI HAUKUBALI KWAMBA ULIKOSEA. Hapo ndio tatizo lililopo sasa hivi. Mungu awaondolee hilo tatizo viongozi wetu. WAONE WANAPOKOSEA, NA WAJIREKEBISHE. Otherwise, hali itazidi kuwa mbaya tu kwa waTz na nchi kwa ujumla.
Ni heri ya mtu anaejifunza tokana na makosa ya wengine kuliko mtu arudiaye makosa yaleyale yaliyofanywa na wengine huku matokeo yakijulika.
Hakuna mtu anaeweza jua KILA kitu lzm ataanguka bahati mbaya hasara inakuwa ya Jamii nzima
 
Nani ana mshara mnono hapa?
Common peoples wana discuss uchumi tu..gafla umekuwa emotional.. grow up man.

Tume politicize uchumi.. tumepoliticize investment. Hii ndio failure namba 1.
Lazima turud nyuma tu modify economy stategies or investors watagoma kabisa kuja kuwekeza kwa policy zetu
Ni ngumu Sana kusonga kwa kupractice uchumi wa kijamaa Zama zimebadilika sana
 
Nani wa kuimplent technology nchini Kama sio mamlaka husika.
Private sector toyota ni kampuni ya serikañi?

Umaskini wa Afrika chanzo kikuu saturados tegemezi sana kwa serikali hadi wanakera ungesema hivi nchi za wenzetu wangekuzaba makofi
 
Private sector toyota ni kampuni ya serikañi?

Umaskini wa Afrika chanzo kikuu saturados tegemezi sana kwa serikali hadi wanakera ungesema hivi nchi za wenzetu wangekuzaba makofi
Mifumo yao ipo vizuri ni mifumo wezeshi ya kuinua watu na sio ya kuwafanya watu wawe masikini ili watawaliwe Kama huku kwetu.
Huku nchi ni Mali binafsi ya mtawala kwao nchi ipo mikononi mwa wananchi.
Sera mbovu uleta umasikini na kuuwa vipaji.
 
Uvivu tu mbona Akina Mengi akina Bakheresa akina Mo Dewji mbona mabiñionea kwenye mifumo hii hii?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom