Wasichokijua mapependekezo ya IMF, WB na Washington Consensus yamesababisha nchi nyingi zinazoendelea kukwama mpaka leo tangu economic liberalization iliyofanyika miaka 1980s, tumekuwa tegemezi zaidi.
China walifanya mageuzi ya kiuchumi lakini WALIKUWA hawataki kabisa kufuata ushauri wa IMF na WB
Thailand iliwalazimu kuachana na mapendekezo ya IMF baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya mwaka 1997 kwenye financial crisis ya asia
Wakati Korea Kusini ikiwa masikini kama sisi miaka 1960s, waliomba mkopo World Bank kwa ajili ya kuunda kiwanda cha chuma, WB ikagoma ikasema nchi maskini kama korea kusini haina uwezo wa kuendesha mradi huo huku wakionyesha nchi zilizo feli kama Brazil wakati huo kwenye chuma
Jamaa wakapata msaada wa pesa kutoka Japan kama faini ya unyanyasaji kipindi cha ukoroni, hela yote ikapelekwa kutengeneza kiwanda cha chuma kinaitwa POSCO, leo hii POSCO ni kiwanda cha sita duniani kwa uzalishaji wa chuma duniani na mpaka miaka ya 80 kiwanda kilianza kutengeneza faida kubwa
Korea Kusini na Taiwan hazikufuata ubepari kama vile inavyoelezewa na USA.
Walikuwa wanachanganya sera za kijamaa na kibepari, ndio maana asia utakuta viwanda vinavyomilikiwa na serikali pia