Wa kulaumiwa ni sisi wenyewe.
Unapozaa watoto watatu au wa nne, kama gharama za kulea mtoto mmoja ni wastani wa Tsh mil 2 kwa mwaka; kwa miaka 30 huyo mtoto atakugharimu milioni 60.
Mchina mwenye mtoto mmoja atagharimika milioni 60, kulea.
Mzungu mwenye watoto wawili atagharimika mil 120 kulea.
Mbongo mwenye watoto watatu atagarimika mil 180 kulea
Na Mtz mwenye watoto wanne atagharimika mil 240 kulea.
Kwa hiyo, sio kwamba wachina na wazungu wametuzidi utajiri, No! Wanapata unafuu wa maisha hivyo kuokoa pesa nyingi kwa kujenga familia ndogo ndio maana wanaweza kununua magari mazuri na hata kufanya utalii.
Afrika itaweza kuondokana na umaskini endapo tu, familia zitajikita kwenye kuzaa mtoto mmoja hadi wawili.
Tofauti na hapo, wazazi wengi wenye watoto wengi watakufa masikini kwa kuwa fedha zao nyingi zimeenda kwenye kulea familia.