Umaskini wa nchi yetu nani alaumiwe?

Umaskini wa nchi yetu nani alaumiwe?

Nyerere.
Angeacha wakoloni waendelee kututawala.
Sisi kujitawala hatuwezi.
 
Ule ule ubinafsi na unafiki. Mtu akila akashiba na familia yake nyie hata mkifa shari yenu.
Hii mbegu imepandwa kwenye kizazi cha Y2K kuja mbele na majibu tunayaona.
Sasa hivi hadi mvua ikinyesha wanaamshukuru Rais[emoji23][emoji23][emoji174]
Viongozi Mungu atawalipa aisee[emoji23][emoji23][emoji23]

Wamekaa wanakula hela,huku wakitembelea magari makali Kwa fedha za wavuja jasho..
Ila mtu hosp anakufa Kwa kukosa pesa ya kulipiwa matibabu.

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
 
Siyo kweli walifanya ya wakati wao Sasa mbona wameshaondoka kea Nini hatuendelei? Huoni Kama Kuna shida?
Wameeondoka wameacha vizazi vyao ndio vinalamba asali hata kesho,walitengeneza misingi bora ya familia zao hazina shida japo awapo.
Hakuna mtawala anaekuwazia wewe,usipopambana na hali yako imekula kwako.
 
Wadau nawasalimu Kwa jina la jamhuri ya muungano wa tanzania. Kazi inaendelea.

Kichwa cha habari chausika. Naenda moja Kwa moja kwenye mada.

Nawaza Sana hivi ni kwanini tangu tumepata Uhuru 1961 mpaka leo neno umaskini ndo kibwagizo chetu?

Na mpaka leo tunaongea Maji Safi kijijini, shule havina vyoo, Uhuru tuliopata umetusaidia Nini Kama nchi? Mbona mimi sielewi tuliopata Uhuru wa kifanya Nini.

Lakini tuache hayo tangu tupate Uhuru tumeweza Nini Cha kuigwa duniani kutoka kwetu tanzania.

Tuna nini la kujivunia tuliyoweza Kila kitu hatuwezi yaani Kwa kweli nashindwa miaka yote hayo hatuna tulichoweza Cha kujivunia

Umaskini huu nani alaumiwe watanzania ni wavivu au nini kimetupata watanzania?

Tusaidiane shida iko wap karibun
Walaumiwe CCM
 
Cha muhimu wananchi watafute macho ya kuziona fursa na Sio kusubiria watawala ndo wawafumbue macho fursa zipo tele kuliko idadi ya watu. Cha msingi ni kupambana kusaka taarifa. Taarifa ndio mtaji wako. Unakuwa masikini kwa sababu we ni kipofu,huna macho uoni fursa tele zilizokuzunguka. Fursa tele zimejaa kwenye ardhi, kilimo, madini, nishati, sekta ya ujenzi, uvuvi. Kwa maana popote penye watu pana pesa ni wewe tu kujua nini wanataka
 
T

Tunalipa Kodi kwa ajili ya Nini na unadhani watanzania hawapambani kuondokana na umaskini
 
Mambo matatu yamesababisha umaskini nchini Tanzania:
1. Falsafa ya uchumi. Hii ndio sumu kali iliolifanya taifa kuwa maskini mpaka leo. Watu wamelemaa kutokana na falsafa hii.
2. Elimu. Mfumo elimu ni mzigo mzito ulioshindwa kusaidia raia kuondokana umaskini. Elimu yetu haimsaidii mtu kutambua fursa zilizopo zinazo weza kumwondoa katika umaskini. Matumizi ya kingereza kama lugha ya kufundishia watoto wetu imekuwa ndio sababu ya wanafunzi wengi kumaliza shule bila elimu.
3. Viongozi. Kuwa na viongozi wasio kuwa na maono ndio sababu ya nchi kubaki maskin. Kwa bahati mbaya tangu uhuru hatujawahi kuwa na viongozi wenye maono kuhusu uchumi. Utaratibu wa kuweka viongozi kwa kujuana utaendelea kuligharimu taifa.
 
T

Tunalipa Kodi kwa ajili ya Nini na unadhani watanzania hawapambani kuondokana na umaskini
Maendeleo binafsi bado ni jukumu la mtu binafsi kuwa na macho ya kuzichangamkia fursa zinazomzunguka.Afrika watawala uwafanya wananchi wawe masikini Ili iwe rahisi kwao kuwatawala.So usipopambana binafsi kupata basic needs imekula kwako.
Ukitoka wakumbuke kuwatoa pia wanaokuzunguka
 
Wadau nawasalimu Kwa jina la jamhuri ya muungano wa tanzania. Kazi inaendelea.

Kichwa cha habari chausika. Naenda moja Kwa moja kwenye mada.

Nawaza Sana hivi ni kwanini tangu tumepata Uhuru 1961 mpaka leo neno umaskini ndo kibwagizo chetu?

Na mpaka leo tunaongea Maji Safi kijijini, shule havina vyoo, Uhuru tuliopata umetusaidia Nini Kama nchi? Mbona mimi sielewi tuliopata Uhuru wa kifanya Nini.

Lakini tuache hayo tangu tupate Uhuru tumeweza Nini Cha kuigwa duniani kutoka kwetu tanzania.

Tuna nini la kujivunia tuliyoweza Kila kitu hatuwezi yaani Kwa kweli nashindwa miaka yote hayo hatuna tulichoweza Cha kujivunia

Umaskini huu nani alaumiwe watanzania ni wavivu au nini kimetupata watanzania?

Tusaidiane shida iko wap karibun
Walaumiwe waTanganyika.
 
Binafsi ninaamini sababu za umasikini wa Taifa letu ni za kiroho chanzo chake ni mwalimu Nyerere. Mwalimu alipokabidhiwa uhuru kutoka kwa wazungu, yeye aliingia mikataba na mizimu (mashetani) kwa namna mbalimbali. Kwa mfano fuatilia ile orodha ya "wazee" waliozindika taifa pamoja na yeye. Kuna kile kikao cha "wazee wa Dare salaam" ambacho hufanyika hata sasa kiliasisiwa na yeye na kiukweli wazee hawa ni wachawi asilimia mia moja. Huyu mzee aliamini sana nguvu za giza na hata kutembea na kafimbo kalikoaminika ni ka kichawi. Alipokuwa nyumbani kwao Butiama ilikuwa ni mitambiko kila kukicha. Wazee wa kimila na mama yake mzazi waliongoza kufanya ibada kwa mashetani na kisha mambo hayo yote yakaharibu baraka zote za Mungu alizotukirimia. Mfano mwingine wa mambo ya kishirikina aliyoyaanzisha mwalimu ni pamoja na kukimbiza moto (mwenge) nchi nzima. Nk Nk

Cha kufanya: tupate watu waliojitoa kikamilifu kwa Mungu waongoze maombi ya Taifa zima kwa ujumla, maombi ya toba na kujitakasa, tuombe rehema kwa Mungu atusamehe atupe neema ya kuanza upya na Yeye. Katika maombi haya tutapigana na adui aliyeshikilia rasilimali zetu hata sisi kushindwa kunufaika nazo. Yako mengi ya kusema hapa. Ila nimeona niseme hilo (in a nutshell) then tuchakate kama vipi tuingie kazini fasta. Haiwezakani baraka zetu zikaliwe na adui miaka nenda rudi HAIWEZEKANI!!!!!!!

YESU KRISTO NI BWANA NA MWOKOZI
 
J
Maendeleo binafsi bado ni jukumu la mtu binafsi kuwa na macho ya kuzichangamkia fursa zinazomzunguka.Afrika watawala uwafanya wananchi wawe masikini Ili iwe rahisi kwao kuwatawala.So usipopambana binafsi kupata basic needs imekula kwako.
Ukitoka wakumbuke kuwatoa pia wanaokuzunguka
Je kodi tunayolipa kwa serikali in faida gani kama serikali haiwezi kubadili maisha ya watu wake
 
Je population ya nchi hizo Kwa square kilometer ni watu wangap. Acha kutudanganya hakuna kitu Kama hicho Africa siyo populated Kama Europe na Asia na marekani
Sijazungumzia kuhusu population. Nimezungumzia family size. Unaweza kuwa na familia 10 zenye members wanne. Jumla watu 40.
Pia unaweza kuwa na familia nne zenye members 10 jumla watu 40.
 
Wadau nawasalimu Kwa jina la jamhuri ya muungano wa tanzania. Kazi inaendelea.

Kichwa cha habari chausika. Naenda moja Kwa moja kwenye mada.

Nawaza Sana hivi ni kwanini tangu tumepata Uhuru 1961 mpaka leo neno umaskini ndo kibwagizo chetu?

Na mpaka leo tunaongea Maji Safi kijijini, shule havina vyoo, Uhuru tuliopata umetusaidia Nini Kama nchi? Mbona mimi sielewi tuliopata Uhuru wa kifanya Nini.

Lakini tuache hayo tangu tupate Uhuru tumeweza Nini Cha kuigwa duniani kutoka kwetu tanzania.

Tuna nini la kujivunia tuliyoweza Kila kitu hatuwezi yaani Kwa kweli nashindwa miaka yote hayo hatuna tulichoweza Cha kujivunia

Umaskini huu nani alaumiwe watanzania ni wavivu au nini kimetupata watanzania?

Tusaidiane shida iko wap karibun
Unafanya kazi nyepesi sana ya kuhoji, kuna wanaofanya kazi ngumu ya kivitendo ya kupambana na umaskini.

Hata mataifa tajiri kama USA na yale ya Ulaya yana watu wenye kufanya kazi nyepesi kama hii ya kwako.
 
Hapana nchi za Asia tuna umri saw na sisi na walikuwa utumwani sawa na sisi lakini Leo wako mbali mfano Malaysia na Singapore na China yenyewe hatujafanya kitu kuchukia umaskini
China ni magiant kwa umri wake hata wazungu hawafikii, amefanya mambo makubwa huko kale,
 
Kufeli au kushindwa Inabidi usitafute mtu wa kumlaumu bali inabidi tujilaumu sisi wenyewe kwa kutokuwa na uwajibikaji mzuri wa kufanya kazi na kuona fursa katika taifa letu
 
Sasa hivi hadi mvua ikinyesha wanaamshukuru Rais[emoji23][emoji23][emoji174]
Viongozi Mungu atawalipa aisee[emoji23][emoji23][emoji23]

Wamekaa wanakula hela,huku wakitembelea magari makali Kwa fedha za wavuja jasho..
Ila mtu hosp anakufa Kwa kukosa pesa ya kulipiwa matibabu.

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
Mtu anakufa kwa kukosa elfu 20 at the same time kuna mtu ana transfer billion 5O kwenda uswisi
 
Back
Top Bottom